Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-08 16:23:30    
Urafiki wa dhati kati ya China na Afrika

cri

Balozi wa zamani wa China aliyekuwa nchini Afrika ya kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Bwana Cui Yongqian alifanya kazi ya kidiplomasia kwa zaidi ya miaka 30. Aliishi barani Afrika kwa miaka 15, na alizitembea nchi nyingi za Afrika, na aliwahi kukutana na marais, viongozi wa ngazi za juu na wakazi wengi wa kawaida, ambapo alijionea urafiki mkubwa kati ya wananchi wa China na nchi hizo za Afrika.

Balozi Cui alisema, alipofanya kazi nchini Guenea alikuwa anaweza kupata misaada kwa ukarimu kutoka kwa wakazi wenyeji wachangamfu. Siku moja Balozi Cui alipopotea njia kijana mmoja alijitolea kumwongoza, kijana huyo alitembea kwa miguu kwa karibu kilomita 6 kwenye njia mbovu iliyozunguka huku na huko, hatimaye balozi Cui alifika sehemu aliyotaka kwenda, kijana huyo alikuwa ametokwa na jasho jingi, balozi Cui alitaka kumshukuru kwa kumpa kifuta jasho, lakini kijana huyo alitabasamu tu, aliondoka bila kuchukua pesa alizopewa huku akisema , "kwa heri, mchina!"

Balozi Cui alipofanya kazi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alipotembea kwenye mitaa ya mijini au vijijini, wakazi wenyeji walipomwona yeye au wachina wengine walipenda kuwasalimia kwa lugha ya kichina japo walikuwa hawawezi kuongea vizuri lugha hiyo. Mwaka 2000 wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilipokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liliamua kutuma jeshi la kulinda amani nchini humo, mabalozi wa nchi 5 wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama waliwahi kwenda katika sehemu za mashariki na kaskazini za nchi hiyo zilizokumbwa na mgogoro ili kufahamu hali halisi ya huko, na kufanya usuluhishi. Jambo lililomshangaza ni kuwa walipokuwa katika sehemu ya mashariki na kaskazini mwa nchi hiyo kilomita zaidi ya 2000 kutoka mji mkuu Kinshasa, wakazi wote walimsalimia kwa lugha ya kichina "Ni Hao", maana yake ni hujambo. Wakazi wa huko hawatumii Kifaransa ambayo ni lugha ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wala Kiingereza ambayo inatumika sana huko, bali wanatumia lugha ya Kichina kuwasalimia mabalozi hao watano. Mabalozi wa Russia, Marekani, Uingereza na Ufaransa walipaswa kujibu kwa lugha ya Kichina "Ni Hao." Mabalozi wa Japan na Korea ya Kusini walioko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliwahi kumwambia Balozi Cui kuwa, kwa sababu wanafanana na wachina, hivyo walikuwa wanatambuliwa kama wachina.

Mwezi Aprili mwaka jana, kwenye michuano ya awali ya bara la Afrika ya kombe la dunia, timu ya Mali ilipambana na timu ya Togo, timu ya Mali ilishindwa. Baadhi ya watazamaji wa Mali walishindwa kudhibiti hisia zao za masikitiko, baadhi ya wahalifu walichukua fursa hiyo kuzusha vurugu mitaani, ambapo majengo mengi ya umma mjini Bamako yaliharibiwa, maduka mengi yakiwemo maduka zaidi ya 20 ya wachina yaliporwa. Wafanyabiashara wa China walikumbwa na hasara kubwa. Serikali ya Mali na maofisa wa ngazi ya juu wa nchi hiyo walifuatilia sana tukio hilo, rais Toumany Toure wa nchi hiyo alimtuma mara moja waziri wa mambo ya nje kuwaangalia wachina walioporwa. Kikundi maalum cha China kilipowasili nchini Mali, walikutana na rais, waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo. Rais Toure alisisitiza mara kwa mara kuwa, Mali na China ni marafiki wakubwa, watu wa nchi hizo mbili ni kama ndugu. Nchi hizo mbili hazina mgogoro ila tu urafiki.

Rais Toure alilaani vikali vitendo vya uhalifu vya kupora maduka, hasa maduka ya wafanyabiashara wa China. Alisema ingawa Mali ni nchi maskini, ina matatizo ya kiuchumi, lakini serikali yake itafanya chini juu kuwafidia wachina waliokumbwa na hasara. Wachina waishio nchini Mali walipoambiwa msimamo wa serikali ya Mali kuhusu tukio hilo walishukuru sana. Tukio hilo lilitatuliwa vizuri na wachina wanaishi pamoja na wenyeji kwa masikilizano zaidi.

Balozi Cui alisema japokuwa hayo ni mambo madogo, lakini yamethibitisha kuwa katika siku zilizopita, hivi sasa au siku zijazo, China na nchi za Afrika ni marafiki wakubwa wa kuungana mkono na kusaidiana. Wananchi wa China na wananchi wa nchi za Afrika ni marafiki, ndugu na washirika wazuri.

Idhaa ya kiswahili 2006-09-08