Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-19 20:53:19    
Mapishi ya vipande vya doufu na samaki

cri

Mahitaji

Samaki mmoja, doufu gramu 200, pilipili hoho gramu 20, chumvi gramu 5, M.S.G gramu 5, sukari gramu 5, vipande vya tangawizi na vitunguu maji kila kimoja gramu 5, pilipili manga gramu 1, sosi ya kambamti gramu 5, yai moja, mvinyo wa kupikia gramu 20, mafuta gramu 100, maji ya wanga gramu 5, supu kiasi kidogo.

Njia

1. ondoa vitu vilivyoko ndani ya samaki, osha samaki halafu mkate awe vipande, mweke kwenye bakuli tia chumvi, mvinyo wa kupikia, pilipili manga, M.S.G, korogakoroga, halafu tia ute wa yai na maji ya wanga.

2. mimina supu kwenye sufuria, tia doufu, korogakoroga, baada ya kuchemka, ipakue. Chemsha maji, baada ya kuchemka, tia vipande vya samaki, mpaka viive halafu vipakue.

3. pasha moto tena, tia mafuta kwenye sufuria yachemsha mpaka yawe na joto la nyuzi 60, tia pilipili hoho, vipande vya tangawizi, vitunguu maji, sosi ya kambamti, korogakoroga, mimina supu, tia M.S.G, sukari, mvinyo wa kupikia, doufu na vipande vya samaki, korogakoroga polepole, mimina maji ya wanga, halafu pakua. Tia vipande vya vitunguu maji.

4. pasha moto tena, tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi 70, pakua na uiweke kwenye samaki. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.