Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-18 18:23:39    
Watu wa hali mbalimbali wa Japan wana matarajio na pia wana wasiwasi kuhusu serikali ya awamu ijayo kuboresha uhusiano na China na Korea ya kusini

cri

Baada ya kwenda kwenye Hekalu la Yasukuni kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita tarehe 15, waziri mkuu wa Japan Koizumi Junichiro alikaa nyumbani akipumzika bila kutoka nje. Watu wa sekta mbalimbali wa Japan wanapomlaani vikali pia wanatupia macho somo kubwa linaloikabili serikali ya awamu ijayo ya Japan, na wana matarajio huku wakiwa na wasiwasi kuhusu mrithi wa Koizumi wa awamu ijayo jinsi atakavyoboresha uhusiano kati ya Japan na China na Korea ya kusini.

Gazeti la Japan Mainichi News tarehe 16 lilitoa makala ikieleza kuwa, Koizumi alikwenda tena kwenye hekalu la Yasukuni tarehe 15, jambo hilo limeibidi serikali ya awamu ijayo ya Japan ikabiliane na somo kubwa kuhusu suala la Hekalu la Yasukuni, ambapo vizuizi vya kuboresha uhusiano kati ya Japan na China na Korea ya kusini vitakuwa vingi zaidi. Masuala mengi yenye utatanishi kuhusu wajibu wa kivita vya vita vikuu vya pili vya dunia, utenganishaji wa mambo ya kisiasa na kidini katika katiba, na utatuzi wa suala la wahalifu wakuu wa kivita, yote hayo hayataweza kuepushwa na serikali ya awamu mpya ya Japan.

Katika sekta ya uchumi sauti za kudai kurekebisha upya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Japan na Korea ya kusini imezidi kuwa kubwa siku hadi siku. Viongozi wengi wa makundi makubwa ya kiuchumi wanatoa matamshi ya kumtaka waziri mkuu wa awamu ijayo aboreshe kwa ufanisi uhusiano kati ya Japan na China. Naibu mkurugenzi wa Shirikisho la makundi ya kiuchumi la Japan Keidanren alieleza matumaini yake kuwa, waziri mkuu wa awamu ijayo ataweza kufanya juhudi ili kuufanya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Japan na China uwe wa kawaida mapema iwezekanavyo. Msaidizi wa mkurugenzi wa Shirikisho la Keidanren la Japan tarehe 13 alipohojiwa na waandishi wa habari alieleza matumaini yake kuwa, waziri mkuu wa Japan wa awamu ijayo ataweza kujenga uhusiano wa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na viongozi wakuu wa nchi zote. Mwakilishi wa kampuni moja maarufu ya Japan nchini China alisema, bila shaka kitendo cha waziri mkuu wa Japan kwenda kwenye Hekalu la Yasukuni kinaweza kuharibu sura za bidhaa za Japan, hivyo wanatarajia serikali ya awamu ijayo ya Japan irekebishe uhusiano kati ya Japan na China.

Lakini hivi sasa mgombea wa wadhifa wa waziri mkuu mwenye nguvu kubwa zaidi Bwana Shinzo Abe bado hajaeleza wazi msimamo wake kuhusu suala la Hekalu la Yasukuni, hii inawafanya watu wa sekta za uchumi wa Japan wawe na wasiwasi mkubwa, na wanahofia kuwa huenda bwana huyo atafuata nyayo za Koizumi na kuzusha matata katika uhusiano wa kidiplomasia kati ya Japan na China.

Hata vyombo vya habari vya Japan vina wasiwasi kama huo. Gazeti la Asahi News la Japan tarehe 16 lilichapisha makala moja kwenye ukurasa wake wa kwanza ikidhihirisha kuwa, Bwana Shinzo Abe anatumia mbinu isiyoeleweka kuhusu suala la Hekalu la Yasukuni, kama anataka kutumia mbinu yake hiyo kuvunja hali ya kukwama ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Japan na nchi za Asia. Lakini Shinzo Abe siku zote hatambui wazi kama wahalifu wa kivita wa ngazi ya A ni "wahalifu wa kivita". Makala hiyo ilisisitiza kuwa kama akiwa kiongozi wa nchi anapaswa kueleza wazi mtizamo wake kuhusu historia na vita. Tofauti na Bw Koizumi kusisitiza mara kwa mara "daima kutoanzisha tena vita", Shinzo Abe anafuatilia sana sera ya ulinzi wa taifa, na pia anafanya juhudi kubwa kuhusu kuendesha mamlaka ya kujilinda ya kundi na mamlaka ya kufanya mapambano fulani fulani. Lakini kadiri siku inavyokaribia kushida katika ugombeaji wa wadhifa wa waziri mkuu, ndivyo Shinzo Abe anavyotakiwa zaidi afanye chaguo kuhusu kutekeleza kwanza kanuni za kisiasa za kuwa "mwanasiasa wa aina ya kimapigano" au kuchukua msimamo wa kufuata hali halisi ya kuwa mwanasiasa wa "kusikiliza sauti ya wananchi.

Msimamo usioeleweka wa Shinzo Abe kuhusu suala la hekalu la Yasukuni, unakosolewa hata na wanachama wa chama tawala cha Japan. Katibu mkuu wa baraza la juu la chama tawala cha Japan Bw Toranosuke Katayama alidhihirisha kuwa, wagombea wa wadhifa wa waziri mkuu wanapaswa kueleza wazi maoni yao kuhusu Hekalu la Yasukuni.