Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-23 16:06:31    
Mapishi ya boga na mayai yaliyotiwa chumvi

cri

Mahitaji

Boga moja, mayai yaliyotiwa chumvi, mafuta vijiko viwili, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, chumvi nusu ya kijiko, unga wa kuku nusu ya kijiko, kiasi kidogo cha vitunguu maji.

Njia

1. weka kiini cha mayai yaliyotiwa chumvi na mvinyo wa kupikia kwenye bakuli moja, mimina maji kwenye sufuria na kuyachemsha, weka bakuli hilo kwenye sufuria na uchemshe kwa mvuke kwa dakika 8, pakua halafu pondaponda kiini uwe laini.

2. ondoa ganda la boga, halafu likate liwe vipande vidogo.

3. tia mafuta kwenye sufuria,wpasha moto tia vipande vya vitunguu maji korogakoroga halafu tia vipande vya boga korogakoroga mpaka viwe laini, tia kiini cha mayai, tia chumvi na unga wa kuku, korogakoroga pakua. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.