Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-11 19:30:38    
Mkutano wa 6 wa wakuu wa Asia na Umoja wa Ulaya wafunguliwa

cri

Mkutano wa 6 wa wakuu wa Asia na Umoja wa Ulaya ulifunguliwa tarehe 10 alasiri huko Helsinki, mji mkuu wa Finland. Kwenye mkutano wa siku mbili, viongozi wa nchi 39 wanachama wa Baraza la Asia na Umoja wa Ulaya ikiwemo China watajadili masuala mbalimbali yanayohusu kauli mbiu ya mkutano huo "Kushirikiana ili kukabiliana na changamoto kote duniani".

Alasiri ya siku hiyo wakuu wa nchi au serikali wa nchi 10 wanachama wa Asia ya kusini mashariki, nchi 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya pamoja na China, Japan na Korea ya kusini na viongozi wa kamati ya Umoja wa Ulaya walihudhuria ufunguzi wa mkutano wa 6 wa wakuu wa Asia na Umoja wa Ulaya. Rais Tarja Halonen wa Finland ambayo ni nchi mwenyekiti wa mkutano huo alitoa hotuba akikumbusha maendeleo makubwa yaliyopatikana katika miaka 10 iliyopita tangu Baraza la Asia na Umoja wa Ulaya lianzishwe. Alisema: 

Mwaka 1996 nilipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Finland nilihudhuria mkutano wa kwanza wa wakuu wa Asia na Umoja wa Ulaya. Wakati huo nchi mbalimbali zilikuwa hazina shauku ya kufanya mawasiliano, kwani zilikuwa zinaanza tu kuwasiliana na kuwa na maingiliano. Lakini mkutano huo ulipata mafanikio, na ulitandika njia ya kufunguliwa mlango na ushirikiano wa hivi leo kwenye sekta mbalimbali halisi. Miaka 10 imepita, baraza hilo limekuwa baraza la kufanya ushirikiano na mazungumzo kati ya Asia na Ulaya. Mazungumzo ya kisiasa kati ya pande hizo mbili yanahusiana na mambo mengi mbalimbali, ambapo mawasiliano ya kiuchumi yanaimarishwa, na ushirikiano kati ya sekta za jamii na utamaduni unaongezeka siku hadi siku.

Mkutano wa Asia na Umoja wa Ulaya una nia ya kuimarisha na kukamilisha utaratibu wa ushirikiano wa pande mbalimbali duniani, kuweka hali mwafaka kwa maendeleo ya uchumi na jamii, na kulinda amani na maendeleo ya dunia. Katika hali ya hivi sasa ambayo dunia nzima inakabiliwa na tishio na changamoto kubwa za uhalifu wa kuvuka mipaka, mazingira yanazidi kuwa mbaya, na nishati zinapungua siku hadi siku, mkutano huo utajadili hasa masuala kuhusu kuimarisha utaratibu wa ushirikiano wa pande mbalimbali na kukabiliana na changamoto dhidi ya usalama, utandawazi wa uchumi duniani na ushindani, usalama wa nishati na mabadiliko ya hali ya hewa, na mazungumzo kati ya nchi zenye utamaduni na ustaarabu tofauti. Waziri mkuu wa Finland Bwana Matti Vanhanen alipohotubia alisisitiza umuhimu wa kuimarisha utaratibu wa Umoja na ushirikiano ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia nzima. 

Mazungumzo kati ya nchi zenye utamaduni na ustaarabu ni mada muhimu kwenye mkutano huo. Nchi na sehemu zinazohudhuria mkutano wa wakuu wa Asia na Umoja wa Ulaya zina utamaduni wa aina mbalimbali, hayo yanasaidia kuhimiza watu wenye ustaarabu, utamaduni au uamini wa dini tofauti wafanye mazungumzo. Naamini kuwa mazungumzo hayo yanasaidia kuongeza maelewano na mapatano, na kuondoa uelewa wa makosa kati ya watu hao. Aidha yanasaidia kuzuia nguvu za mabavu kwa kisingizio cha dini.

Hivi sasa idadi ya watu wa nchi wanachama wa Baraza la Asia na Umoja wa Ulaya inachukua zaidi ya theluthi moja ya ile ya jumla duniani kote, na thamani ya jumla ya uzalishaji mali imezidi nusu ya ile ya jumla ya duniani. Waziri mkuu wa Vietnam Bwana Nguyen Tan Dung alipotoa hotuba alisema, maendeleo mazuri ya baraza hilo yameleta manufaa kwa pande mbili za Asia na Umoja wa Ulaya na kusukuma mbele maendeleo endelevu ya jamii na uchumi wa pande hizo mbili, pia kutoa mchango katika kuanzisha utaratibu mpya duniani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Bwana Jose Manuel Barroso alipohotubia alisisitiza kuwa, tunapaswa kutupia macho siku za mbele. Katika miaka 10 iliyopita mkutano wa wakuu wa Asia na Umoja wa Ulaya umetoa mchango mkubwa kwa kuendeleza zaidi uhusiano wa pande mbili, tunatarajia mkutano wa safari hii utapata matunda kemkem ili kutandika njia kwa ajili ya kuendeleza ushirikiano wa kiwenzi wenye nguvu zaidi.