Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-16 20:03:12    
Kutoa mafunzo na kufuatilia wanawake ni kazi muhimu katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi

cri

Katika dunia nzima, miongoni mwa watu milioni 40 walioambukizwa virusi vya Ukimwi, nusu ni wanawake. Hali ya urahisi ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa wanawake inatokana na sababu mbalimbali, na sababu kuu ni wanawake wanakosa vitendo vya kujilinda. Mkutano wa 16 wa ugonjwa wa Ukimwi duniani unafanyika hivi sasa huko Toronto, Canada. Watu wanaohudhuria mkutano huo wamedhihirisha kuwa, kazi muhimu ya kupata ufanisi katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi ni kutoa elimu na mafunzo kwa wanawake, kuwafuatilia na kuboresha hadhi ya wanawake.

Mwenyekiti wa Kamati ya matibabu ya utekelezaji ya Canada Bwana Louise Binder alisema, ni lazima uwekwe mkakati wa kuwaelimisha wanawake vijana katika mikakati ya kinga na udhibiti wa Ukimwi kote duniani. Alisema:

Hata kama wanawake fulani wanajua kuwa huenda wako katika hatari ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi, lakini kutokana na hali ya ubaguzi wa kijinsia na hali isiyo ya usawa katika hadhi ya kiuchumi na kijamii, wanawake hao huwa katika hali ya dhaifu kuliko wanaume wakati wa kujamiiana, tena hawana haki ya kuamua kuchagua njia ya kujilinda.

"Haki ya kujilinda" aliyosema Bwana Binder ni kwamba baadhi ya wanawake hawawezi kuwataka wapenzi wao watumie kondomu, hivyo wanaambukizwa virusi vya Ukimwi kwa kupitia vitendo vya kujamiiana. Hali hii ni ya kawaida katika mchakato wa kuambukiza Ukimwi kote duniani, hata imesababisha watoto wengi wachanga waambukizwe virusi vya Ukimwi kutokana kwa mama wazazi wao wenye virusi vya Ukimwi.

Mfuko wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton siku zote unafanya juhudi za kutoa dawa za kupambana na Ukimwi na misaada husika kwa nchi zilizoko nyuma katika maendeleo ya uchumi. Bwana Clinton anaona kuwa, kazi muhimu ya kukinga Ukimwi ni kuwawezesha wanawake wapewe haki. Bwana Clinton akisema:

Hili ni suala kuhusu haki. Hasa katika nchi nyingi za Afrika, kama wanawake wakipewa haki kubwa zaidi, miradi ya kutoa elimu kuhusu kinga ya Ukimwi itapata ufanisi mkubwa zaidi, ili kupunguza idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya Ukimwi katika nchi mbalimbali.

Hivi sasa wagonjwa wanawake wa Ukimwi wamechukua nusu ya wagonjwa wote wa Ukimwi na wenye virusi vya Ukimwi kote duniani. Na hatari ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa vijana wa kike na watoto wa kike ni mara 2.5 kuliko vijana wa kiume wenye rika moja kote duniani. Na robo tatu ya wanawake walioambukizwa virusi vya Ukimwi ni vijana wa kike wenye umri kati ya 15 hadi 24.

Bibi Sherry ni mgonjwa wa Ukimwi mjini Philadelphia, Marekani. Kwa kuwa hapo awali yeye hakuweza kuchukua hatua za kujilinda, hivyo aliambukizwa virusi vya Ukimwi, na baadaye akawa sehemu moja ya watu wanaoambukiza virusi vya Ukimwi. Alisema:

Baada ya kuambiwa kuwa nimeambukizwa virusi vya Ukimwi, hata mimi sikutaka kutambua ukweli wa mambo, ambapo nilikuwa bado ninajamiiana na wengine, kwa uchache nilificha hali halisi ya ugonjwa wangu kwa nusu ya watu waliojamiiana nami.

Ili kuimarisha haki ya kujiamulia waliyo nayo wanawake wakati wa kujikinga dhidi ya virusi vya Ukimwi, na kudhibiti kwa ufanisi maambukizi ya virusi vya Ukimwi, idara za sayansi za nchi mbalimbali siku zote zinatafiti dawa za kuua viumbe vidogo, lakini mpaka sasa bado hazijapata maendeleo makubwa.

Meneja mkuu wa Kampuni ya software ya Marekani Bwana Bill Gates ambaye siku zote anafanya juhudi kuchangia kinga na tiba ya Ukimwi alieleza matumaini yake kwenye mkutano huo kuwa, wanasayansi wataharakisha utafiti kwenye sekta hiyo, na yeye atatoa michango mingi zaidi kwa utafiti na uvumbuzi wa sekta hiyo. Alisema:

Tunatoa mwito wa kuwataka wanasayansi waharakishe utafiti wao kuhusu dawa zitakazotumiwa na wanawake kuua viumbe vidogo au kupata vidonge vya dawa hiyo, ili kuzuia virusi vya Ukimwi visiambukizwe kwa wanawake. Ni matumaini yetu kuwa dawa hizo zitaleta maendeleo makubwa katika kinga na tiba ya Ukimwi. Hasa kwa wanawake ili kuokoa maisha yao, si lazima kutegemea ruhusa za wanaume za kutumia kondomu.

Hakika kupambana na Ukimwi kunatubidi tuchukue njia mbalimbali, kwani suala hilo linahusiana na masuala mengi ya kuhimiza utafiti wa kisayansi, kuwahimiza watu kwenye jamii nzima waongeze ufahamu juu ya Ukimwi na kuondoa hali ya kuwanyanyapaa wagonjwa wa Ukimwi, huu ni mchakato wenye utatanishi na taabu kubwa.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Ukimwi barani Afrika Bwana Stephen Lewis anaona kuwa, kama mpango wa kuwasaidia wanawake utatekelezwa kihalisi, ndipo binadamu watakapoweza kushinda balaa inayoletwa na Ukimwi. Alisema jambo muhimu zaidi ni kuanzisha shirika moja la wanawake linalowakilisha wanawake wa nchi zote duniani zikiwemo nchi za Afrika na nchi zilizoendelea, na shirika hilo lingeendeshwa kwa njia ya Umoja wa Mataifa. Kama wanawake hawataweza kuhamasishwa na kuchukua hatua, basi kamwe hatutaweza kushinda balaa hilo la Ukimwi.