Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-09 16:53:13    
Mapishi ya yai la kukaanga lililokorogwa pamoja na tango chungu na kamba-mwakaje

cri

mahitaji:

matango machungu mawili, mayai mawili, kamba-mwakaje gramu 100, kiasi kidogo cha chumvi, mafuta

njia:

1. ondoa vitu vilivyoko ndani ya matango machungu, uyakate yawe vipande vipande, chemsha maji na tia chumvi kidogo, baada ya kuchemka, weka vipande vya matango machungu kwenye maji korogakoroga, halafu uvipakue na uweke kwenye maji baridi, uvipakue na uvikaushe.

2. koroga mayai pamoja na chumvi, osha kamba-mwakaje na uwakaushe.

3. tia mafuta kwenye sufuria washa moto mpaka yawe joto la nyuzi 60, tia kamba-mwakaje korogakoroga halafu tia vipande vya matango machungu kisha korogakoroga, uvikusanye na mimina mayai yaliyokorogwa polepole, yakaange pamoja na vipande vya matango na kamba-mwakaje mpaka yawe na rangi ya hudhurungi, endelea kukaanga upande mwingine mpaka yawe rangi ya hudhurungi. Kisha pakua. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.