Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-16 19:50:07    
Mapishi ya nyama ya ng'ombe na ufuta

cri

Mahitaji

Nyama ya ng'ombe gramu 200, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, yai moja, mafuta ya pilipili hoho nusu kijiko, wanga vijiko viwili, ufuta kijiko kimoja, mchuzi wa soya kijiko kimoja, sosi ya nyanya, siki vijiko vitatu, sukari vijiko vitatu, chumvi roba tatu kijiko, sosi ya chaza vijiko vitatu, wanga wa pilipili manga kijiko kimoja, kiasi kidogo cha vipande vya vitunguu saumu na pilipili hoho

Njia

1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, koroga pamoja na mchuzi wa soya na wanga wa pilipili manga.

2. koroga yai, washa moto na tia mafuta kwenye sufuria, chovya vipande vya nyama ya ng'ombe kwenye yai na wanga halafu uviweke kwenye sufuria vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi, vipakue.

3. washa moto tena, tia vipande vya vitunguu saumu na pilipili hoho, mafuta ya pilipili hoho, mimina mvinyo wa kupikia, siki, sosi ya chaza, sosi ya nyanya, korogakoroga, tia sukari, na chumvi na endelea korogakoroga, baada ya kuchemka tia vipande vya nyama ya ng'ombe vilivyokaangwa, korogakoroga halafu vipakue. Tia ufuta kwenye kitoweo hicho. Mpaka hapa kitoweo hicho kiko tayari kuliwa.