Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Kofi Annan tarehe 3 mwezi huu alimaliza ziara ya siku 2 nchini Iran. Bw. Annan ameitembelea Iran baada ya kupita tarehe iliyowekwa katika azimio la baraza la usalama la kuitaka Iran kusimamisha shughuli za kusafisha uranium. Mchambuzi alisema lengo la ziara yake ni kuhimiza mazungumzo kuhusu suala la nyukilia la Iran na kuepusha suala hilo kuwa na utata zaidi.
Katika ziara yake hiyo Bw. Annan alikuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw.Manochener Motaki, mwakilishi wa kwanza wa Iran katika mazungumzo ya nyukilia aambaye pia ni katibu wa kamati ya usalama wa taifa Bw. Ali Larijani, mwenyekiti wa kamati ya uthibitishaji wa maslahi ya taifa Bw. Akbar Hashemi Rafsanjani na rais Mahumd Ahmadinejad wa Iran. Katika mazungumzo hayo, pande mbili zinaona kuwa mazungumzo ni njia nzuri zaidi ya kutatua suala la nyukilia la Iran.
Lakini vyombo vya habari vinaona kuwa, Iran bado inashikilia msimamo wake kuhusu suala la nyukilia. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran ambaye ni mwakilishi wa nchi hiyo katika shirika la nishati ya atomiki duniani tarehe 3 mwezi huu rais Ahmadinejad wa Iran alipokuwa na mazungumzo na Bw. Kofi Annan alisema, Iran iko tayari kuwa na mazungumzo na jumuiya ya kimatiafa kuhusu suala la nyukilia, lakini alisisitiza kuwa Iran haitakubali kusimamisha kusafisha uranium kabla ya kufanyika kwa mazungumzo.
Vyombo vya habari vinaona kuwa, hivi sasa baraza la usalama la Umoja wa Matiafa linakabiliwa na changamoto kubwa la suala la nyukilia la Iran. Kutokana na uhasama mkubwa na mvutano mkubwa wa kimsimamo uliopo kati ya Iran na Marekani, ni vigumu kwa pande mbili husika katika suala la nyukilia la Iran kuamini, kuwa masuala mangi halisi yatatatuliwa katika ziara ya Bw. Annan. Ingawa kabla ya hapo Bw. Annan amekuwa akitaka Marekani itatue suala la nyukilia la Iran kwa utulivu, na kutaka Iran ifahamu matarajio ya jumuiya ya kimataifa kutoka kwake na kujitahidi kuifanya jumuiya ya kimataifa iwe na imani na Iran tena, lakini Marekani na Iran zote zinashikilia msimamo wake na kukataa kufanya usuluhisho. Iran si kama tu inakataa azimio la baraza usalama linaloitaka isimamishe kusafisha uranium, bali pia ilifanya luteka kubwa ya kijeshi na kufanya sherehe ya kuzinduliwa kwa kinu cha maji mazito ili kuonesha azma yake isiyobadilika kuhusu uendelezaji wa teknolojia ya nyukilia. Kwenye sherehe ya uzinduzi wa kinu cha wa maji mazito, rais Ahmadinejad alisisitiza kuwa watu wa Iran watalinda haki yao ya kuendeleza teknolojia ya nyukilia kwa nguvu za kijeshi. Wakati huo huo Marekani ilisisitiza mara nyingi kuwa baada ya kupita kikomo cha tarehe kilichowekwa katika azimio la baraza la usalama, endapo Iran haitasimamisha shughuli za kusafisha uranium, Marekani itahimiza baraza la usalama kupitisha azimio la kuiwekea Iran vikwazo, hata ilisema kuwa itachukua hatua peke yake bila kupitia Umoja wa Mataifa.
Aidha hivi sasa kuna maoni tofauti kati ya nchi wanachama wa baraza la usalama kuhusu suala la nyukila. Habari zinasema katika suala la kuiwekea vikwazo Iran, nchi nyingi haziungi mkono sana uwekaji wa vikwazo isipokuwa Marekani na Uingereza. Russia toka zamani haitaki Iran iwekewe vikwazo mara moja, wakati baadhi ya nchi za Ulaya ikiwemo Ufaransa zina wasiwasi mkubwa kuhusu kuweka vikwazo kwa kuhofia kuwa huenda hatua hiyo itabadilika kuwa mapambano kati ya nchi za magharibi na nchi za kiislamu.
Wachambuzi wanasema ingawa ziara ya Bw. Annan nchi Iran haiwezi kuondoa kimsingi mgongano kati ya Marekani na Iran, lakini wakati Marekani inapojiandaa kuhimiza kuweka vikwazo dhidi ya Iran, Bw. Annan bado anatarajia ziara yake nchini Iran itahimiza ushirikiano kati ya Iran na shirika la nishati ya atomiki duniani, hususan kutaka kufahamu masharti ambayo Iran inaweza kukubali kabla ya mazungumzo, ili kufanya kila awezalo kuzipatanisha na kuzisuluhisha.
Wachambuzi wanakadiria kuwa baada ya Bw. Annan kufanya ziara nchini Iran atasuluhisha maslahi ya pande mbalimbali za baraza la usalama na kujitahidi kufanikisha pande husika zishiriki kwenye mazungumzo ya suala nyukilia la Iran.
Idhaa ya Kiswahili 2006-09-04
|