Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-02 20:17:56    
Mapishi ya maharagwe marefu yaliyo matamu na nyama ya nguruwe iliyokaushwa

cri

Mahitaji:

Maharagwe marefu yaliyo matamu gramu 200, nyama ya nguruwe iliyokaushwa gramu 200, tangawizi gramu 5, chumvi gramu 5, M.S.G gramu 3, mvinyo wa kupikia gramu 5.

Njia:

1. kata maharagwe marefu yaliyo matamu na nyama ya nguruwe iliyokaushwa vyote viwe vipande vipande. Kata tangawizi iwe vipande vidogovidogo.

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi 60 tia vipande vya tangawizi na nyama ya nguruwe, korogakoroga kwa haraka, halafu tia vipande vya maharagwe marefu yaliyo matamu, korogakoroga, mimina mvinyo wa kupikia, korogakoroga, tia chumvi na M.S.G, korogakoroga, kasha pakue. Mpaka hapo kitoweo hicho kiko tayari kuliwa.