Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-11 14:46:03    
Ziwa la Baiyangdian

cri

Ziwa la Baiyangdian liko katika Wilaya ya Anxin mkoani Hebei, ambayo iko kwenye umbali wa zaidi ya kilomita 160 kutoka Beijing. Eneo la ziwa hilo ni kilomita 366 za mraba, ambapo kuna maziwa 143. Matete yaliyositawi yametapakaa kwenye eneo la ziwa hilo na kugawanya njia ya maji ya ziwa hilo kuwa sehemu ndogondogo zaidi ya 3700, wageni wakiingia kwenye sehemu hizo watapotea njia mara kwa mara. Kuhusu maziwa mengi kwenye sehemu ya Ziwa Baiyangdian, mwongozaji wa watalii Bi. Ren Li alituelezea hadithi moja akisema:

Hekaya aliyosimulia ilisema, wakati wa usiku wenye mbalamwezi, malaika Chang Er alikula dawa ya kuruka aliyopata mume wake, Chang Er aliporuka mbinguni, kioo cha hazina alichokuwanacho mfukoni kilianguka chini na kuvunjika kuwa sehemu 143, sehemu hizo zikawa maziwa makubwa na madogo yapatao 143 yaliyotapakaa kwenye sehemu hiyo.

Tukizungumzia Ziwa Baiyangdian, lazima tuzungumzie kwanza matete ya ziwani, matete hayo ni kama hazina ya ziwa hilo. Watu wa sehemu hiyo wanasema, kila tete ni kama kipande kimoja cha dhahabu. Kila ifikapo mwezi Agosti na Septemba, matete yanayopevuka yamekuwa ya rangi ya dhahabu na kujaa kwenye ziwa kubwa, ambapo mandhari ya ziwa inawavutia sana watu.

Matete ya Ziwa Baiyangdian yamegawanywa katika ngazi tatu, matete ya ngazi ya kwanza yanatumika kutengenezea mapazia, na matete ya ngazi ya pili yanatumiwa kutengeneza picha za sanaa ya matete, na matete ya ngazi ya tatu yanatumiwa kuwa raslimali ya kutegeneza karatasi au raslimali za nishati. Mizizi miteke ya matete inaweza kuchemshwa na kuwa supu na kutengenezwa kuwa pombe, na mizizi iliyokomaa inaweza kutumiwa kama dawa. Mashuke ya matete yanaweza kutengenezwa kuwa mifagio, na maua ya matete yanaweza kujazwa kwenye mto.

Mkazi wa sehemu hiyo Bibi Yang Xue anaendesha duka moja linalouza vitu vya sanaa ya mikono vilivyotengenezwa kwa matete, alisema vitu vilivyosukwa kwa matete si kama tu vinaweza kuwa zawadi ya kumbukumbu, bali vinaweza kutumiwa na watu. Watalii wakinunua kofia zilizosukwa kwa majani ya matete wanaweza kukwepa jua kali, na wakinunua viatu vilivyosukwa kwa majani ya matete kwa Yuan kadhaa wanaweza kutembea kwenye ziwa la Baiyangdian bila matatizo. Alisema:

Viatu vilivyosukwa na watu kwa majani ya matete haviwezi kuifanya miguu kuona joto, watu wakivaa wanaona raha.

Mbali na kuangalia matete bustani ya maua ya yungiyungi katika sehemu ya Ziwa Baiyangdian pia inawavutia sana watalii. Katika bustani hiyo yamepadwa maua ya yungiyungi tu. Kila ifikapo majira ya joto?maua ya yungiyungi yanachanua vizuri kwenye bustani hiyo na kuwavutia sana watalii, ambapo maji ya dimbwi la bustani hiyo, zaidi ya nusu imefunikwa na maua ya yungiyungi, majani ya maua yanaegemeana na kutandika kwenye uso wa maji, wakati upepo mwororo ukivuma, maua ya yungiyungi kwenye dimbwi hilo yanapepea kwa pamoja, hali ya kupendeza inafurahisha kweli.

Ndani ya dimbwi la maua ya yungiyungi kuna njia moja nyembamba iliyojengwa kwa mawe, watalii wanaweza kutembea kwenye njia hiyo na kupiga picha, kwa kuwa njia hiyo nyembamba hufunikwa na maua na majani, hivyo watalii wakitembea kwenye njia hiyo kama wanatembea juu ya maua ya yungiyungi. Msichana Zhao Jie kutoka Beijing aliyefika huko kutazama maua ya yungiyungi alisema:

Bustani hiyo ya maua ya yungiyungi kweli inatuvutia sana, sijawahi kuona maua mengi namna hii, kwenye bustani hiyo naona maua ya yungiyungi ni mazuri sana, nilipiga picha nyingi ili kuwafurahisha marafiki zangu.

Miongoni mwa maua mengi ya yungiyungi katika bustani hiyo, kuna aina moja ya maua ya yungiyungi inayowavutia sana watu ambayo kwenye tawi moja yanachanua kwa pamoja maua mawili ya yungiyungi. Maua ya yungiyungi ya aina hiyo ni yenye thamani kubwa na ni nadra kupatikana duniani. Nchini China maua kama hayo yanamithilisha mapenzi kati ya mume na mke. Mwongozaji wa utalii wa Ziwa Baiyangdian Bi. Ren Li alisema, kuhusu chanzo cha maua hayo kuna hadithi moja inayowavutia watu katika sehemu hiyo. Alisema:

Zamani katika sehemu hiyo kulikuwa na kijana mmoja aitwaye Shuisheng, mke wake alikuwa ni mrembo. Siku moja Shuisheng alipokwenda nje kuvua samaki, mkorofi mbaya wa kijiji chake alikwenda nyumbani kwake kumbaka mke wake, mke wake aliona huzuni kubwa akajitosa mtoni akafa. Kijana Shuisheng alighadhabika sana na akamwua mkorofi huyo mbaya, halafu pia alijitosa mtoni akafa. Baada ya siku kadhaa, katika sehemu waliojitosa mtoni, yakaota maua ya yungiyungi, ambayo kwenye tawi moja yalichanua kwa pamoja maua mawili ya yungiyungi, wakazi wa huko waliyapa maua hayo jina la Bingdilian, maana yake ni mapenzi ya kudumu.

Hadithi hiyo ya zamani haiwezi kuthibitishwa, lakini imewawezesha watu waone hali ya ajabu kwenye sehemu ya Ziwa Baiyangdian. Mwandishi wetu wa habari alipotembelea sehemu hiyo alipanda mashua akiangalia mandhari ya ziwa, aliona ukungu ukielea kwenye uso wa maji, na matete yenye urefu wa mita 3 yaliyositawi kwenye ziwa hizo yaliwafanya watalii wasiweze kuona hali ya mbali na ndani ya ziwa. Mashua aliyopanda ilifuata njia ya mto iliyogawanyika kwa sehemu ya matete, alipofika kwenye sehemu yenye uso mpana wa maji, aliona wavuvi wa huko wakivua samaki kwa njia iliyotumiwa na watu wa zamani sana, ambapo mvuvi mmoja mzee aliyevaa kofia ya matete alipopiga mwanzi wake mtoni, mara ndege wa majini waliosimama kwenye safu moja kwenye mashua walipiga mbizi kwa haraka majini, waliporudi kwenye mashua, kila mmoja alikuwa na samaki mmoja mdomoni. Zamani wavuvi wa Ziwa Baiyangdiam walitegemea kazi ya uvuvi ili kujikimu kimaisha, lakini hivi sasa wakazi wengi wa sehemu hiyo wanashughulikia mambo ya utalii, kila siku wanatumia mashua zao za uvuvi kuwapokea na kuwapeleka watalii kuingia na kutoka Ziwa Baiyangdian. Mwongozaji Bi.Ren Li alisema:

Kijiji cha wavuvi kimejengwa kwenye kisiwa, hivyo kila familia ina mashua yake. Na mashua hizo zote zinaendeshwa kwa mikono, na baadhi ya wanakijiji walifunga injini kwenye mashua ili kuwapeleka watoto wao shuleni au kuwapokea wakitoka shuleni.

Watalii wakifika sehemu ya Ziwa Baiyangdian wasikose fursa ya kuonja vyakula vya samaki vya sehemu hiyo. Vyakula vya Samaki vilivyopikwa kwenye mikahawa ya sehemu hiyo vina ladha nzuri sana na virutubisho vingi. Watalii wakiwa na nafasi ya kutosha, wanaweza kuwafuata wavuvi kuvua samaki mtoni, halafu wakaingia kwenye mkahawa wowote unaoendeshwa na wanakijiji wa huko, ambapo wapishi wanaweza kupika samaki waliovuliwa katika muda mfupi. Na vyakula vingine vilivyopikwa na wenyeji wa sehemu ya Ziwa Baiyangdian kutumia mazao ya kilimo na samaki waliofugwa huko pia vinawavutia sana watalii.

Idhaa ya Kiswahili 2006-09-11