Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-01 15:25:51    
Sheria mpya ya kamati ya usimamizi wa sekta ya bima kuanza kutekelezwa

cri

Hivi karibuni kamati ya usimamizi wa sekta ya bima ya China imetangaza "kanuni kuhusu sifa za wakurugenzi na wasimamizi wa ngazi ya juu wa kampuni za bima" na "usimamizi kuhusu wawakilishi wa kampuni za bima za kigeni nchini China", ambazo zitaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 mwezi Agosti mwaka 2006.

Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa sekta ya bima Bw. Wu Dingfu alisisitiza kuwa, katika miaka ya karibuni habari kuhusu kufilisika kwa kampuni za bima na kashfa za uhasibu zilisikika kutoka Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya na Asia, sababu kubwa zilitokana na kukosa usimamizi kwa wasimamizi wa kampuni hizo, kwani watu hao ni muhimu sana katika uendeshaji wa shughuli za kampuni.

Kanuni kuhusu sifa za wakurugenzi wa kampuni za bima kuna vitu vitatu muhimu: Kwanza ni kupanua eneo la wasimamizi wa ngazi ya juu, ambapo mhasibu mkuu atachukuliwa kuwa ni msimamizi wa ngazi ya juu, na kuona kuwa ana madaraka ya kufanya uamuzi au kuwa na athari kubwa katika uendeshaji wa shughuli za kampuni ya bima.

Pili, kuimarisha usimamizi kuhusu kazi za wakurugenzi na wasimamizi wa ngazi ya juu. Kwa mfano kuweka utaratibu wa kutoa ripoti kuhusu mambo muhimu, kampuni za bima zinatakiwa kutoa taarifa kwa wakati kwa idara ya usimamizi kuhusu mabadiliko ya kazi za wakurugenzi na wasimamizi wa ngazi ya juu, au vitendo vyao vya kukiuka nidhamu na sheria; Kuweka utaratibu wa kutoa barua za onyo kuhusu hatari zinazoweza kutokea, wakati wakurugenzi au wasimamizi wa ngazi ya juu wanapotuhumiwa kukiuka kanuni na sheria au kuwa wazembe, ambao ungeleta athari mbaya kwa kampuni, wanapewa barua za onyo au kuwa na mazungumzo nao na kuwataka wajirekebishe katika muda unaowekwa; wakurugenzi na wasimamizi wa ngazi ya juu wanatakiwa kukaguliwa kabla ya wao kuondoka madarakani.

Na tatu, ni kusisitiza uaminifu wa wakurugenzi na wasimamizi wa ngazi ya juu. Wakurugenzi na wasimamizi wa ngazi ya juu wanatakiwa kutia saini kuhusu sifa zao kwenye karatasi za ombi la wadhifa katika kampuni, na kuwajibika kuhusu ukweli wa sifa zao, na pindi wakigunduliwa kufanya udanganyifu katika kujipatia wadhifa katika kampuni, karatasi hizo zitakuwa ushahidi wa moja kwa moja wa kuthibitisha vitendo vya kukiuka kanuni. Kwa wakurugenzi au wasimamizi wa ngazi ya juu waliopata nyadhifa katika kampuni kwa njia isiyo ya haki, kamati ya usimamizi wa sekta ya bima katika ngazi mbalimbali zitakataa maombi yao ya kazi katika muda wa miaka mitatu.

"Usimamizi kuhusu wawakilishi wa kampuni za bima za kigeni nchini China" umekamilisha utaratibu wa uidhinishaji kwa kampuni za bima za kigeni zinazotoa maombi ya kuingia nchini China. Maagizo hayo yameweka wazi athari za vitendo vya kukiuka kanuni za wawakilishi kwa kampuni za bima za kigeni, na kuhimiza kampuni za bima za kigeni kuimarisha usimamizi kuhusu wawakilishi wao walioko nchini China.

"Usimamizi kuhusu wawakilishi wa kampuni za kigeni za bima nchini China" unaagiza kuwa, endapo ofisi za wawakilishi wao zimepewa adhabu zaidi ya mara 3 na kamati ya usimamizi wa sekta ya bima ya China, au kushiriki katika shughuli zinazokwenda kinyume cha sheria na kuwa na pato kubwa kutokana na shughuli hizo, ambazo zinaleta athari mbaya kwa China, kamati ya usimamizi wa sekta ya bima ya China itafikiria kwa uangalifu sifa za kampuni hizo za bima za kigeni zilizoanzisha kampuni ya bima nchini China.

Ofisi za wawakilishi wa kampuni za bima za Hong Kong, Macau na sehemu ya Taiwan pia zinatakiwa kufuata kanuni hiyo. Kanuni nyingine zilizotolewa miaka ya nyuma zikiwemo "kanuni za usimamizi wa sifa za wasimamizi wa ngazi ya juu wa kampuni za bima" zilizotolewa mwaka 2002, "Kanuni kuhusu marekebisho ya usimamizi kuhusu sifa za wasimamizi wa ngazi ya juu wa kampuni za bima" ya mwaka 2003 na "Usimamizi kuhusu ofisi za wawakilishi wa kampuni za bima za kigeni nchini China" ya mwaka 2004, zitabatilishwa kwa wakati mmoja.

Idhaa ya kiswahili 2006-08-01