Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-02 19:12:11    
Maoni tofuati yaoneokana kwenye uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

cri

Uchaguzi wa rais na baraza la chini la bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ulifanyika tarehe 30 mwezi Julai na matokeo ya uchaguzi yatatolewa baada ya wiki kadhaa. Tarehe mosi mwezi Agosti, mmoja wa wagombea urais Bw. Azarias Ruberwa alieleza kuwa atakataa matokeo ya uchaguzi huo, ambapo maoni tofauti yameonekana kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia wa nchi hiyo uliokuwa unasubiriwa na watu kwa miaka zaidi ya 40 iliyopita.

Bw. Azarias Ruberwa ni makamu wa rais wa serikali ya mpito ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kiongozi wa chama cha RCD. Alipohojiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini Kinshasa alieleza kuwa kutokana na ripoti iliyotolewa na waungaji mkono wake, hali mbaya ya ukiukaji wa taratibu za uchaguzi ilitokea katika baadhi ya vituo vya kupigia kura ambayo itaathiri sana matokeo ya uchaguzi huo. Kwa hiyo ametaka uchaguzi ufanyike tena katika sehemu zilizokuwa na matatizo hayo, la sivyo atatumia njia zote halali kukataa matokeo ya uchaguzi huo.

Uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia kufanyika nchini humo tangu miaka 46 iliyopita tangu nchi hiyo ipate uhuru. Wagombea 33 akiwemo rais Joseph Kabila wa serikali ya mpito ya nchi hiyo wanagombea wadhifa wa urais, na wagombea 9700 wanagombea viti 500 vya bunge la taifa . Ingawa tukio kuhusu vyama vya upinzani kususia uchaguzi huo lilitokea kabla ya kupiga kura, lakini watu zaidi ya milioni 25 walioteseka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe walipiga kura zao katika vituo elfu 5 vya kupigia kura na kutumai kuwa uchaguzi huo utaifanya nchi hiyo yenye mandhari nzuri na maliasili nyingi lakini migogoro ilitokea mara kwa mara iweze kufuata njia ya amani na maendeleo.

Jumuiya ya kimataifa imesifu sana uchaguzi huo uliofanyika kwa mafanikio nchini humo. Vikundi vinane vya ujumbe wa wachunguzi wa kimataifa ukiwemo Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya vilivyokwenda nchini humo kusimamia uchaguzi huo, tarehe mosi vilitoa taarifa ya pamoja kupongeza kufanyika kwa mafanikio kwa uchaguzi huo na kuwahimiza wagombea waheshimu uchaguzi wa wananchi wa nchi hiyo, kutumia ipasavyo njia zote halali kutatua maoni tofauti juu ya matokeo ya uchaguzi huo, kutekeleza ahadi walizotoa kwa mchakato wa amani ya nchi hiyo na kuendelea kusonga mbele kuelekea kwenye njia ya masikilizano ya taifa na ukarabati wa nchi. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan pia alitoa taarifa akisema, uchaguzi wa nchi hiyo ni ukurasa mpya katika mchakato wa amani ya nchi hiyo, na anazitaka pande mbalimbali zipokee matokeo ya uchaguzi zikiwa na moyo wa amani na maafikiano. Kituo cha Carter cha Marekani kilichosimamia uchaguzi huo pia kimeridhishwa na kufanyika kwa uchaguzi huo, kilisema, ingawa yalikuwa na matatizo fulani yaliyohusika na taratibu katika mchakato wa upigaji kura, lakini matatizo hayo yalikuwa ni madosari madogo kwa kufanyika kwa uchaguzi huo.

Hivi sasa tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo haijatoa jibu kutokana na maoni aliyoeleza Bw. Azarias Ruberwa. Vyombo vya habari vinaona kuwa ingawa kabla ya hapo baadhi ya vyama vya upinzani vililalamikia kuwepo kwa hali ya kutofuata taratibu katika uchaguzi huo, lakini malalamiko hayo hayakutolewa hadharani, na Bw Ruberwa ni mgombea wa kwanza wa kulalamikia uchaguzi huo hadharani. Zaidi ya hayo, ingawa tume hiyo ilisisitiza kuwa mto yeyote na chama chochote hakiruhusiwi kutangaza matokeo ya uchaguzi huo kabla ya serikali kutangaza matokeo rasmi, lakini makamu wa rais Jean Pierre Bemba ambaye ni mshindani mkuu kwa Joseph Kabila, tarehe 31 alitangaza kuwa anaongoza katika uchaguzi huo, hii hakika imeongeza hali isiyo mwafaka kwa uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo.

Wachambuzi walidhihirisha kuwa kufanyika bila vikwazo kwa uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni hatua ya kwanza iliyopigwa na nchi hiyo kuelekea kwenye mchakato wa amani, na jambo muhimu zaidi ni kuwa pande mbalimbali zipokee matokeo ya uchaguzi huo kwa moyo wa amani na masikilizano na kuendelea kusonga mbele kwenye njia ya maafikiano ya taifa na ukarabati wa nchi. Watu wanafuatilia matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.