Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-24 14:40:03    
Mandhari nzuri ya sehemu ya Magenge Matatu yavutia watu zaidi

cri

Ujenzi wa Boma kubwa la Magenge Matatu kwenye Mto Changjiang nchini China umekamilika, ambapo kiwango cha maji kwenye Bwawa la Magenge Matatu kimeinuka na kufikia mita 135, hivyo bonde hilo kubwa ni bonde pekee linaloweza kuwawezesha watalii kupanda meli kuangalia mandhari, ni bonde linalowavutia zaidi watalii.

Mto Changjiang ambao chanzo chake kinatoka Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet una vipengele vingi, unapotiririka hadi mji wa Zhongqing na kwenye sehemu ya mkoani Hubei, ukaumbika kuwa Magenge Matatu yaani bonde kubwa lenye urefu wa kilomita 200. Ujenzi wa Mradi wa maji wa Magenge Matatu ulioanzia miaka 12 iliyopita umekifanya kiwango cha maji kwenye Bwawa la Magenge Matatu kiinuke kwa jumla, ambapo sehemu zilizo juu ya Boma kubwa zimekuwa bwawa refu lililo kama mto. Baada ya kulimbikizwa kwa maji, upana wa usawa wa mto katika sehemu nyingi umeongezeka mara mbili, umeonekana kama ni ziwa kubwa lililoko katikati ya magenge ambalo linapendeza sana.

Naibu mkurugenzi wa Idara ya utalii ya Yichang mkoani Hubei Bwana Gao Chao alisema mwezi Juni mwaka huu, malimbikizo ya maji kwenye Bwawa la Magenge Matatu yalifikia mita 135, baada ya hapo, sehemu zenye vivutio vya utalii kwenye kando za Magenge Matatu kimsingi hazikuzama majini, badala yake vipengele vya mto vimeongezeka kwenye sehemu ya Magenge Matatu, ambapo visiwa vingi vimetapakaa kote na kuongeza mandhari nzuri ya kuvutia. Alisema:

Zamani Magenge Matatu yalisifiwa kuwa ni magenge marefu yaliyosimama kidete kwenye Mto Changjiang. Lakini baada ya kulimbikizwa kwa maji kwenye bwawa, mtiririko wa maji imepungua nguvu, na maji yamekuwa safi zaidi, hivyo watu wanaweza kuona kuwa Magenge Matatu kama yanasimama kidete kwenye ziwa kubwa, ambapo mandhari ya Magenge Matatu inaonekana ni nzuri zaidi kuliko zamani.

Bwana Gao alisema, kwa kuwa Magenge Matatu yako kwenye mwinuko wa zaidi ya mita elfu moja kutoka usawa wa bahari, hivi sasa kiwango cha maji ndani ya bwawa kimeinuka, ingawa kwenye sehemu hiyo mtiririko mkali wa maji ya mto ulio wa zamani umetoweka, lakini mandhari ya Magenge Matatu yanayosimama kidete kwenye ndani ya bwawa bado ni nzuri inayowavutia watu. Na sehemu ya Yichang ya Magenge Matatu ni sehemu inayowawezesha zaidi watalii waangalie mandhari ya Magenge Matatu yaliyoko kwenye mto, ambapo watalii wanaweza kujiburudisha katika sehemu yenye mandhari nzuri ya mto na milima.

Katika sehemu ya Magenge Matatu kuna kijito cha Shennong kinachojulikana sana. Kijito hicho kina urefu wa kilomita 60, kando mbili za kijito ni miamba mikali na mirefu, vivuli vya milima na miti vinaonekana kwenye usawa wa kijito, maji yanaonekana ni safi zaidi. Sehemu nyembamba zaidi kwenye Kijito cha Shennong haifikii mita 5, ambapo watalii wanaweza kupanda mashua kutembelea kwenye kijito hicho, na wanaweza kujihisi kama wamezingirwa na milima na miti ya kijani, sehemu hiyo kuna hewa safi na hali ya utulivu zaidi, milio ya ndege inasikika kwa mbali, ama sauti ya wimbo wa kutia moyo unaoimbwa na wafanyakazi wanaovuta mashua kwa kamba, ambapo watalii wataona kama wako katika sehemu iliyoko mbali na dunia.

Mwongozaji wa utalii wa Shirika la utalii wa kimataifa la China Bi.Wang Yuan alifahamisha kuwa, kwa kweli kwenye sehemu ya Magenge Matatu, kuna vijito zaidi ya 10 kama kijito cha Shennong, kabla ya kulimbikizwa kwa maji kwenye Bwawa la Magenge Matatu, meli za watalii hazikuweza kuingia kwenye sehemu zenye kimo kirefu cha vijito hivyo. Hivi sasa Bwawa la Magenge Matatu limelimbikizwa maji, meli za watalii zinaweza kuingia huko, na watalii wanaweza kutazama mandhari ya ajabu zaidi ya huko. Bi. Wang alisema miongoni mwa vivutio vipya vya Magenge Matatu, kupanda meli kutembelea kwenye vijito kutawavutia zaidi watalii. Bi.Wang alisema:

Watalii wakitaka kutembelea kwenye kijito wanapaswa kupanda mashua madogo ya mbao inayovutwa kwa kamba au mianzi, ambapo mashua ya mbao inayosonga mbele karibu inakwaruza mawe chini ya kijito, kwani kimo cha maji cha kijito ni kifupi. Watu wakikaa kwenye mashua ya mbao, wanapoangalia mandhari ya maumbile, wanaweza kujihisi wako karibu sana na dunia ya maumbile.

Kwa kweli kuanzia miaka ya 90 ya karne iliyopita, kutokana na kuanzishwa kwa ujenzi wa mradi wa Magenge Matatu, sehemu ya Magenge Matatu ya Mto Changjing inajulikana sana, na watalii wengi kutoka nchini na ng'ambo walikwenda kwenye sehemu hiyo kutalii. Mwaka 2005 tu vivutio vya Magenge Matatu ya Mto Changjiang viliwavutia watalii laki 2 kutoka nchi za nje, na vimekuwa sehemu muhimu nchini China ya kuwavutia watalii kutoka nchi za nje.

Mhusika wa Idara ya kazi ya mawasiliano katika shirika kuu la utalii wa kimataifa la China Bwana Huang Jie alisema, kutokana na kupanda kwa juu kwa kiwango cha maji kwenye Magenge Matatu, watalii wengi kutoka nchi za nje wanapenda zaidi kutalii kwenye sehemu ya mtiririko wa juu wa Mto Changjiang katika majira ya siku za joto. Alisema:

Tumeandaa safari fupi ya kwenda Yichang mkoani Hubei kutoka Zhongqing mkoani Sichuan, ambapo watalii wanaweza kupanda meli kufanya utalii, vivutio vya kando mbili za Mto Changjiang vinawavutia zaidi watalii kutoka nchi za nje.

Hivi sasa Bwawa la Magenge Matatu bado liko katika kipindi cha kulimbikizwa maji kwa hatua ya mwanzo. Ifikapo mwaka 2009 wakati ujenzi wa mradi wa Magenge Matatu utakapokamilika, kiwango cha maji cha Bwawa la Magenge Matatu kitainuka na kufikia mwinuko wa mita 175 kutoka usawa wa bahari, ndipo mandhari ya Magenge Matatu itapendeza zaidi.

Naibu mkurugenzi wa Idara ya utalii ya Yichang mkoani Hubei Bwana Gao Chao anaona kuwa, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Magenge Matatu, miamba mirefu ya magenge makubwa itapatana zaidi na bwawa lililo kama ziwa kubwa lenye mawimbi tulivu, ambapo watalii wa nchini na nje wataona mvuto mkubwa wa sehemu hiyo ya Magenge Matatu ya Mto Changjiang. Alisema:

Magenge Matatu ya Mto Changjiang daima ni yenye hali ajabu ya miujiza, mabadiliko yake mazuri yatawavutia zaidi watalii. Ni matumaini yetu kuwa watalii kutoka nchi za nje watavutiwa zaidi na Boma kubwa la Magenge Matatu, sehemu zenye mandhari nzuri ya kimaumbile na utamaduni wa Magenge Matatu. Tutatoa huduma nzuri zaidi na kupanga mpango mzuri zaidi ili watalii waweze kupata picha mpya na burudani mpya kila wakifika kwetu kutalii.

Idhaa ya kiswahili 2006-06-24