Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-06 16:37:09    
Mapishi ya supu ya vipande vya nyama ya ng'ombe na figili

cri

Mahitaji

Nyama ya ng'ombe gramu 250, figili moja, chumvi gramu 10, mvinyo wa kupikia gramu 8, mchuzi wa sosi gramu 10, tangawizi gramu 5, vitunguu maji gramu 5.

Njia

1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, tia vipande vya nyama ya ng'ombe kwenye maji ya moto ili kuondoa damu, halafu ipakue. Ondoa gamba la figili na uikate iwe vipande.

2. kata tangawizi na vitunguu maji viwe vipande. Tia vipande vya tangawizi na vipande vya nyama ya ng'ombe kwenye sufuria mimina maji kasha yachemshe, baada ya kuchemka, punguza moto kidogo, tia mvinyo wa kupikia na mchuzi, endelea kuchemsha kwa nusu ya saa, pakua bakuli moja ya supu. Tia vipande vya figili, endelea kuchemsha. Baada ya dakika 20, tia bakuli hiyo ya supu. Baada ya saa mbili tia chumvi, tia vipande vya vitunguu maji. Ondoa mafuta kwenye supu. Ipakue mpaka hapo supu hiyo iko tayari kuliwa.