Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-12 15:11:20    
Barua 0912

cri

Msikizaji wetu Stephen Magoye Kumalija wa S.L.P 1067 Kahama, Tanzania ametuletea barua akisema kuwa, ana tumaini kuwa wafanyakazi wote wa idhaa ya kiswahili wa Redio China Kimataifa hawajambo. Yeye pamoja na marafiki zake wanapenda kutumia fursa hii kuwapa pole marafiki zao wachina waliokumbwa na kimbunga katika sehemu za kusini mashariki mwa China bara pamoja na katika kisiwa cha Taiwan ambacho ni kisiwa cha hazina ya China.Msikilizaji Wema Kumalija anawapa pole za dhati wachina wote waliokubwa na janga hilo la kimaumbile lililosababisha vifo vya wachina wengi ambao ni nguvu kazi na tegemeo la ujenzi wa jamhuri ya watu wa China. Anasema kazi ya Mungu haina makosa na anamuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Bwana Stephen anawatakia kila la Kheri na ufanisi kazini wafanyakazi wote wa idhaa ya kiswahili wa Radio China Kimataifa.

Msikizaji wetu Stephen Magoye Kumalija pia ametuletea Hadithi moja inayoitwa: Busu La Utumwa, hadithi hiyo inauliza kuwa, Mahabusu ni wapi? Bahati alijibu kwa sauti iliyojaa simanzi, mahabusu ni chumba wanachowekwa watuhumiwa. Akasema naomba niende huko nikatoe shukrani zangu kwa Mongi, hata wazazi wangu sijui sijui kama wapo hai au laa!! Hapana Bahati unaumwa na unatumia dawa hutaweza kuondoka. Ukipona vizuri utaenda kumsalimu. Nitashukuru daktari. Daktari akasema usihofu, pengine Mongi ndiye wa kumpa shukrani nyingi.

Lilikuwa ni jambo la kushangaza kwa Bahati, kwani hakuwahi kupata msaada kutoka kwa mtu yeyote. Aliamini kuwa ameumbwa kwa shida na mateso, hakutegemea kuwa kuna wanadamu wanaoweza kupata mateso kama hayo. Askari alipofungua mlango aliita, Mongi vaa viatu toka nje twende chumba cha upelelezi ukajieleze tayari kwa kwenda mahakamani kesho. Kwanza mwanzoni alihisi alikuwa anaachiwa na kufutiwa kesi, lakini sentensi ilipomalizika alinyong'onyea, mbaya zaidi aliwaona marafiki zake Benson na Lilian wakiwa wanamtizama.

Aliingizwa kwenye chumba cha upelelezi kuhojiwa, aliyekuwa mpelelezi wa kesi yake alijulikana kwa jina la afande Kinyo.Wewe ndio Mongi? Afande Kinyo alimuuliza kwa macho ya udadisi, ndio afande! Mongi alijibu kwa sauti chini sana, hakuamini sauti yake ilitokaje ambayo ilikuwa ya huzuni. Kaa chini upesi, wenzako wanajitahidi kuliongezea taifa fedha za kigeni wewe unaharibu. Sasa tutakufunga, haya sema ukweli wako wote, ukisema uongo tutakufunga. Bwana Kumalija anasema hiyo ndiyo hadithi yake, hadithi ni ndefu sana ila tu ameona aikatishe.

Bwana Kumalija pia alitutumia barua nyingine ambayo tulichelewa sana kuipata, kwenye barua hiyo alizungumzia mambo ya kombe la dunia lililofanyika miezi mitatu iliyopita. Kwenye abrua hiyo almepongeza wachezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani waliokusanyika huko Ujerumani kugombea Kombe la dunia.

Hata hivyo Bwana Kumalija hakufuatilia vizuri maendeleo ya China kwenye michezo ya awali ya kombe la dunia, kwa hiyo yeye alidhani kuwa timu ya China ilipata nafasi ya kushiriki kwenye fainali za kombe hilo. Hata hivyo anawatakia ndugu, marafiki wapenzi wa wanamichezo wa China mafanikio makubwa katika michezo mbalimbali.

Tunamshuku sana msikilizaji wetu Bwana Kumalija kwa barua yake ingawa tumechelewa kuipata, lakini tunatiwa moyo na ushabiki wake kwa michezo na hisia zake kwa wanamichezo wa China. Asante sana.

Msikilizaji wetu Richard Chenibei Mateka wa S.L.P 65 Kapkateny nchini Kenya ametuletea barau akitoa salamu zake kwa watangazaji na wasikilizaji wa Radio China kimataifa kutoka nchini Kenya, anasema matangazo na vipindi vya radio China kimtaifa vinaendelea kunawiri na wasikilizaji wanaongezeka maradufu. Anatoa shukrani kwa Radio China kimataifa kufungua kituo cha mtangazo jijini Nairobi kinachorusha matangazo kwa masafa ya FM.

Bwana Mateka anaiomba Radio China Kimataifa ifungue kituo kingine cha matangazo mjini Eldoret ili kuweza kustawisha vipindi na matangazo. Ili pia wakazi wa huko waweze kupata huduma ya karibu kwani matangazo huenda na biashara kwani watalii wengi kutoka China hufika kwa wingi mjini Eldoret. Pia anaiomba idhaa ya kiswahili kama ina uwezo wa kuwapa posta card na majarida ili waweze kujua matukio yanayotekea nchini China, pia anawahimiza watangazaji wa idhaa ya kiswahili wazidishe bidii kwani wakenya wananufaika sana na matangazo ya Radio China Kimataifa.

Bwana Mateka anaamini kuwa mwaka huu watalii watafika kwa wingi sana kwenye Mlima Elgon. Anaomba wafanyabiashara wa China kama wakipenda, kupitia idhaa ya kiswahili ya Radio China Kimataifa wanaweza kuwasiliana naye kwa anuani yake, ili waweze kushirikiana nae. Anasema kuna nafasi za biashara ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa abiria na mizigo, kujenga shule za binafsi, hospitali, pamoja na biashara ya bidhaa na huduma nyingine muhimu. Anaona kuwa hii itasaidia kuleta maendeleo katika wilaya za Mlima Elgon, Bungoma, Busia na Eldoret, na mwisho anaomba ushirikiano na urafiki kati ya wachina na wakenya uzidi kudumishwa, na wachina wawe huru kutembelea Kenya, kwani urafiki ni maendeleo.

Tunamshukuru Bwana Richard Chenibei Mateka kwa barua yake inayoeleza hisia zake kwa wananchi wa China, na ushauri wake mzuri, lakini kweli bado kuna njia ndefu ya kutimiza lengo la kupanua matangazo yetu kwenye mawimbi ya FM, kazi yetu muhimu ya hivi sasa ni kuwa, tunapaswa kufanya juhudi kuboresha vipindi vyetu, kuongeza vipindi vinavyowafurahisha wasikilizaji wetu, ni matumaini yetu kuwa wasikilizaji wetu watatusaidia.

Msikilizaji wetu Anna Chemonges wa Eldoret Nchini Kenya anatoa pongezi kwa wafanyakazi wa Radio China Kimataifa, bila kusahau kupongeza kutokana na kusomwa kwa salamu zake ambazo anazituma kupitia Radio China Kimataifa. Anasema saa moja usiku ya tehehe 28 mwezi Mei mwaka 2006 alitembelewa na mgeni anayemfahamu vizuri Bwana Ayub Mutanda Sharifu wa Bungoma nchini Kenya. Baada ya kupumzika kwa muda kutokana na uchovu wa safari yake alianza kutusimulia lengo la safari yake. Alisema yeye ana habari kuhusu Radio china Kimataifa ambayo ndio lengo la safari yake.

Jambo lilimshangaza msikilizaji wetu huyu ni jinsi Bwana Sharifu alivyoweza kuendesha baiskeli katika barabara inayopita magari makubwa kutoka mjini Bungoma hadi mjini Eldoret. Baiskeli aliyotumia ilikuwa haina tochi lakini kutokana na maelezo yake ni kuwa alitumia mwanga wa simu yake ya mkononi.

Na walipomwuliza kama hiyo kama idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa inamlipa au imemwajiri, alisema hapana, alisema anafurahi kupata zawadi kutoka Radio China kimataifa na ana matumaini kuwa siku moja ataweza kutembelea Beijing au ataweza kuhusishwa na kazi zake. Na hivi karibuni ataweza kutembea na kuendesha baiskeli kwenye sehemu mbalimbali za mkoa wa magharibi kuwafahamisha watu na kuwavutia waisikilize matangazo ya Radio China Kimataifa kama yeye.

Tunamshukuru msikilizaji wetu Anna Chemonges kwa barua yake iliyotusimulia kuhusu Bwana Sharif ambaye ni msikilizaji wetu mtiifu kweli, kwa jinsi anavyopenda kusikiliza idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa na kuisaidia kuwavuta wasikilizaji wengi. Tumetiwa moyo sana na juhudi zake, kweli kutokana na uungaji mkono wa wasikilizaji wetu, tunaweza kuchapa kazi zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasikilizaji wetu.

Idhaa ya kiswahili 2006-09-12