Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-23 17:02:42    
China yajitahidi kuboresha kiwango cha matibabu kwenye sehemu zilizo nyuma kiuchumi

cri

China ni nchi inayoendelea na yenye eneo kubwa la ardhi, na sehemu mbalimbali zinatofautiana kimaendeleo. Kwenye miji kadha ya mashariki ya China, watu wanaishi maisha mazuri, na kwenye sehemu kadhaa za magharibi na za kati, japokuwa wakazi wa huko wanaweza kumudu maisha ya kimsingi lakini kiwango cha mazingira kwenye sehemu hizo bado kina tofauti kubwa ikilinganishwa na sehemu za mashariki.

Kwenye sehemu zilizonyuma kiuchumi nchini China, kupata magonjwa ni moja ya jambo ambalo linawatia wasiwasi wakazi wa huko, kwani watu wengi wanashindwa kumudu malipo ya matibabu wakiwa wagonjwa, hata kama wakiwa na hali nzuri ya kiuchumi, haawwezi kupata matibabu kwa ufanisi kutokana na vifaa duni vya matibabu na kiwango cha chini cha udaktari cha huko.

Pamoja na maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China, serikali ya China imezingatia zaidi umuhimu wa kuimarisha uwekezaji wa sekta ya matibabu, na inafanya juhudi kuboresha kiwango cha matibabu kwenye sehemu zilizo nyuma kiuchumi. Hivi karibuni, mwandishi wetu wa habari alitembelea wilaya ya Pan mkoani Guozhou iliyoko kusini magharibi mwa China.

Wilaya ya Pan ni moja kati ya wilaya 600 zilizothibitishwa na serikali ya China kupewa misaada ya kiuchumi ili ziondokane na umaskini, yaani wilaya hiyo ni moja ya sehemu zilizo nyuma kabisa kiuchumi. Pato la jumla la sehemu hiyo kwa kila mtu ni dola za kimarekani 500, likiwa ni nusu ya kiwango cha wastani cha China. Kutokana na umaskini, wakazi wengi wa huko wanashindwa kumudu malipo ya matibabu. Ili kutatua suala hilo, wilaya hiyo imetekeleza utaratibu mpya wa ushirikiano wa matibabu vijijini kuanzia mwaka 2005. mkuu wa wilaya hiyo Bw. Luo Zixiang alieleza:

"wilaya ya Pan ni wilaya ya majaribio ya utekelezaji wa utaratibu mpya wa ushirikiano wa matibabu vijijini. Sera hiyo inalenga kuwasaidia wakazi wa huko wasirejee maskini kutokana na kupatwa magonjwa. Kwa jumla, wakazi wanaiunga mkono sera hiyo na kuona hii ni sera yenye manufaa sana."

Utaratibu mpya wa ushirikiano wa matibabu vijijini unawekwa na serikali kwa ajili ya kuboresha kiwango cha matibabu kwenye sehemu za vijijini, yaani kila mwaka serikali kuu inatoa ruzuku ya yuan 20 kwa kila mkulima anayeshiriki kwenye utaratibu huo, serikali ya mitaa kutoa ruzuku ya yuan 20 kwa kila mkulima, kila mkulima kutoa yuan 10 peke yake na fedha hizo zinawekwa kwenye mfuko wa ushirikiano wa matibabu. Wakulima hao wakipatwa magonjwa, wataweza kulipiwa kwa kiasa fulani. Mpaka sasa, asilimia 78.5 ya wakulima wameshiriki kwenye utaratibu huo.

Mwandishi wetu wa habari alizungumza na wakulima kadhaa waliokuwa wanapewa matibabu kwenye kituo cha huduma za afya cha wilaya hiyo. Mzee moja wa kabila la waYi Bw. Li Kaijiang alipatwa ugonjwa wa gastric ulcer, hivi sasa matibabu yake yamegharamia zaidi ya yuan 2200, na mfuko wa ushirikiano wa matibabu ulimlipia yuan zaidi ya 1000. Mzee huyo alisema, jamaa zao wote wameshiriki kwenye utaratibu huo. Anaona kuwa utaratibu huo ni mzuri na unawapunguzia kwa kiasi kikubwa mizigo ya matibabu.

Daktari kijana wa kituo hicho cha huduma za afya Bw. Zhang Ge alieleza, kutokana na sera hiyo mpya, wakulima wamepunguziwa kwa kiasi malipo ya matibabu. Tangu sera hiyo ianze kutekelezwa, wakulima wengi zaidi wanakwenda kuonana na daktari kila siku.

Ingawa suala la matibabu ya wakazi wa wilaya hiyo limetatuliwa kiasi, lakini vifaa duni vya matibabu na kiwango cha chini cha udaktari pia vinaathiri huduma za afya za huko. Mwuguzi wa kituo cha huduma za afya cha tarafu ya Machang Bi. Zhang Yaling alisema, sasa wakazi wengi wanakuja kuonana na daktari, basi kiwango cha chini cha udaktari, vifaa duni vya matibabu na upungufu wa nguvu kazi zinaonekana wazi zaidi. Bi. Zhang Yaling alisema,

"tunaweza kutibu magonjwa ya kawaida, kwa mfano mafua. Kwa watu waliopatwa magonjwa makubwa, tunawapendekeza kwenda kutibiwa katika hospitali ya wilaya. Sasa tuna mashine moja ya kuchunguzia magonjwa kwa mawimbi ya ultrasonic ya aina ya B, lakini sote hatujui kuitumia. Tunatumai kuwa tutaweza kupewa mafunzo katika hospitali za wilaya."

Aidha, baadhi ya wakazi walilalamika kuwa, wakipatwa magonjwa makubwa kidogo, ni lazima waende hospitali ya wilaya kupata matibabu, hali hiyo imeongeza gharama ya matibabu kiasi fulani.

Ili kutatua kabisa masuala hayo, serikali ya wilaya ya Pan inafanya juhudi kuchukua hatua mbalimbali. Kwa mujibu wa mkuu kaimu wa wilaya hiyo Bw. Luo Zixiang, kwanza serikali inapaswa kuajiri wafanyakazi wengi zaidi katika vituo vya huduma za afya. Kwa mfano kuwahamasisha wanafunzi wahitimu wa vyuo vikuu kufanya kazi katika vituo hivyo na kuwatuma madaktari wa hospitali za wilaya watoe mafunzo katika vituo hivyo. Pili, inapaswa kuboresha kiwango cha matibabu vijijini kwa kutegemea sera nafuu ya taifa na fedha za madeni ya taifa. Mwaka huu serikali ya wilaya ya Pan imetenga yuan milioni moja kurekebisha vifaa ya matibabu ya vituo vya huduma za afya. Aidha, inatakiwa kuimarisha kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya, hasa watumishi wa afya wa zahanati za vijiji, kujitahidi kuinua kiwango chao cha udaktari, pia inapaswa kuwawekea sera na mazingira mazuri na kuhakikisha pato lao la kimsingi.

Licha ya hayo, mwandishi wetu wa habari pia aligundua zahanati ndogo binafsi katika wilaya hiyo, zahanati hizo kwa kiasi fulani zimefidia upungufu wa idara za matibabu za kiserikali. Wakulima wakipatwa magonjwa madogo wanaweza kujipata matibabu kwa urahisi katika zahanati hizo. Lakini zahanati hizo pia zinakumbwa na matatizo kadhaa na kadhaa, Bw. Wang Qing aliendesha zahanati moja kwa miaka zaidi ya 10. alisema:

"sehemu hiyo iko nyuma sana kiuchumi, wakazi wengi wanashindwa kumudu malipo ya matibabu. Baadhi ya wagonjwa wa nimonia walikuja zahanati yangu walipokuwa wana homa ya digri 39 na 40, lakini walikuwa na pesa chache tu mfukoni. basi tunaweza kuwatibu tu. Hivi sasa watu wengi bado hawajalipa."

Bw. Wang Qing alitaka serikali ya huko iweze kutambua umuhimu wa zahanati binafsi na kuziunga mkono zahanati hizo.