Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya kidiplomasia na sera za usalama Bw. Javier Solana na mwakilishi mkuu wa Iran kwenye mazungumzo ya suala la nyukilia Bw. Ali Larijani hivi karibuni walikuwa na mazungumzo. Inasemekana kuwa mazungumzo hayo yalipata baadhi ya mafanikio na kufuatiliwa na vyombo vya habari. Mchambuzi alisema, unyumbufu uliooneshwa na Umoja wa Ulaya baada ya tarehe 31 mwezi Agosti umefanya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuelekea kupinga kuchukua hatua ya kuiwekea vikwazo Iran. Baadhi ya watu wengine wanasema, baada ya kutafakari sana, umoja wa Ulaya unajaribu kufanya kazi muhimu za kipekee zilizo tofauti na za Marekani kuhusu suala la nyukilia la Iran.
Tangu Marekani iwe na wasiwasi na tabia ya amani ya mpango wa nyukilia wa Iran mwezi Machi mwaka 2003, mabadiliko mengi yalitokea kuhusu suala la nyukilia la Iran, ambapo katika wakati fulani karibu ulizuka mgogoro mkubwa. Kwa kutupia macho mambo yaliyotokea katika kipindi hicho kuhusu suala la nyukilia la Iran, watu wanaona Ulaya ambayo ni upande unaohusika na pia ni msuluhishi ilifanya kazi muhimu.
Nchi 3 za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zinazouwakilisha Umoja wa Ulaya, baada ya kufikiria kuwa ukaguzi wa silaha za Iraq zinazokiuka kanuni haukuweza kuiepusha Marekani kuanzisha vita, ziliamua kujitokeza kuongoza usuluhishi wa suala la nyukilia la Iran, zikijaribu kupata ushirikiano wa Iran kwa njia ya kutosheleza matakwa ya haki ya Iran kuhusu suala la nyukilia kwenye mazungumzo ili kuondoa kisingizio cha kuzusha mgogoro kwa Marekani. Nchi hizo tatu ziliafikiana na Iran kwenye "Mkataba wa Paris" mwezi Novemba mwaka 2004, na Iran ikasimamisha shughuli zake za kusafisha uranium tarehe 22 mwezi huo. Mafanikio ya mwanzo ya usuluhishi huo yanaonesha kosa la sera za Marekani na mafanikio ya uzoefu wa Umoja wa Ulaya wa kutekeleza msimamo mmoja wa kidiplomasia.
Ingawa Marekani imekuwa ikitekeleza sera thabiti dhidi ya Iran, lakini haikupata ufanisi wowote katika muda mrefu uliopita. Vita ya Iraq inaifanya Marekani ibanwe na matatizo, na haina uwezo tena wa kuanzisha vita nyingine ambayo haina uhakika na matokeo yake. Licha ya hayo mpasuko mkubwa uliotokea katika uhusiano wa pande mbili za bahari ya Atlantiki kutokana na vita ya Iraq, unaifanya Marekani ione kuwepo kwa haja ya kuuondoa kwa vitendo halisi. Mawazo hayo yanaihimiza Marekani irekebishe sera zake kuhusu Iran: mwezi Machi mwaka 2005 Marekani ilitangaza kuunga mkono Umoja wa Ulaya kuwa na mazungumzo na Iran kuhusu suala la nyukilia. Marekani kujisogeza kwenye msimamo wa Umoja wa Ulaya ni mafanikio ya hatua ya kwanza ya wazo la kidiplomasia la Umoja wa Ulaya.
Lakini mabadiliko yalitokea kuanzia mwezi Agosti mwaka 2005 baada ya kuchaguliwa serikali mpya ya Iran inayoongozwa na Mahmoud Ahmadinejad. Iran ilirudisha shughuli za nyukilia na kutangaza kufanikiwa kuzalisha uranium nzito ya kiwango cha chini. Vitendo vya Iran siyo tu kwamba vilikiuka kikomo kilichowekwa na nchi za magharibi, bali iliufedhehesha Umoja wa Ulaya, Umoja wa Ulaya ukasimamisha mazungumzo kati yake na Iran. Tokea hapo, msimamo wa ukaidi wa Iran uliuhimiza Umoja wa Ulaya ujisogeze kwa Marekani na kutenda vitendo kwa kushirikiana na Marekani mara kwa mara, ambapo iliipa Marekani nafasi ya kujitokeza upya kuongoza kwenye suala la nyukilia la Iran. Hata hivyo majadiliano makali kuhusu kuchukua msimamo wa thatibi au msimamo wa usuluhishi, hayakusimama ndani ya Umoja wa Ulaya.
Majadiliano hayo makali ndani ya Umoja wa Ulaya yalipamba moto zaidi baada ya kufikia kikomo kilichowekwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa cha kutaka Iran iache kusafisha uranium kabla ya tarehe 31 mwezi Agosti, hususan kuhusu kuiunga mkono Marekani kuiwekea vikwazo Iran au la. Hali ya hivi sasa inaonesha kuwa nchi nyingi za Umoja wa Ulaya zimetambua kuwa kuweka vikwazo kutaleta hasara kwa pande zote mbili; Tena njia hiyo itaifanya Iran iwe imara zaidi katika kuendeleza teknolojia ya nyukilia, na zinatumai kuipa nafasi moja nyingine Iran.
Wachambuzi wanaona kuwa, pengine yatatokea mabadiliko katika suala hilo, endapo Iran itakataa kurekebisha msimamo wake hadi kumaliza uvumilivu wa Umoja wa Ulaya, kutakuwa na uwezekano wa Umoja wa Ulaya kujisogeza kwa mara nyingine kwa Marekani.
|