Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-26 18:38:13    
Kauli ya "mashariki ya kati ya aina mpya" ya Rice inalenga nini?

cri

 

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice tarehe 25 alifanya ziara ya siku moja nchini Israel na Palestina. Katika mazungumzo yake na viongozi wa Israel na Palestina, Rice alitoa kauli moja kuhusu "mashariki ya kati ya aina mpya", kauli hiyo imewavutia watu macho.

Alipozungumza na waziri mkuu wa Israel Bwana Ehud Olmert, Bi. Rice alisema, "Wakati wa kuanzisha mashariki ya kati ya aina mpya umewadia", hakika "watu fulani wanajaribu kuiangamiza Lebanon yenye demokrasia na mamlaka ya uhuru ndani ya susu, hivi sasa lazima tuzioneshe nguvu zile ambazo hazitaki kuona mashariki ya kati ya aina mpya kuwa, watakaopata ushindi wa mwisho ni sisi. Na alipokuwa na mazungumzo na mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw Mahamoud Abbas, Bi Rice alisema, Marekani inatumai kutimiza "amani ya kudumu", ili kuzuia vita visitokee tena.

Wachambuzi wamedhihirisha kuwa, tokea mgogoro kati ya Lebanon na Israel uibuke, Marekani ikiwa nchi kubwa yenye ushawishi mkubwa zaidi katika sehemu ya mashariki ya kati, siku zote ilikuwa ikiziacha pande hizo mbili zipambane, hata kuichochea Israel ifanye mashambulizi mara kwa mara dhidi ya Lebanon, hadi baada ya wiki mbili, waziri wa mambo ya nje Rice akahimizwa na jumuiya ya kimataifa kwenda mashariki ya kati kufanya usuluhisho. Alipotembelea sehemu za Palestina na Israel, hakuihimiza Israel kwa nguvu iache vitendo vya kijeshi, na kukomesha vita kwenye sehemu ya mpaka kati ya Lebanon na Israel, bali alisisitiza tu ulazima wa kuanzisha ati "mashariki ya kati ya aina mpya", kidhahiri, lengo lake hasa ni kutumia fursa ya mgogoro kati ya Lebanon na Israel kutekeleza mikakati yake ya mashariki ya kati na kujenga upya utaratibu mpya wa mashariki ya kati.

Kwanza, Israel kupambana na chama cha Hezbollah cha Lebanon, kitendo hiki kinalingana na mikakati ya Marekani ya kujenga demokrasia ya sehemu kubwa ya mashariki ya kati. Baada ya kuuawa kwa Bwana Hariri aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon, nguvu inayopendelea magharibi imeongoza kwenye jukwaa la Lebanon, na Marekani pia inaichukulia Lebanon kuwa chesi moja kubwa kwenye mpango wake wa kuhimiza "utandawazi wa demokrasia" kwenye mashariki ya kati. Lakini nguvu ya kuipinga Marekani ya chama cha Hezbollah na makundi mengine pia ni kubwa sana, tena chama cha Hezbollah pia kina jeshi ambalo hata serikali ya Lebanon haiwezi kulidhibiti, hali hii inaifanya hali ya uwiano wa kisiasa nchini Lebanon iwe ya dhaifu sana, hivyo kubadilisha mwundo huo wa kisiasa wa Lebanon ni lengo la Marekani tangu zamani. Safari hii Israel imetoa pigo kubwa kwa chama cha Hezbollah, hii imekuwa fursa nzuri kwa Marekani kudhoofisha nguvu ya kuipinga Marekani na kuongeza nguvu ya kupendelea magharibi. Bi. Rice alipofanya ziara ya ghafla nchini Lebanon tarehe 24, alisema maneno mengi matamu kumsifu waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora, alisema ushujaa wake wa kukabiliana na mgogoro unastahili kusifiwa, kusudi lake la kumvuta linaonekana wazi.

Aidha Marekani siku zote inakichukulia chama cha Hezbollah kuwa ni wakala wa Iran na Syria katika sehemu ya mashariki ya kati, Marekani inaona kuwa, mgogoro wa hivi sasa kati ya Lebanon na Israel si kama tu ni mapambano kati ya Israel na chama cha Hezbollah, bali pia ni mapambano yasiyo moja kwa moja kati ya Marekani na Iran na Syria. Kama ikiweza kutumia fursa hii kukishinda chama cha Hezbollah, na kukidhibiti kwa kupitia utaratibu wake wa muda mrefu wa kisiasa na kidiplomasia, hakika italeta nafasi kubwa zaidi kwa Marekani kuweza kupambana na Iran na Syria. Wachambuzi wa kisiasa wa nchi za kiarabu wanaona kuwa, Marekani inataka kuanzisha "mashariki ya kati ya aina mpya isiyokuwa na chama cha Hezbollah na kundi la Hamas", na inazishinikiza nchi za kiarabu zishirikiane nayo katika mapambano dhidi ya Syria na Iran.

Zaidi ya hayo Marekani inajaribu kupitia hatua ya kutoa pigo kwa chama cha Hezbollah kutekeleza mikakati yake ya kupambana na ugaidi duniani, na kutoa onyo kwa nguvu zenye siasa kali za kuipinga Marekani duniani. Wachambuzi wanasema, kabla ya kutimiza lengo lake Marekani haiwezi kuipa Israeli shinikizo halisi kuhusu suala la kusimamisha vita na Lebanon.

Idhaa ya Kiswahili 2006-07-26