Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-25 15:33:02    
China yajenga mfumo kamambe wa utafiti wa sayansi ya kilimo

cri

Waziri wa kilimo wa China Bw. Du Qinglin tarehe 6 mwezi Julai alisema, baada ya maendeleo katika miaka 50 iliyopita, hivi sasa China imeshajenga mfumo kamambe wa utafiti wa kilimo duniani.

Bw. Du Qinglin katika mkutano wa taifa wa uvumbuzi wa teknolojia ya kilimo alisema, hivi sasa nchini China kuna vituo zaidi ya 1,200 vya utafiti wa teknolojia ya kilimo vyenye wafanyakazi zaidi ya elfu 120 pamoja na vituo laki 1.55 vya uenezaji wa teknolojia ya kilimo vyenye wafanyakazi milioni 1.03.

Bw. Du Qinglin alisema utafiti wa sayansi ya kilimo na uenezaji wa teknolojia ya kilimo vimetoa mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya kilimo ya China, hususan kwa vituo vya utafiti wa sayansi ya kilimo katika ngazi mbalimbali vilivyofanya kazi muhimu sana za kuhimiza uvumbuzi wa teknolojia ya kilimo na kuhimiza maendeleo ya kilimo katika vipindi mbalimbali katika historia. Katika miaka mingi iliyopita, vituo vya utafiti wa sayansi ya kilimo vya serikali kuu na mikoa ilipata mafanikio mengi katika utafiti wa sayansi ya kilimo.

Lakini pia alisema, hivi sasa kuna maswala mengi yanayohitaji kutatuliwa kwa haraka kati ya utaratibu wa utafiti na uenezaji wa sayansi ya kilimo na kuharakisha uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ya kilimo, hususan kuweko kwa vituo vingi vya namna moja, ambayo vinafanya utafiti unaofanana, mafanikio machache kutokana na kuweko ushindani mkubwa kupita kiasi, mambo ya utafiti wa sayansi hayaendani na mahitaji ya wakulima, na kuondoka kwa wingi mafundi waenezaji wa teknolojia ya kilimo.

Hivi sasa nchini China, ingawa mchango unaotolewa na maendeleo ya teknolojia ya kilimo umefikia 48% hivi, lakini bado uko mbali sana ikilinganishwa na ule wa kiasi cha 81%, ambayo 85% yake yanatumika katika uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Bw. Du Qinglin alisema, tukitaka kutatua masuala hayo, hatuna budi kuharakisha ujenzi wa mfumo wa uvumbuzi wa teknolojia ya kilimo, na kuendeleza kwa undani zaidi mageuzi ya mfumo wa sayansi na teknolojia ya kilimo. China itaimarisha vituo vya utafiti wa sayansi ya kilimo vya serikali kuu na vya mikoa, pamoja na ujenzi wa miundo-mbinu ya utafiti wa sayansi ya vyuo vikuu inayohusika na kilimo, kuunda kundi jipya la watafiti na ujenzi wa utamaduni wa uvumbuzi ili kukuza uwezo wa wakulima wa uvumbuzi wa teknolojia, uvumbuzi wa sayansi ya wataalamu na uvumbuzi katika kutumia zana za kilimo zilizoagizwa kutoka nchi za nje.

Alisema China itajitahidi kukamilisha mfumo mpya wa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia wa ngazi ya taifa kwenye vituo vilivyopangwa kwenye sehemu mbalimbali nchini, uwezo kamili, ufanisi mkubwa, na ni imara ili kutoa uungaji mkono wa kielimu na kiteknolojia kwa kilimo cha kisasa ifikapo mwaka 2020, ambapo kiasi cha mchango utakaotolewa na maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kilimo cha China kitainuka na kufikia 63%.

Idhaa ya kiswahili 2006-07-25