Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-29 16:47:24    
China yachukua hatua kudhibiti ongezeko kubwa la uwekezaji

cri

Mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Ma Kai tarehe 25 mwezi huu hapa Beijing alisema, ongezeko kubwa la uwekezaji kwa mali zisizohamishika limekuwa tatizo kubwa katika mambo ya uchumi wa China. Katika nusu ya pili ya mwaka huu, China itadhibiti ipasavyo uidhinishaji wa maombi ya matumizi ya ardhi na kuingia sokoni pamoja na utoaji wa mikopo ili kudhibiti ongezeko kubwa la uwekezaji.

Bw. Mai Kai aliyasema hayo wakati alipotoa taarifa kwa idhini ya baraza la serikali kwenye kikao cha 23 cha mkutano wa kamati ya kudumu ya bunge la taifa la awamu ya kumi. Alisema tokea mwaka huu uanze, ongezeko kubwa la uwekezaji, utoaji mikopo mingi na hali ya kukosa ulingano katika biashara ya nje yalikuwa matatizo makubwa katika shughuli za uchumi wa China. Uwekezaji uliendelea kuwa na ongezeko kubwa, katika miezi 7 ya mwanzo ya mwaka huu, uwekezaji kwenye mali zisizohamishika katika miji ulikuwa na ongezeko la 30.5%, likiwa ni ongezeko la 3.3% kuliko lile la mwaka jana katika kipindi kama hiki. Miradi mipya iliyozinduliwa ilikuwa elfu 115 ikiwa ni ongezeko la elfu 20 kuliko mwaka jana katika kipindi kama hiki. Ujenzi wa miradi iliyokiuka taratibu ulikuwa tatizo kubwa. Utoaji mikopo uliendelea kuongezeka kwa kasi, katika miezi 7 ya mwanzo ya mwaka huu, ongezeko la utoaji mikopo lilifikia Yuan za Renminbi trilioni 2.35 likiwa ni ongezeko la Yuan bilioni 926.8 kuliko mwaka jana katika kipindi kama hiki. Katika kipindi hicho tofauti kati ya matumizi ya fedha na mapato katika biashara ya nje iliongezeka zaidi. Matatizo hayo matatu yalichanganyikana na kuhimizana, lakini hali dhahiri zaidi ni ongezeko kubwa katika uwekezaji kwenye mali zisizohamishika.

Alifafanua kuwa, kuongezeka haraka kwa uwekezaji kwa hivi sasa kunahusiana na kipindi cha historia cha hivi sasa, ambacho China inaharakisha kujenga viwanda na miji, pamoja na kuinuka kwa kiwango na kuongezeka kwa matumizi ya fedha ya watu. Licha ya hayo, marekebisho ya miundo ya kiuchumi, mageuzi ya teknolojia na uimarishaji wa hifadhi ya mazingira pia yanahitaji uwekezaji mwingi, hivyo si ajabu kuona ongezeko kubwa katika uwekezaji. Lakini chanzo muhimu cha ongezeko kubwa la uwekezaji ni kuwa mtindo wa ongezeko la kiwango cha chini bado haujabadilika, baadhi ya mikoa inaendelea kufuatilia kasi ya ongezeko, kuwa na ongezeko la uchumi kwa kutegemea uwekezaji, hususan ni kuwa vikwazo vilivyoko katika mfumo wa utaratibu wa jamii bado havijaondolewa kabisa.

Alisema katika nusu ya pili ya mwaka huu, China itadhibiti kithabiti ongezeko kubwa la uwekezaji kwa hatua za kudhibiti ipasavyo uidhinishaji wa maombi ya matumizi ya ardhi na kuingia sokoni na utoaji mikopo. Kwanza China itatekeleza utaratibu wa kubeba majukumu katika usimamizi wa ardhi na hifadhi ya mashamba, kudhibiti usimamizi wa uidhinishaji wa ombi la matumizi ya ardhi, kuwachukulia hatua maofisa walioidhinisha matumizi ya ardhi kwa kukiuka madaraka, na kuidhinisha matumizi ya ardhi kwa mtindo wa kukodisha na kutumia ardhi kabla ya kutoa maombi. China itachukua hatua halisi kuimarisha hifadhi ya mashamba, na kusisitiza utaratibu wa kutoa fidia kwa ardhi inayotumiwa na kuongeza gharama ya matumizi ya ardhi. Kudhibiti matumizi ya ardhi ya ujenzi wa viwanda na kufuata utaratibu wa namna moja wa kikomo cha chini cha matumizi ya ardhi.

Pili ni kudhibiti ipasavyo ongezeko la utoaji wa mikopo ya fedha, na kuchukua hatua mbalimbali kupunguza nguvu za mzunguko wa fedha wa benki. Kuonesha mfano wa kuigwa na kuelekeza benki za biashara kudhibiti ipasavyo utoaji wa mikopo. Kutia mkazo katika kuboresha muundo wa utoaji mikopo, kudhibiti kithabiti kutoa mikopo kwa viwanda hafifu vinavyotumia nishati bila ufanisi, vinavyotoa uchafuzi mwingi dhidi ya mazingira na vyenye uwezo mkubwa wa uzalishaji wa kuzidi mahitaji. Kuimarisha usimamizi dhidi ya benki na kuendelea kurekebisha utoaji wa mikopo inayoambatana na masharti. Tatu kukamilisha kigezo cha uidhinishaji wa ombi la kuingia sokoni, hususan kuzingatia vigezo vya matumizi ya nishati na hifadhi ya mazingira.

Idhaa ya Kiswahili 2006-08-29