Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao tarehe 9 Septemba atakwenda Ulaya kuhudhuria Mkutano wa 9 wa wakuu wa China na Umoja wa Ulaya na mkutano wa wakuu wa Asia na Umoja wa Ulaya, pia atafanya ziara katika nchi 3 za Ulaya ikiwemo Finland.
Kabla ya kufunga safari waziri mkuu Wen Jiabao alidokeza kuwa, mktuano huo wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya utajadili suala kuhusu kusaini mapema iwezekanavyo "Makubaliano mapya kati ya China na Umoja wa Ulaya", ili ushirikiano kati ya pande hizo mbili usije ukabadilikabadilika kutokana na mabadiliko ya mambo fulani ya wakati fulani au mabadiliko ya viongozi. Dokta Hu Dawei wa Taasisi ya utafiti wa masuala ya kimataifa ya China alipozungumzia umuhimu wa mkataba huo mpya alisema:
Makubaliano mapya yatasainiwa badala ya "Makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na China" yaliyosainiwa mwaka 1985, kwani makubaliano hayo hayawezi kuonesha ushirikiano wa kina wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Umoja wa Ulaya uliopo kwa hivi sasa. Ili kuweka msingi imara wa kisheria kwa ajili ya kuendeleza vizuri na kwa kina uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya, kuna haja ya kufanya mazungumzo kuhusu kusaini makubaliano mapya, na mazungumzo hayo hakika yatasukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.
Dokta Hu Dawei anaona kuwa hivi sasa uhusiano kati ya China na Ulaya umeingia katika kipindi cha maendeleo mazuri na ya utulivu. Katika ziara hiyo ya Waziri mkuu Wen Jiabao nchini Finland, Uingereza na Ujerumani, makubaliano ya ushirikiano kwenye sekta mbalimbali kati ya China na nchi hizo tatu yatasainiwa. Dokta Hu alisema, hii itainua zaidi maendeleo ya uhusiano kati ya China na nchi za Umoja wa Ulaya. Alisema:
Umaalum wa uhusaino kati ya China na Ulaya ni kuwa uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya na kati ya China na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya uendelea sambamba, ni uhusiano unaohimizana na kusaidiana. Ushirikiano barabara na mawasiliano ya karibu kati ya China na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya umekuwa msingi imara wa uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya, ambapo nchi mbalimbali wanachama wa Umoja wa Ulaya pia zinajitaidi kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na China.
Lakini bado kuna migongano kadhaa kati ya China na Ulaya kuhusu masuala mbalimbali kama vile Umoja wa Ulaya kupiga marufuku kuiuzia China silaha, mikwaruzano ya kibiashara na kutambua hadhi ya uchumi wa soko huria ya China na kadhalika. Bwana Hu anasema ni lazima kutupia macho siku za mbele kuhusu uhusiano kati ya China na Ulaya. Alisema:
Njia ya kwanza yenye ufanisi zaidi ya kuondoa migongano hiyo ni kutambua migongano, kujadili vyanzo vya kihistoria na kiutamaduni vilivyosababisha migongano hiyo, wakati huo huo kuimarisha mazungumzo na mawasiliano ili kupata maoni ya pamoja, kuzingatia uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya kutokana na mtizamo wa maendeleo na mikakati, ili kushinda taabu zilizotokea katika mambo fulanifulani.
Waziri mkuu Wen Jiabao atahudhuria mkutano wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya, pia atahudhuria mkutano wa wakuu wa Asia na Umoja wa Ulaya. Dokta Hu anaona kuwa baada ya maendeleo ya miongo kadhaa, nguvu na uwezo wa China umeimarishwa siku hadi siku, hali hiyo imeongeza athari ya China duniani. Kuhudhuria mikutano hiyo kwa Waziri mkuu Wen Jiabao hakika kutaleta athari kubwa za mbali kwa uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya na kati ya Asia na Umoja wa Ulaya. Amesema katika hali ya utandawazi wa uchumi duniani, uchumi wa China unahusiana karibu zaidi siku hadi siku na uchumi wa dunia, waziri wa mambo ya nje wa Finland alisema, maendeleo ya China ni fursa ya dunia, hivyo Bwana Hu anaona kuwa Umoja wa Ulaya unapenda kufanya juhudi kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Umoja wa Ulaya.
Idhaa ya Kiswahili 2006-09-08
|