Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-03 19:22:00    
Hali ya siku za baadaye ya Iran inayotatizwa na suala la nyukilia

cri

Tarehe 3 mwezi Agosti ni siku ya kutimiza mwaka mmoja tangu Bw Mohamed Ahamednejad aapishwe kuwa rais wa Iran. Ni siku chache tu zilizopita baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio No. 1696 kuhusu suala la nyukilia la Iran, likiitaka Iran isimamishe shughuli zote za utafiti kuhusu usafishaji wa uranium kabla ya tarehe 31 mwezi Agosti. Kwa kuwa siku hizo mbili zinakaribiana sana, hivyo baadhi ya watu wanamhusisha Bw. Ahmednejad na suala la nyukilia la Iran lenye matatizo.

Baada ya baraza la usalama kupitisha azimio, jumuiya ya kimataifa inaona azimio hilo ni mwafaka. Kwanza azimio hilo linaonesha kazi muhimu ya Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, ambalo mtu yeyote mwingine hawezi kuchukua nafasi yake katika shughuli za kutatua suala la nyukilia la Iran, na limesisitiza umuhimu wa utatuzi suala la nyuklia la Iran kwa njia ya mazungumzo ya kisiasa na kidiplomasia.

Pili, ingawa azimio hilo linaitaka Iran itekeleze maazimio ya Umoja wa Mataifa kabla ya tarehe 31 mwezi Agosti, lakini kwa kufikiria kuwa Iran imekuwa ikitaka kutoa jibu rasmi kuhusu mpango wa nchi 6 wa utatuzi wa suala la nyukilia la Iran kabla ya tarehe 22 mwezi Agosti, azimio hilo limeipa Iran muda wa kutafakari na kuchukua hatua. Tatu, kuchukulia Iran kusimamisha kwa muda shughuli za kusafisha uranium kuwa sharti la kimsingi, ambalo linaendana na matakwa ya jumuiya ya kimataifa ya kutoeneza silaha za nyukilia. Nne, kabla ya kuchukua hatua zinazofuata, baraza la usalama linatakiwa kufanya uamuzi mpya. Hatua hiyo inamaanisha kuwa, azimio No. 1696 haliwezi kuweka vikwazo dhidi ya Iran, hata kama haitasimamisha shughuli za kusafisha uranium kabla ya tarehe 31 mwezi Agosti.

Kwa vyovyote vile azimio hilo limeifanya Iran ikabiliwe na hali ya kufanya uchaguzi wa mwisho: yaani kupunguza masharti yake na kukubali kufanya mazungumzo katika hali ya kusimamisha kusafisha uranium, au kuendelea kufanya shughuli husika za nyukilia bila kujali kuwekewa vikwazo na jumuiya ya kimataifa. Endapo Iran itafanya uamuzi wa kwanza, basi suala la nyukilia la Iran litawekwa kwenye njia ya utatuzi wa mazungumzo. Lakini kutokana na mabadiliko ya suala la nyukilia la Iran katika mwaka uliopita, si ajabu kuona Iran ikachuka uamuzi wa pili.

Katika muda wa mwaka zaidi ya mmoja uliopita tangu Bw. Ahmedinejad awe rais, Iran imekuwa ikitekeleza sera zilizofikia kikomo cha mwisho kwa hatua madhubuti, toka kuchambua malighafi ya madini ya uranium hadi kuzindua shughuli za kusafisha uranium. Ingawa kila mara nchi hiyo inapingwa vikali na kupatwa na mashinikizo makubwa kutoka nchi za magharibi, lakini hatimaye imefaulu kuhimili shinikizo hilo na kuifanya jumuiya ya kimataifa ikubali kwa shingo upande ukweli uliopo. Hapo awali Iran ilikuwa na silaha mbili nzuri ya kuikabili Marekani ambazo ni suala la Iraq na bei ya mafuta, kuibuka kwa mgogoro kati ya Lebanon na Israel kumezidisha athari mbaya kwa hali ya mashariki ya kati, hatua ambayo imeongeza nguvu ya Iran kuhusu suala la nyukilia la nchi hiyo.

Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Ulaya vinasema, hata kama Iran itafanya uamuzi wa aina ya pili, haitakataa kabisa katika jibu lake kuhusu mpango wa nchi 6 kabla ya tarehe 22 mwezi Agosti, lengo lake huenda ni kuendelea kuchuana na jumuiya ya kimataifa katika hali ya kutosimamisha shughuli za kusafisha uranium. Lakini hali hiyo huenda itakataliwa na nchi za magharibi. Lakini nchi hizo zitafanya nini baada ya Iran kukataa? Katika miaka ya karibuni, Iran ikitumia raslimali yake kubwa ya mafuta na gesi ya asili, iliingiza karibu nchi zote kubwa katika soko la ushirikiano la mafuta na gesi la Iran, na kuwa umoja wa faida uliofungamanishwa pamoja. Endapo Marekani itashikilia kuiwekea Iran vikwazo vya kiuchumi, ni hakika kuwa maslahi ya nchi hizo kubwa yataathirika vibaya, na endapo vikwazo vikali vitawekwa dhidi ya Iran, basi huenda Iran itajitoa kutoka kwenye "mkataba ya kutoeneza silaha za nyukilia", hatua ambayo jumuiya ya kimataifa haitaki kuona. Watu wanatarajia kuona suala la nyukilia la Iran linatatuliwa kwa njia ya mazungumzo ya kisiasa na kidiplomasia.