Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia tarehe 18 mwezi huu kilitoa pendekezo la makubaliano ya kusimamisha mapigano ya mgogoro wa mashariki ya kati kwa Israel. Pamoja na wasuluhisho wa kimataifa kuingilia kati mgogoro huo hatua kwa hatua, hivi sasa mgogoro kati ya Israel na Lebanon umeingia katika kipindi kipya ambacho nchi mbili zinafanya mazungumzo huku zikipigana. Wachambuzi wanasema, wakati wa kusimamisha mapigano hayo utategemea malengo ya kijeshi na kisiasa inayotaka kutimiza Israeli, kwa kuwa Israeli ina ubora wa nguvu ya kijeshi na imepata mafanikio katika mapigano.
Waziri wa mambo ya nje wa Israeli Bi. Tzipi Livni tarehe 18 alipokuwa na mazungumzo na tume ya Umoja wa Mataifa inahyoshughulikia utatuzi wa migogoro alisema, Israel inakubali usuluhishi wa kimataifa, lakini kuanza kwa mchakato wa usuluhishi wa kidiplomasia hakumaanishi kutanguliza kukomesha vitendo vyake vya kijeshi au kupunguza vitendo vya kijeshi. Ofisa wa jeshi la Israel alisema, Israel haitaki kusimamisha mashambulizi ya kisilaha kabla ya kutimiza lengo kuu lake la kukomesha tishio la kijeshi la chama cha Hezbollah. Habari kutoka jeshi la Israel zinasema, udondoshaji wa mabomu unaofanywa na ndege za kivita umeteketeza 50% ya nguvu ya kijeshi ya jeshi la chama cha Hezbollah, lakini kutaka kutimiza lengo la kijeshi lililowekwa bado kutahitaji wiki moja.
Wachambuzi wanasema, Marekani ni nchi yenye ushawishi mkubwa zaidi kwa Israel, hivyo mwelekeo wa mgogoro kati ya Lebanon na Israel unahusiana sana na msimamo wa Marekani. Tokea kuzuka kwa mgogoro huo, Marekani inachukua msimamo wa kujiepusha nao, na haitaki kuuingilia kwa haraka. Wachambuzi walisema, Marekani ina mawazo mawili kuhusu mgogoro kati ya Lebanon na Israel. Kwa upande mmoja, Marekani inatumai kutoa pigo kwa chama cha Hezbollah kwa kutumia mikono ya Israel ili kuzitishia Syria na Iran; Kwa upande mwingine haitaki kuona mgogoro huo unaingia hatua isiyoweza kudhibitiwa na kuvuruga mipango ya kimkakati ya Marekani, kwa kuwa masuala mawili muhimu ya Iran na Iraq bado hayajatatuliwa. Jambo lingine muhimu zaidi ni kuwa Marekani haitaki mashambulizi ya Israel kudhoofisha utawala wa serikali ya hivi sasa ya Lebanon, ambayo nguvu kuu ya kisiasa inaipinga Syria. Tarehe 18, rais Bush alisema tena, "kuna haja ya kuepusha kuanguka kwa serikali ya Lebanon."
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleezza Rice tarehe 18 alisema, Lebanon na Israel haziwezi kufikia usimamishaji mapigano bila kuwa katika wakati mwafaka, na yeye atafanya ziara katika mashariki ya kati katika "mazingira yanayofaa". Hivi sasa ziara ya bibi Rice ya kutembelea mashariki ya kati imekuwa alama muhimu ya mwelekeo wa mgogoro kati ya Lebanon na Israel. Habari zinasema huenda bibi Rice atatembelea sehemu ya mashariki ya kati mwishoni mwa wiki hii. Wachambuzi wanasema, siku ya ziara ya bibi Rice huenda ni wakati wa kupungua kwa mashambulizi ya kijeshi ya Israel, kwani Marekani haitaki kuwapa watu picha ya Marekani kutopata mafanikio yoyote.
Hivi sasa Israel imetoa masharti ya kusimamisha mapigano kwa Lebanon, yaani kuwaachia huru askari wa Israel waliotekwa nyara; chama cha Hezbollah kiache kuishambulia Israel; Jeshi la chama cha Hezbollah liondoke kusini mwa Lebanon na kuacha jeshi la serikali ya Lebanon liingie kwenye sehemu hiyo. Hivi sasa mgongano hasa kati ya Israel na kikundi cha utatuzi migogoro cha Umoja wa Mataifa ni kama ifuatavyo: Kwanza, Israel inataka askari wa Israel waliotekwa waachiwe huru kabla ya kusimamisha mapigano; Pili, kutekeleza kwa ukamilifu azimio No. 1559 la Umoja wa Mataifa, kuacha jeshi la serikali ya Lebanon liingie kwenye sehemu ya kusini mwa nchi hiyo, na kuvunja jeshi la chama cha Hezbollah. Dalili zinaonesha kuwa Israel imeanza kulegeza msimamo wake kuhusu suala la pili. Waziri wa mambo ya nje wa Israeli Bi. Tzipi Livni tarehe 18 alidokeza kuwa Israel haipingi Umoja wa Mataifa kupeleka jeshi la kimataifa la kulinda amani kusaidia jeshi la serikali ya Lebanon kudhibiti sehemu ya kusini mwa Lebanon. Endapo jeshi la serikali ya Lebanon litawaweka askari mara moja kwenye mpaka kati ya Lebanon na Israel, Israel inakubali kuahirisha muda wa kuvunja jeshi la chama cha Hezbollah. Wachambuzi wanasema, huenda Israel itashirikiana na Marekani kuitaka jumuiya ya kimataifa ipange hatua halisi za kulivunja jeshi la chama cha Hezbollah baada ya kumalizika kwa mgogoro.
|