Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-08-30 19:21:07    
Shughuli za mafunzo ya ufundi wa kazi zaendelea kwa kasi nchini China

cri

Shughuli za mafunzo ya ufundi wa kazi mbalimbali za China zimepata maendeleo makubwa katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa katika vyuo vikuu, wachina wengi zaidi wamepata fursa ya kujiendeleza na kupata elimu ya juu. Lakini kutokana na hali hiyo, jamii ya China imeanza kutilia maanani zaidi elimu ya shahada, na kupuuza mafunzo ya ufundi wa kazi mbalimbali. Hali hiyo imesababisha upungufu wa mafundi kwenye sehemu kadhaa nchini China. Serikali ya China imechukua hatua mbalimbali kusukuma mbele maendeleo ya mafunzo ya ufundi wa kazi.

Kuna ngazi mbili za shule za ufundi wa kazi nchini China, yaani ngazi ya shule ya sekondari na ngazi ya chuo. Msichana Zhang Jiaji mwenye umri wa miaka 18 anasoma katika shule ya usimamizi wa upashanaji habari ya Beijing, ambayo ni shule ya ufundi wa kazi wa kompyuta. Mwanafunzi huyo alisema, anapenda kuchora tangu utotoni mwake, hivyo baada ya kuhitimu kutoka kwenye shule ya sekondari, alichagua mchepuo wa usanifu na uchoraji kwa kompyuta. Alisema:

"nadhani mchepuo huo unahitajika katika jamii. Hivi karibuni, tumepewa mazoezi ya kusanifu picha ya video kwa kauli mbiu ya Olimpiki ya kiungwana. kazi bora kati ya mazoezi hayo itachaguliwa na kuoneshwa kwenye televisheni. Naona kuwa naweza kuifanya vizuri."

Zamani shule kama hiyo hazikupokewa na wazazi wa wanafunzi wa China. Waliona kuwa watoto wao wanaweza tu kuwa watumishi wa serikali au kufanya kazi ofisini baada ya kuhitimu kutoka kwenye vyuo vikuu, na mafunzo ya ufundi wa kazi lilikuwa ni chaguo la kulazimika.

Jiang Jiaji pia aliwahi kuwa na wasiwasi kama huo. Alisema, wakati alipochagua kusoma katika shule ya mafunzo ya ufundi wa kazi, wazazi wake hawakuelewa uamuzi wake na walikuwa na wasiwasi juu ya mustakabali wake. Lakini baada ya mwaka mmoja tu, matokeo mazuri aliyopata katika masomo yake yaliwashangaza wazazi wake. Kinachomfurahisha zaidi ni kuwa wanafunzi wahitimu wa shule hiyo wanapata ajira yenye pato zuri kwa urahisi.

Waziri wa elimu wa China Bw. Zhou Ji alisema, takwimu husika zimeonesha kuwa, hivi sasa kuna shule 16000 za ufundi wa kazi nchini China, kila mwaka mamilioni ya wanafunzi wanahitimu kutoka kwenye shule hizo. Kutokana na hali ya miaka ya karibuni, idadi ya wanafunzi wahitmu wa shule hizo wanaopata ajira ni kubwa zaidi kuliko ya wanafunzi wa vyuo vikuu. Bw. Zhou Ji alisema:

"katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya wanafunzi wahitimu wa shule za mafunzo ya ufundi wa kazi imendelea kuongezeka, hata idadi ya wanafunzi wahitimu wa shule kadhaa haitoshi mahitaji ya jamii. Baadhi ya wakuu wa shule hizo waliniambia kuwa makampuni mengi bado yanasubiri kuwaajiri wanafunzi watakaohitimu mwakani."

Mabadiliko hayo ya hivi karibuni kwa ukweli yanaonesha mabadiliko ya mitizamo wa serikali ya China yaliyotokea katika mchakato wa maendeleo ya uchumi. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na ongezeko la kasi la uchumi wa China, makampuni mengi maarufu duniani yamaanzisha viwanda au idara za utafiti nchini China; makampuni ya China pia yanajitahidi kuongeza kiasi cha teknolojia ya juu kwenye bidhaa zao, na hali hiyo inahitaji mafundi wengi wenye ujuzi wa nadharia na uwezo wa kufanya mazoezi. Hivi sasa, hali ya upungufu mkubwa wa mafundi wa teknolojia za usimamizi wa kitarakimu na wa kutengeneza ya magari. Idadi ya mafundi bingwa inachukua asilimia 3.5 tu miongoni mwa wafanyakazi, ambayo ina pengo kubwa kuliko asilimia 20 hadi 40 katika nchi zilizoendelea.

Kutokana na hali hiyo, serikali ya China imetambua wazi zaidi kuwa, teknolojia ya juu na mfumo wa kisasa wa usimamizi zote zinaweza kuingizwa, lakini idadi kubwa ya wafanyakazi mafundi haiwezi kuingizwa, na inaweza kutatuliwa kwa kuendeleza elimu ya ufundi wa kazi hapa nchini .

Hivyo serikali ya China imechukua hatua mbalimbali kuendeleza elimu ya ufundi wa kazi na itatumia yuan bilioni 10 katika kuimarisha elimu ya ufundi wa kazi, ikiwemo kuboresha miundo mbinu na vifaa vya shuleni na kukamilisha mwundo wa michepuo. China pia imeanzisha ushirikiano wa kimataifa na kujifunza kutokana na uzoefu mzuri wa elimu ya ufundi wa kazi katika nchi za nje. Katika siku za hivi karibuni, wizara ya elimu na wizara ya fedha ya China zimeamua kutoa misaada ya yuan milioni 800 kwa wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi wa shule za ufundi wa kazi kuanzia mwaka huu. Aidha, sehemu mbalimbali pia zitaanzisha misaada ya masomo ya kiserikali na misaada ya michepuo kwenye shule za ufundi wa kazi za sekondari; kuhamasisha na kuongoza idara za fedha zitoe mikopo midogo kwa wanafunzi wa familia yenye matatizo ya kiuchumi. Naibu waziri wa elimu wa China Bi. Wu Qidi alieleza:

"kwa kutumia yuan milioni 800 zilizotengwa na serikali kuu pamoja na misaada iliyotolewa na serikali za mitaa, shule na jamii, asilimia 20 ya wanafunzi wa shule za ufundi wa kazi watapewa misaada ya aina mbalimbali na viwango tofauti katika mwaka huu, hali hiyo itasukuma mbele shughuli za kupanua elimu ya ufundi wa kazi, kuhimiza maendeleo endelevu ya elimu ya ufundi wa kazi nchini China.

Pamoja na uungaji mkono wa serikali kuu ya China, shule za ufundi wa kazi kwenye sehemu mbalimbali nchini China zinajitahidi kuboresha mafunzo ya ufundi wa kazi kutokana na umaalum wa shule hizo. Kwa mfano wa shule ya usimamizi wa upashanaji habari ya Beijing tuliyoitaja, zamani shule hiyo haikuwa na vifaa vingi kwa wanafunzi kufanya mazoezi, hali hiyo ilisababisha wanafunzi wa shule hiyo bado walikuwa na pengo na mafundi yanayohitajika katika makampuni. kwa hivyo shule hiyo imetumia nguvu kazi na fedha nyingi ili kuwapatia wanafunzi fursa za kufanya mazoezi. Mkuu wa shule hiyo Bw. Han Lifan alisema:

"kwa shule za mafunzo ya kazi za sekondari, ni lazima zifuate faida na kuepuka kasoro. Hivyo tunafundisha nadharia kidogo tu, na uzoefu mwingi wa kazi, na kuwapatia fursa nyingi zaidi za kufanyia mazoezi. Kwa mfano wa mchepuo wa teknolojia za mtandao wa kompyuta, tumejenga kituo cha kufanya mazoezi, na vifaa vya kituo hicho vyote ni vya kisasa."

Mikoa ya Henan, Zhejiang, Shandong inaongeza uhai na nguvu ya ushindani ya elimu ya ufundi wa kazi kwa njia ya kutumia ipasavyo raslimali za sekta mbalimbali kwenye sehemu mbalimbali. Hivi sasa makundi zaidi ya 20 ya mafunzo ya ufundi wa kazi yameanzishwa kwenye sehemu hizo, si kama tu shule elfu kadhaa za ufundi wa kazi zinaweza kufidiana, bali pia shule hizo zimejenga mawasiliano bora kati yao na makampuni.

Imefahamika kuwa, katika miaka mitano ijayo, elimu ya ufundi wa kazi itaandaa mafundi zaidi ya milioni 26, na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi zaidi ya milioni 400, hali hiyo itainua ubora wa wafanyakazi na kuboresha mundo wa ufundi wa kazi wa nguvu kazi. Hivi sasa, ili kukidhi mahitaji ya mafundi kutokana na mendeleo ya uchumi na jamii, elimu ya ufundi wa kazi ya China inaweka mkazo katika mradi wa taifa wa kuandaa mafundi, mradi wa taifa wa kutoa mafunzo kwa nguvu kazi ya watu vjijini wanaohamahama na mradi wa mafunzo wa kujiendeleza na ya kujiajiri tena. Wachambuzi wanaona kuwa, sekta ya elimu ya ufundi wa kazi imeingia kwenye enzi yenye fursa nyingi na maendeleo makubwa.