Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-11 19:36:36    
Kwanini mapambano dhidi ya ugaidi duniani yameleta tishio kubwa zaidi?

cri

Leo miaka mitano imetimia tangu tukio la mashambulizi ya kigaidi ya tarehe 11 Septemba litokee, lakini jeraha lililosababishwa na mashambulizi hayo duniani bado halijapona. Jitihada za jumuiya ya kimataifa dhidi ya ugaidi hazikusita hata siku moja, lakini ugaidi duniani umezidi kuongezeka. Lakini ni kwanini hali ya namna hiyo imetokea? Mwandishi wetu wa habari alimhoji mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya kigaidi ya taasisi ya utafiti wa uhusiano wa kimataifa wa hivi sasa ya China Bw. Li Wei, kuhusu jambo hilo.

Tovuti ya habari za televisheni ya cable ya Marekani hivi karibuni ilionesha filamu moja ya habari ikisema, "wakati mashambulizi ya 9.11 yanafanyika kulikuwa na Bin Laden mmoja, lakini baada ya tukio la 9.11 kumekuwa na kina Bin Laden 1,000. Bw. Li Wei anaona, chanzo kubwa la kutokea hali ya namna hii ni jumuiya ya kimataifa kutofahamu vizuri maana ya ugaidi.

"Hivi sasa bado hakuna maoni ya namna moja kuhusu maana halisi ya ugaidi. Baadhi ya nchi hazizingatii maslahi ya jumuiya ya kimataifa, bali zinafanya vitendo mbalimbali kutokana na maslahi ya nchi yake duniani, hivyo zinaweza kutenda vitendo vinavyohusiana na siasa za kimwamba, uongozi wa kimwamba, hata kuangusha serikali ya nchi nyingine kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, kuimarisha nguvu ya athari yake duniani au kupora raslimali za mafuta ya petroli duniani. Hali halisi ya masuala hayo kwa upande mwingine ni kama kunainua nafasi za kujiendeleza kwa ugaidi."

Bw. Li Wei alisema chanzo cha malumbano kwenye jumuiya ya kimataifa kuhusu maana ya ugaidi na kushindwa kuafikiana kwenye maoni ya namna moja, ni kuwa kila nchi inapigania maslahi yake tu.

"Hivi sasa tunasema kuna maoni tofauti kuhusu ugaidi, vilevile kuna matatizo mengine husika, likiwemo tatizo la kutumia vigezo viwili kuhusu ugaidi, ambalo ni tatizo la kimsingi kabisa la kupambana na ugaidi kwa jumuiya ya kimataifa, hivyo mara kwa mara Umoja wa Mataifa ulitaka nchi wanachama zithibitishe kigezo cha namna moja kuhusu ugaidi ili kuifanya jumuiya ya kimataifa iweze kuwa na nia moja katika mapambano dhidi ya ugaidi na kuratibu vizuri hatua za kupambana na ugaidi, lakini naona kuwa suala hilo haliwezi kutatuliwa kwa muda mfupi".

Bw. Li Wei alisema chanzo kingine cha kutokea hali ya namna hiyo ni kuwa baadhi ya nchi bado hazijapata njia sahihi ya kupambana na ugaidi. Kwa mfano zinapuuza umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika mapambano dhidi ya ugaidi duniani. Mwaka 2003, Marekani ilianzisha vita dhidi ya Iraq bila kujali upinzani wa Umoja wa Mataifa kwa kisingizio kuwa Iraq ilikuwa na silaha nyingi za kuhilikisha umma. Hadi sasa mashambulizi ya nchini Iraq dhidi ya Marekani yamesababisha vifo vya askari 2,600 wa Marekani, ambapo Iraq imekuwa sehemu mpya ya kuzalisha ugaidi. Kuhusu suala hilo, Bw. Li Wei alisema, mapambano ya Marekani dhidi ya ugaidi kwa kiwango fulani yanachangia kuongezeka kwa nguvu za magaidi.

"Marekani ilishambulia Iraq bila idhini ya Umoja wa Mataifa, na kuifanya Iraq iwe sehemu mpya ya kufanya propaganda, kuandikisha wanachama na kutoa mafunzo kwa wanachama wapya wa makundi ya kigaidi, si kama tu imevutia magaidi walioko sehemu mbalimbali duniani, bali pia inapeleka magaidi kwenye sehemu nyingine."

Bw. Li Wei alisema chanzo kingine ni kwamba vitendo vya baadhi ya nchi katika mapambano dhidi ya ugaidi vilizidisha upinzani wa nchi zenye dini na tamaduni tofauti. Alisema kwenye uwanja wa vita nchini Iraq, gereza la Guantanamo, matukio ya udhalilishaji wa wafungwa, kudhalilisha Qorani, kashfa za gerezani ikiwemo askari wa Marekani kuua watu ovyo nchini Iraq, michoro ya katuni kuhusu mambo ya dini barani Ulaya, vimezidisha kukabiliana kiuhasama, na mambo hayo pia yalitumiwa na magaidi ambao wanaeneza habari hizo ili kuweza kuandikisha vijana wengi zaidi."

Bw. Li Wei alisema baadhi ya nchi kuchukua msimamo wa upendeleo katika shughuli za kimataifa na kulenga baadhi ya makundi maalumu ya watu katika mapambano dhidi ya ugaidi pia vinazidisha nguvu za ugaidi duniani.