Tarehe 27 baraza la mawaziri wanaoshughulikia ulinzi ya Israel liliamua kuendelea na kiwango chake cha opresheni ya kijeshi katika sehemu ya kusini ya Lebanon na litawaandikisha askari ili kujiandaa kwa mashambulizi mengine. Wachambuzi wanaona mgogoro kati ya Israel na Lebanon umeingia siku ya siku 16, lakini ni vigumu kusema matokeo ya opresheni hiyo ni mazuri au mabaya, hasa baada ya jeshi la nchi kavu la Israel kupingwa vibaya na vikosi vya Hezbollah na kupata hasara kubwa. Hivyo mkakati wa opresheni ya jeshi la Israel nchini Lebanon umetiliwa mashaka.
Tokea tarehe 26 opresheni ya jeshi la Israel imeingia katika wiki ya tatu. Ingawa jeshi la Israel limetangaza kuwa limewaua wafuasi 150 wa chama cha Hezbollah na limeharibu makao makuu ya chama hicho huko Beirut, maghala mengi ya silaha na vituo vingi vya kurushia maroketi, lakini mashambulizi ya vikosi vya jeshi la chama cha Hezbollah kwenye sehemu ya kaskazini ya Israel hayakupungua, na opresheni ya jeshi la Israel ya "kumkata kichwa" kiongozi wa chama cha Hezbollah Hassan Nasrallah haina matokeo yoyote, zaidi ya hayo jeshi lililoingia kwenye sehemu ya kusini ya Lebanon limeonja ukali wa "vita vya msituni". Tarehe 26 kikosi kimoja cha jeshi la Israel kiliingia kwenye mtego uliotekwa na chama cha Hezbollah kwenye kijiji cha Bint Jbail ambacho kilikuwa kama ni "roho" ya chama cha Hezbollah, askari tisa wa Israel waliuawa na wengine 27 kujeruhiwa. Wachambuzi wanaona kwamba kutokana na hali ilivyo sasa, vikosi vya jeshi la chama cha Hezbollah vimetapakaa hapa na pale na vinafanya mashambulizi kwa mwendo mwepesi, na vinajitahidi kuhifadhi nguvu yake ili viweze kupambana kwa muda mrefu. Hivi sasa jeshi la Israel limedhibiti vijiji kadhaa tu kwenye sehemu ya kusini ya Lebanon, lakini kwa makadirio, jeshi la chama cha Hezbollah lina vituo kiasi cha 170 kusini mwa Lebanon.
Kutokana na hali hiyo isiyo ya kuridhisha, watu wengi wana mashaka kuhusu mkakati wa opresheni ya jeshi la Israel. Maoni ya kwanza yanasema, hivi sasa mbinu za kivita za Israel za kutumia vikosi vidogo kupambana uso kwa uso na vikosi vya chama cha Hezbollah, licha ya kutoweza kuzuia mashambulizi ya maroketi ya chama cha Hezbollah, zimeviingiza ndani ya mitego ya jeshi la chama hicho, na kufanya vita vya kupoteza nguvu visivyomalizika. Mbinu sahihi ni kupeleka jeshi kubwa na kupambana kwa nguvu kubwa dhidi ya jeshi la chama hicho moja kwa moja. Maoni ya aina nyingine tofauti yanaona kuwa kujaribu kufanya vita kwa nguvu dhidi ya vikosi vya msituni na kuvimaliza kwa haraka hakuambatani na hali ilivyo, na kupeleka jeshi kwenye sehemu ya kusini ya Lebanon kutahasarisha hali nzuri ya teknolojia ya kisilaha, na mbele ya vikosi vilivyofundishwa vizuri na havijulikani kama vinatokea wapi kwa ghafla, askari wa jeshi la Israel watapoteza uhodari wao. Mbinu sahihi ni kukusanya pamoja nguvu zote za idara za upelelezi, jeshi maalumu na nguvu za angani, jeshi maalumu linawajibika kugundua mahali vilipoficha vikosi na kuliarifu jeshi la angani na kuvishambulia kutoka angani. Na hii ina maana ya kuwa jeshi la Israel lazima lipambane "vita virefu visivyo vikali" na hatua kwa hatua.
Bw. Moshe Arens aliyekuwa waziri wa ulimzi wa Israel kwa vipindi vitatu alisema, mkakati wa jeshi la Israel ni "mbaya kabisa", lazima urekebishwe mara moja, sivyo "pengine Israel itajitoa kutoka kwenye mgogoro bila kulijeruhi jeshi la chama cha Hezbollah", na hii itakuwa ni kushindwa vibaya kwa Israel.
Kwa ufupi, watu wa Israel wametiliwa mashaka na wanazungumza sana kuhusu mkakati wa jeshi la Israel, lakini maoni karibu yote yanalenga namna ya kupiga vita hivyo, wala sio kusema kama vita hivyo vinastahili kupiganwa au la. Gazeti la Israel limesema kwamba Israel haitavumilia "sura ya kushindwa", kwani hali ya kushindwa itaathiri hadhi ya Israel katika Mashariki ya Kati.
Idhaa ya kiswahili 2006-07-28
|