Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao tarehe 9 atafanya ziara nchini Finland na kuhudhuria mkutano wa 9 wa wakuu wa China na Umoja wa Ulaya. Mwandishi wetu wa habari hivi karibuni alimhoji balozi wa China katika Umoja wa Ulaya Bwana Guan Chengyuan.
Balozi Guan kwanza alijulisha mkutano huo wa wakuu wa China na Umoja wa Ulaya utakaofanyika tarehe 9. Alisema:
Mkutano huo unatokana na utaratibu muhimu wa majadiliano katika uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya, ambao utafanya mpango kutoka pande zote kuhusu uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya. Mkutano huo utajumuisha maendeleo ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya na masuala kadhaa yaliyoko tokea mkutano wa 8 wa wakuu wa China na Umoja wa Ulaya ufanyike. Wakati huo huo utaelekeza mwelekeo wa uhusiano kati ya China na Ulaya katika siku zijazo, kuthibitisha sera muhimu na hatua husika na kubadilishana maoni kwa kina kuhusu masuala ya kimataifa. Baada ya mkutano, China na Umoja wa Ulaya zitatoa taarifa ya pamoja kuhusu mambo mengi mbalimbali.
Balozi Guan alisema ushirikiano wa kimkakati na kiwenzi kati ya China na Umoja wa Ulaya umeingia katika kipindi kinachopevuka na kupata matokeo halisi. Pande hizo mbili zinajitahidi kutekeleza maoni ya pamoja yaliyofikiwa kwenye mkutano wa 8 wa wakuu wa China na Umoja wa Ulaya. Hasa zimeanzisha utaratibu wa mazungumzo ya kimkakati kila baada ya muda kati ya manaibu mawaziri wa mambo ya nje wa China na nchi za Umoja wa Ulaya, mkutano huo ulifanyika mara mbili mwezi Desemba mwaka jana na mwezi Juni mwaka huu.
Biashara ni sehemu muhimu ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya. Katika mwaka mmoja uliopita ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Umoja wa Ulaya umepata maendeleo ya haraka. Balozi Guan alisema:
Katika mwaka mmoja uliopita uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Umoja wa Ulaya uliendelea kwa haraka, ambapo thamani ya biashara iliongezeka kwa kiasi kikubwa. Ilipofika mwezi Juni mwaka huu, thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili iliongezeka kwa asilimia 20.8. Thamani ya makubaliano kuhusu kuingiza teknolojia kutoka Umoja wa Ulaya imechukua asilimia 42 ya ile ya jumla ya China, thamani hii imezidi ile ya makubaliano kuhusu China kuingiza teknolojia kutoka Marekani na Japan. Aidha viongozi wa China na Umoja wa Ulaya wameamua kwenye mkutano wa mwaka jana kuwa, kuanzia mwaka huu China na Umoja wa Ulaya zitaandaa mwaka wa sayansi na teknolojia za China na Umoja wa Ulaya. Baada ya maandalizi ya mwaka mmoja, shughuli za mwaka wa sayansi na teknolojia za China na Umoja wa Ulaya zitaanzishwa rasmi mwezi Oktoba mwaka huu, na mkutano wa wakuu wa China na Umoja wa Ulaya wa mwaka huu utatangaza kuanzishwa kwa shughuli hizo.
Ili kusukuma mbele zaidi maendeleo ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya, katika mwaka mmoja uliopita China imedumisha uhusiano wa kikazi na Kamati ya Umoja wa Ulaya, Baraza la Umoja wa Ulaya, Bunge la Ulaya na nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya. Balozi Guan alisema:
Katika mwaka mmoja uliopita, viongozi wa pande hizo mbili walitembeleana mara kwa mara, kwa mfano waziri mkuu wa nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya mwaka jana alifanya ziara isiyo ya rasmi nchini China, na mwaka huu amefanya ziara tena nchini China. Na zaidi ya nusu ya wajumbe wa kamati ya Umoja wa Ulaya wameitembelea China. Ziara hizo zimewapata watu wa Umoja wa Ulaya kumbukumbu nyingi na kuwawezesha wajionee mabadiliko ya China na maendeleo mapya yaliyopatikana nchini China siku hadi siku, hayo yameonesha umuhimu kwa maendeleo mazuri na ya utulivu ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.
Idhaa ya Kiswahili 2006-09-07
|