Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-30 19:13:47    
Mapishi ya supu nzito ya samaki ya Songsao

cri

Mahitaji

Samaki gramu 600, paja la ash gramu 10, mzizi wa kichipukizi gramu 25, uyoga gramu 25, viini vitatu vya mayai, vipande vya vitunguu gramu 25, tangawizi gramu 5, wanga wa pilipili manga gramu 2, mvinyo wa kupikia gramu 30, mchuzi wa soya gramu 25, chumvi gramu 3, siki gramu 25, M.S.G gramu 3, maji gramu 250, wanga wa maji gramu 30, mafuta gramu 50.

Njia

1. ondoa vitu vilivyoko ndani ya tumbo la samaki, kata samaki awe vipande na viweke kwenye bakuli moja, koroga pamoja na vipande vya vitunguu maji, tangawizi, mvinyo wa kupikia na chumvi,. Chemsha maji kwenye sufuria, weka bakuli hiyo ndani ya sufuria endelea kuchemsha kwa mvuke kwa dakika 6, ipakue, ondoa vitunguu maji na tangawizi, uvisage vipande vya samaki. Kata paja la ash, mzizi wa vichipukizi na uyoga ziwe slesi, koroga viini vya mayai

2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria tia vipande vya vitunguu maji, korogakoroga, mimina maji, baada ya kuchemka ondoa vitunguu maji, tia mvinyo wa kupikia, slesi za mzizi wa vichipukiki, uyoga, baada ya kuchemka tia nyama ya samaki iliyosagwa, korogakoroga, tia mchuzi wa soya, chumvi, M.S.G mimina maji ya wanga, baada ya kuchemka mimina viini vya mayai vilivyokorogwa, siki na mafuta kidogo. Ipakue. Tia slesi ya paja la ash, vipande vya tangawizi na wanga wa pilipili manga. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.