Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-24 18:20:59    
Shirika la chakula na kilimo cha Umoja wa Mataifa lazingatia udhibiti wa matumizi ya maji kwa ajili ya kilimo

cri

Hivi sasa matumizi ya maji kwa ajili ya ya kilimo yanachukua sehemu kubwa zaidi katika matumizi ya maji ya baridi duniani. Katika hali ya kupungukiwa na raslimali ya maji baridi huku mahitaji ya maji yanaongezeka kwa mfululizo, udhibiti wa matumizi ya ovyo ya maji kwa ajili ya kilimo yanafuatiliwa na pande mbalimbali husika. Shirika la chakula na kilimo cha Umoja wa Mataifa, FAO, ambalo makao makuu yao yako mjini Rome, limekuwa likizisaidia nchi wanachama kutatua matatizo mbalimbali yanazikuta katika matumizi ya maji kwa ajili ya kilimo.

"Taarifa kuhusu uendelezaji wa rasilimali ya maji duniani" iliyotolewa mapema mwaka huu na Umoja wa Mataifa ilisema, hivi sasa matumizi ya maji yanayotumika katika kumwagilia mashamba yanachukua karibu 70% ya matumizi ya maji baridi ya binadamu duniani. Ofisa mwandamizi wa idara ya uendelezaji wa rasilimali za ardhi na maji ya FAO Bw. Daniel Renault alisema,

"Majini muhimu sana kwa kilimo, binadamu anakunywa kiasi cha lita 2 za maji kwa siku sana sana lita 4, lakini kuzalisha chakula kinachotosheleza mahitaji ya mtu mmoja, kunahitaji mita za ujazo 4 za maji, hali hiyo inaonesha kuwa matumizi ya maji kwa ajili ya kilimo ni mara 1,000 hivi ya matumizi ya maji ya watu."

Maendeleo ya jamii yamezidisha ushindani wa kupata maji kati ya idara nyingi, wakati ongezeko kubwa la watu linahitaji chakula kingi mwaka hadi mwaka. Taarifa moja ya FAO inaonesha kuwa, katika miaka 30 ijayo, ikiwa uzalishaji chakula utaongezeka kwa 60%, ndipo itakapoweza kutosheleza mahitaji ya chakula ya ongezeko la idadi ya watu. Bw. Daniel Renault alisema ingawa dunia inakabiliwa na changamoto kubwa, lakini tatizo kubwa lililoko hivi sasa ni ufanisi mdogo katika matumizi ya maji kwa ajili ya kilimo. Kuzisaidia nchi wanachama kuinua ufanisi wa matumizi ya maji ya kilimo kutakuwa kazi muhimu za idara ya rasilimali ya maji ya FAO. Licha ya kutoa misaada katika utekelezaji wa sera na uinuaji wa uwezo wa usimamizi raslimali ya maji, FAO inazingatia zaidi kutoa uungaji mkono wa kiteknolojia.

"Tulifanya kazi nyingi kuinua ufanisi wa matumizi ya maji kwa ajili ya kilimo na kutokomeza matumizi ya ovyo ya maji kwa ajili ya kilimo. Misaada tuliyotoa ni ya ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzisaidia serikali za nchi wanachama kuboresha mfumo wa umwagiliaji maji mashambani na kukusanya maji ya mvua, hususan katika nchi za bara la Asia."

Bw. Daniel Renault alieleza mpango wa ushirikiano uliofikiwa kati ya China na FAO mwezi Mei mwaka huu wa kuzisaidia nchi nyingine zinazoendelea kuinua ufanisi wa uzalishaji mazao ya kilimo. Hii ni sehemu moja ya "mpango wa ushirikiano kati ya nchi za kusini na kusini" wa FAO, tunatarajia kuinua ufanisi wa uzalishaji mazao ya kilimo kutokana na usimamishaji wa ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea zilizoko katika vipindi mbalimbali vya maendeleo.

"Moja ya miradi muhimu ya ushirikiano kati ya China na FAO ni mradi wa ushirikiano kati ya nchi za kusini na kusini, hususan ni ushirikiano katika ujenzi wa miradi ya maji. China ni nchi kubwa, na ina uzoefu mkubwa kuhusu mazingira mbalimbali ya uzalishaji mazao ya kilimo. Hivyo kuna wataalamu wenye uzoefu mkubwa wa China kuzisaidia nchi nyingine zinazoendelea, hususan nchi za Afrika, hali hiyo itaisaidia sana kazi za FAO."

Bw. Daniel Renault alisema, kauli-mbiu ya wiki ya maji duniani mwaka huu ni "kukiuka mamlaka ya mito, tunufaike na kubeba majukumu kwa pamoja". Ili kukabiliana na hali ya upungufu wa maji baridi duniani, ziwe sekta zinazotumia maji, au ni nchi na sehemu fulani duniani, licha ya kunufaika kwa raslimali ya maji, pia zinatakiwa kubeba majukumu ya kuhifadhi na kutumia rasilimali ya maji ipasavyo.

Idhaa ya Kiswahili 2006-08-24