Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-31 14:32:43    
Jumba la makumbusho la Henan

cri

Mkoa wa Henan ulioko katikati ya China ni moja ya chimbuko la ustaarabu wa zama za kale za China. Historia ndefu ya mkoa huo imeuachia mali nyingi za urithi wa historia na utamaduni. Takwimu zilizokusanywa zinaonesha kuwa, idadi ya mabaki ya utamaduni wa kale yaliyofukuliwa mkoani Henan ni kubwa zaidi kuliko yale yaliyofukuliwa katika mikoa mingine nchini China, na Jumba la makumbusho la Henan ni moja kati ya majumba makubwa matatu ya makumbusho ya China.

Jumba la makumbusho la Henan liko Zhengzhou, mji mkuu wa mkoa wa Henan, jumba hilo limekuwa na historia ya zaidi ya miaka 70, jengo kuu la jumba hilo lilijengwa kwa kuiga mabaki ya kituo cha unajimu kilichojengwa mapema zaidi kuliko vingine nchini China, maumbo ya jengo ni ya kawaida lakini jengo lenyewe linaonekana ni kifahari sana. Katika jumba hilo, vimehifadhiwa vitu vya mabaki ya utamaduni milioni 1.3, kiasi hicho kinachukua moja ya nane ya idadi ya jumla ya vitu vya mabaki ya utamaduni wa kale vinavyohifadhiwa katika majumba ya makumbusho ya nchi nzima ya China. Kulikuwa na watu wanaoeleza kuwa, tukizungumzia thamani ya utamaduni ya mabaki ya kale yaliyohifadhiwa katika majumba yote ya makumbusho ya China nzima, yale yaliyohifadhiwa katika Jumba la makumbusho la Kasri ya ufalme yanachukua nafasi ya kwanza, na yanayohifadhiwa katika Jumba la makumbusho la Henan yanachukua nafasi ya pili. Mkuu wa Jumba la makumbusho la Henan Bwana Ding Fuli alisema, vitu vya mabaki ya utamaduni vinavyohifadhiwa kwenye jumba hilo ni vingi vya aina mbalimbali, vingi miongoni mwake ni vyenye thamani kubwa. Alisema:

Katika Jumba la makumbusho la Henan, vitu kadhaa vya mabaki ya utamaduni wa kale ni vyenye thamani kubwa ambavyo vinaweza kuwashangaza watu, thamani yake inatia fora nchini China, na hata ni nadra kuonekana katika majumba mengine ya makumbusho nchini China. Ndiyo maana, watalii wanaotembelea mkoani Henan, kama hawatapata fursa ya kutembelea Jumba la makumbusho la Henan, watasikitika sana.

Bwana Ding alisema miongoni mwa vitu vya mabaki ya utamaduni wa kale vilivyohifadhiwa katika Jumba la makumbusho la Henan, vyombo vya shaba nyeusi ni vyenye umaalamu zaidi. Zaidi ya miaka 4000 iliyopita, China ilikuwa na ufundi wa kuyeyusha na kusubu shaba nyeusi, ambapo vyombo vya shaba nyeusi vya China vilijulikana na kung'ara duniani kutokana na ustadi mzuri wa utengenezaji wake, ambao ulikuwa ni wa kiwango cha juu. Katika zama za kale za China, vyombo vya shaba nyeusi ni alama moja ya madaraka na hadhi, ambavyo vilitumiwa mara kwa mara kuwa vyombo vyenye thamani kubwa vinavyotumiwa kwenye karamu au sherehe ya kutambika mababu katika mahekalu. Kutokana na thamani kubwa ya vyombo vya kale vya shaba nyeusi, kulikuwa na watu waliosimulia kuwa, "vyombo vya shaba nyeusi vya China vinajulikana duniani hata sawasawa na ukuta mkuu wa kale wa China.

Mkoa wa Henan ulikuwa ni kituo cha kisiasa na kiuchumi katika zama za vyombo vya shaba nyeusi za China ya kale, hivyo vyombo vingi vya shaba nyeusi vilifukuliwa katika mkoa huo, miongoni mwa vyombo hivyo, vyombo kadha wa kadha vyenye thamani kubwa zaidi vimehifadhiwa kwenye Jumba la makumbusho la Henan. Vyombo hivyo vinatafsiri utamaduni wa shaba nyeusi wa China kwa raslimali zake, maumbo ya ajabu na mistari na madoadoa yaliyochongwa kwenye vyombo hivyo, seti moja ya vinanda vya "Wang Sun Gao Yongzhong" vilivyohifadhiwa kwenye Jumba la ukumbusho la Henan ni hazina ambayo ni nadra kupatikana.

"Yongzhong" ni kinanda kikubwa cha kupiga, pia ni kinanda ambacho hakikukosekana katika sherehe za kutambika mababu zilizofanyika kwenye mahekalu katika zama za kale, na kwenye karamu kubwa zilizofanyika katika kasri la ufalme. Seti hiyo ya "Yongzhong" ilisubiwa na mtoto wa mfalme mmoja wa zama za China ya kale, alisubu seti hiyo ya "Yongzhong" ili kumkumbuka baba yake mzazi; kwenye vinanda hivyo yalichongwa maneno ya kumbukumbu, ambayo yanaweza kuthibitisha historia hiyo. Mwelezaji wa Jumba la makumbusho la Henan Bi. Liu Heng alieleza kuwa, seti hiyo ya "Yongzhong" imekuwa na historia ya miaka 2,500 hivi. Alisema:

Seti hiyo ya "Yongzhong" ilifukuliwa bila kuharibiwa hata kidogo, kwa jumla ina vinanda 26, miongoni mwake, kinanda kikubwa zaidi ni chenye uzito wa kilo 152.8, na kinanda kidogo zaidi kina uzito wa kilo 2.8, vinanda hivyo vimekuwa na sauti 7 za muziki, ambavyo vinaweza kupiga muziki wa aina mbalimbali wa zama tulizo nazo, hii ni seti moja ya vinanda vingi zaidi ambavyo vinaweza kupiga sauti za aina nyingi zaidi, vilivyotengenezwa katika Enzi ya Spring na Autumn ambavyo vilifukuliwa nchini China.

Na "Birika lenye umbo la mraba la Yungiyungi na Korongo" ni hazina nyingine yenye thamani kubwa iliyohifadhiwa kwenye Jumba la makumbusho la Henan, umbo la birika hilo likilinganishwa na seti ya vinanda vya shaba nyeusi ni dogo, kwani kimo cha birika hilo ni sentimita 12 tu, ambalo linasifiwa kuwa ni moja kati ya vyombo vya shaba nyeusi vya mashariki vinavyopendeza zaidi. Birika hilo liligunduliwa na mkulima mmoja wa Xinzheng mkoani Henan mwaka 1923 alipokuwa anachimba kisima katika bustani ya mboga ya familia yake, birika hilo limekuwa na historia ya zaidi ya miaka 2500. Kwenye sehemu ya juu ya birika hilo kuna matabaka mawili ya ua la Yungiyungi linalochanua, katikati ya ua la Yungiyungi amesimama Korongo mmoja anayetaka kuruka angani, hivyo birika hilo limepewa jina la "Birika lenye umbo la mraba la Yungiyungi na Korongo"; nje ya birika hilo kuna mapambo ya aina ya dragon na wanyama wadogo wa aina mbalimbali wanaopendeza, umbo la birika hilo ni la ajabu ambalo linawavutia sana watu. Utafiti unaonesha kuwa, chombo hicho cha shaba nyeusi kilitengenezwa katika kipindi cha mwisho cha jamii ya utumwa. Vyombo vya shaba nyeusi vilivyotengenezwa katika kipindi cha mwanzo au cha katikati ya jamii ya utumwa vingi vinaonekana ni vyenye hali ya kuzingatia utaratibu na heshima, au hali ya ukatili na hofu, lakini chombo hicho kinaonesha hali inayojaa uhai na furaha, wataalamu wanadhani kuwa, hii labda ilitokana na sababu ambayo wakati chombo hicho kilipotengezwa ulikuwa ni wakati ambapo mfumo wa utumwa ulipokaribia kwisha nchini China, hivyo chombo hicho cha shaba nyeusi pia kinachukuliwa kuwa ni chombo cha mwisho kilichotengenezwa kwa ustadi mkubwa katika "zama za vyombo vya shaba nyeusi".

Katika Jumba la makumbusho la Henan, pia kuna "jambia la chuma ambalo ndani yake ni la shaba", hilo ni jambia la chuma lililosubiwa kwa nguvu ya binadamu ambalo lilifukuliwa mapema zaidi nchini China, hivyo jambia hilo pia linachukuliwa pia kuwa ni "Jambia la kwanza la taifa la China". Mwelekezaji wa Jumba la makumbusho la Henan Bi. Liu Heng alisema, kufukuliwa kwa jambia hilo la chuma kuliwahi kuwashangaza watu wa sekta ya utafiti wa mabaki ya kale. Alisema:

Hili ni jambia la chuma lenye mkono wa jade, na ndani ya mkono huo wa jade ni shaba, na kwenye sehemu ya kiungo cha mkono na jambia pia kuna mawe ya turquoise, kabla ya miaka 2800, namna ya kusubu vitu vinne vyenye tabia tofauti vya shaba, jade, chuma na mawe ya turquoise, kweli pia lilikuwa tatizo kubwa.

Katika Jumba la makumbusho la Henan pia kuna vitu vingine vingi vya mabaki ya kale vyenye thamani kubwa sana. Jumba hilo la makumbusho linawavutia watalii wengi wa China na nchi za nje kwa utamaduni unaong'ara wa China. Mwalimu kutoka Korea ya kusini Bi.Kim Min R alisema:

Mabaki ya kale ya kihistoria yanayohifadhiwa kwenye Jumba la Ukumbusho la Henan yanasaidia sana masomo ya watoto, nikipata nafasi, nitakuja tena.

Idhaa ya Kiswahili 2006-07-31