Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-08 10:18:28    
Ongezeko la thamani ya uzalishaji mali lazima liambatane na udhibiti wa matumizi ya ovyo ya raslimali

cri

Hivi karibuni kuongezeka kwa matumizi ya nishati katika uzalishaji mali katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu, kumekuwa moja ya masuala yanayofuatiliwa sana na watu wa sekta mbalimbali nchini China. Suala hilo liakiangaliwa kwa mtazamo wa maendeleo na sayansi, ina maana kunatakiwa kuwepo na wazo la kudhibiti matumizi ya ovyo ya rasilimali, mbali na taifa kuwa na ongezeko la pato.

Ongezeko la uchumi linaloambatana na matumizi ya ovyo ya rasilimali katika miaka mingi iliyopita, limefanya maendeleo ya uchumi wa China kukabiliwa na shinikizo kubwa la mahitaji ya raslimali. Kama China ikitaka kudumisha maendeleo ya uchumi na jamii ya China, inapaswa kudhibiti matumizi ya ovyo ya raslimali, na hili limekuwa ni jukumu la haraka linaloikabili China kwa sasa.

Tunapaswa kuona kuwa wingi wa nishati iliyotumika katika uzalishaji mali nchini China ni nishati inayotumika mara moja tu. Jukumu lililopo sasa hivi la kujenga viwanda na miji nchini China bado halijatimizwa, mfano wa matumizi ya rasilimali nchini China bado yako katika kipindi cha kupanda mlima, ambapo shinikizo la rasilimali litakuwa kubwa kadiri siku zinavyokwenda. Endapo China haitabadilisha haraka mtizamo wa zamani na mtindo wa ongezeko, basi maendeleo ya uchumi na jamii ya China yatakwama. Mpango wa 11 wa maendeleo ya miaka 5 unaagiza kujenga jamii inayodhibiti matumizi ya ovyo ya raslimali, na kupunguza 20% ya matumizi ya nishati kwenye uzalishaji mali. Hali ya maendeleo ya uchumi katika nusu ya kwanza ya mwaka huu inaonesha kuwa si rahisi kutimiza lengo hilo. Endapo ongezeko la uchumi halitahusishwa na udhibiti wa matumizi ya ovyo ya rasilimali na kuhimiza pande mbalimbali husika kutupilia mbali desturi ya zamani ya kuleta maendeleo kwa kutumia ovyo rasilimali na kujikuza katika kiwango cha chini bila kujali gharama, basi lengo la udhibiti wa matumizi ya ovyo ya rasilimali la mpango wa 11 wa maendeleo ya miaka 5 halitaweza kutimizwa.

Udhibiti wa matumizi ya ovyo ya raslimali na kuwa na ongezeko la uchumi siyo mambo mawili yanayopigana, bali ni pande mbili za sarafu moja, udhibiti wa matumizi ya ovyo ya raslimali pia ni nguvu ya uzalishaji mali. China inapaswa kuwa na mtazamo wa maendeleo ya kisayansi na kuwa na wazo la lazima kudhibiti matumizi ya ovyo ya raslimali katika shughuli za kuleta ongezeko la uchumi, kudhibiti miradi inayotumia nishati kwa wingi, kuchukua hatua mbalimbali za kisera za kushawishi serikali, viwanda na watu wote kudhibiti ipasavyo matumizi ya ovyo ya rasilimali, kuunga mkono viwanda na kampuni kudhibiti matumizi ya ovyo ya nishati, maji na vifaa, na kufanya mageuzi ya teknolojia na kutumia raslimali kwa njia mbalimbali. Idara husika na serikali za mitaa zinatakiwa kuimarisha usimamizi na ukaguzi kuhusu udhibiti wa matumizi ya ovyo ya rasilimali, kufanya utafiti kuhusu utaratibu, mfumo, ukusanyaji wa kodi na bei za vitu ili kuhimiza jamii nzima ya China kudhibiti na kupiga vita matumizi ya ovyo ya raslimali.

Idhaa ya kiswahili 2006-08-08