Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-01 18:25:44    
Radio China Kimataifa kukutana na wasikilizaji wake wa Russia huko Ulan-Ute

cri

Tarehe 31 Julai Mkutano kati ya Radio China kimataifa na wasikilizaji wake wa Russia ulifanyika huko Ulan-Ute, mji mkuu wa Jamhuri ya Buriat ya Russia, mkutano huo uliandaliwa na ujumbe wa waandishi wa habari wa "Safari ya Urafiki wa China na Russia".

Saa 9 alasiri tarehe 31 Julai ya saa za Ulan-Ute, wasikilizaji zaidi ya 10 wa Radio China kimataifa kutoka sekta mbalimbali za Russia walikusanyika kwenye chumba cha mkutano katika Hoteli ya Buriat, wasikilizaji hao wote ni wasikilizaji watiifu sana wa matangazo ya kirussia ya Radio China kimataifa, hata wameanzisha kwa hiari klabu yao ya wasikilizaji. Msururu wa magari ya waandishi wa habari wa "Safari ya urafiki wa China na Russia" ulipopita kwenye sehemu hiyo, mkutano kati ya Radio China kimataifa na wasikilizaji wake wa Russia ulifanyika kwa wakati.

Ili kueleza makaribisho yao kwa ujumbe huo wa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari vya China ikiwemo Radio China kimataifa, mkurugenzi wa Klabu ya wasikilizaji wa Radio China kimataifa mjini Ulan-Ute Bwana Arshalanov Budazhap alisoma mashairi yake matatu aliyotunga, kabla ya kuimba wimbo alisema:

Marafiki wapenzi, nafurahi sana kukutana nanyi hapa nyumbani kwetu. Kwenye mkutano huu napenda kuimba wimbo kwa ajili ya mashujaa waliowahi kufanya mapigano huko Manzhouli, na kwa ajili ya China, nchi jirani yetu. Tuimbe wimbo kwa pamoja ili kuimarisha na kuendeleza uhusiano kati ya China na Russia.

Aliwaongoza wasikilizaji hao wa Russia kuimba wimbo maarufu wa Russia "Katyusha" na nyimbo nyingine za urafiki wa China na Russia walizotunga wenyewe, ndani ya chumba cha mkutano, makofi ya furaha yalipigwa mara kwa mara.

Waandishi wa habari wanaoshiriki kwenye "Safari ya Urafiki wa China na Russia" inayoandaliwa na Radio China kimataifa walifika Ulan-Ute. Jamhuri ya Buriat, uliko mji wa Ulan-Ute ni moja kati ya Jamhuri 21 za Shirikisho la Russia, upande wake wa kusini unapakana na Mongolia, eneo lake ni zaidi ya kilomita laki 3.5, na idadi ya watu wake ni milioni 1.05. Na huko Ulan-Ute kuna wachina zaidi ya 4500 wanaoishi huko, mkurugenzi wa "Shirikisho la urafiki wa China na Russia" la Ulan-Ute Mzee Wang Sijie pia alihudhuria mkutano huo na kuukaribisha ujumbe wa waandishi wa habari wa "Safari ya Urafiki wa China na Russia". Alisema:

Safari ya ujumbe huo ina umuhimu mkubwa katika kuzidisha maelewano na urafiki kati ya wananchi wa China na Russia, hali kadhalika kwa sisi wachina tunaoishi nchini Russia, kwani itasaidia kuboresha mazingira ya kuishi na kuanzisha shughuli kwa wachina wanaoishi hapo, hivyo tunawashukuru na kuukaribisha ujumbe huo wa waandishi wa habari kuja Ulan-Ute kufanya ziara.

Mkurugenzi wa Idara kuu ya habari ya Radio China kimataifa Bwana Yin Li aliwaelezea wasikilizaji CRI hali halisi ya ujumbe wa waandishi wa habari wa "Safari ya Urafiki wa China na Russia", tena kuonesha video yenye picha safi. Alipozungumzia urafiki kati ya China na Russia alisema:

China na Russia nchi mbili kubwa tena ni majirani wema, kufanya ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili ni msingi wa kujipatia ustawi wa pamoja wa nchi hizo mbili, ndiyo maana sisi waandishi wa habari tunataka kuandika, kupiga picha na Kurekodi hali halisi kuhusu maendeleo ya Russia.

Kwenye mkutano huo waandishi wa habari wa ujumbe huo kutoka shirika la habari la China Xinhua, gazeti la Renminribao na vyombo vingine vya habari vya China pia walizungumza na wasikilizaji wa Radio China kimataifa katika hali iliyojaa urafiki na uchangamfu. Mwisho watu wote walioshiriki kwenye mkutano huo waliimba wimbo maarufu wa Russia uitwao Jioni ya kitongoji cha Moscow", mkutano huo ulifikika kilele cha furaha.