Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-13 19:26:16    
Mkutano wa 61 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa wa mwaka wafuatiliwa zaidi na watu

cri

Mkutano wa 61 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa ulifunguliwa tarehe 12 huko New York, makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kwenye mkutano huo, mada za jadi na masuala mengi kuhusu kutekeleza zaidi "Waraka wa matokeo" wa mkutano wa wakuu duniani, uchaguzi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na masuala mengine makubwa ya kikanda yatajadiliwa kwa pamoja, hivyo yameleta taabu kubwa.

Wakati wa kufanyika kwa mkutano wa mwaka jana, uliitishwa mkutano wa wakuu duniani, hivyo masuala mengi ya kimataifa ambayo yangejadiliwa kwenye mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa yaliwekwa kando kwa kiasi fulani. Tokea majira ya siku ya joto ya mwaka huu, suala kuhusu mageuzi ya Umoja wa Mataifa, suala la maendeleo na suala la mapambano dhidi ya ugaidi na masuala mengine yameonekana dhahiri siku hadi siku. Wakati huo huo masuala mengine yanayofuatiliwa zaidi na watu kama vile suala la nyuklia la Iran, suala la mashariki ya kati na suala la Darfur la Sudan pia yako katika kipindi muhimu cha utatuzi, ambapo nchi mbalimbali zinayafuatilia sana masuala hayo, hivyo masuala hayo hakika yatajadiliwa zaidi kwenye mkutano wa mwaka huu. Kutokana na makadirio ya hatua ya mwanzo ya Umoja wa Mataifa, kuna mada zaidi ya 150 kwenye mkutano wa Baraza la kuu la Umoja wa Mataifa wa mwaka huu, mada hizo zinahusu amani na usalama, maendeleo, haki za binadamu, misaada ya kibinadamu, kuhimiza utaratibu wa kisheria, kupambana na ugaidi, kupunguza silaha na yale yanayohusu mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Aidha kwa kuwa katika utekelezaji wa "Waraka wa matokeo" wa mkutano wa wakuu, masuala kadhaa yenye migongano na taabu bado hayajatekelezwa, yakiwemo yale yanayohusu mageuzi ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na mageuzi ya ofisi ya sekretarieti, kutunga mkataba wa kupambana na ugaidi kutoka pande zote, kutekeleza malengo ya maendeleo ya milenia, pamoja na masuala yale kuhusu kutoeneza nyuklia, kupunguza silaha , na biashara ya haki. Watu wa nchi mbalimbali duniani wanatarajia masuala hayo yatatatuliwa kwa kiasi fulani kwenye mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Kutokana na hayo inakadiriwa kuwa, wakuu wa mataifa au viongozi wa serikali kati ya 80 na 90 watahudhuria mkutano huo. Na waziri wa mambo ya nje wa China Bwana Li Zhaoxing atatoa hotuba kwenye Baraza kuu la Umoja wa Mataifa ili kueleza msimamo wa serikali ya China kuhusu masuala kadhaa makubwa duniani.

Zaidi ya hayo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Kofi Annan atakamilisha muda wake wa madaraka mwishoni mwa mwaka huu, hivyo kwenye mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka huu, suala la uchaguzi wa katibu mkuu mpya pia litajadiliwa. Hivi sasa nchi 5 za Asia za Korea ya kusini, Thailand, Sri lanka, India na Jordan zimechagua wagombea wao wa wadhifa wa katibu mkuu, na huenda nchi nyingine kadhaa pia zitateua wagombea wao. Ndiyo maana uchaguzi wa katibu mkuu utafuatiliwa zaidi kwenye mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Na mwenyekiti wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa la mwaka huu Bibi Haya Khalifa ni mwenyekiti mwanamke anayejitokeza katika miaka 36 iliyopita. Bibi Khalifa anafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa namna atakavyofuata nyazo zilizoachwa na wenyeviti wa awamu zilizopita, na kulifanya Baraza kuu la Umoja wa Mataifa la awamu hii lisonge mbele katika kukabiliana na changamoto mbalimbali. Katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa mkutano Bibi Khalifa alisema, ataendelea kuenzi umuhimu wa Umoja wa Mataifa, ambapo Baraza kuu la Umoja wa Mataifa linatakiwa kufanyiwa mageuzi na kutoa mpango wa kukabiliana na changamoto wenye ufanisi katika utatuzi endelevu. Alisisitiza kuwa hivi leo nchi mbalimbali zinategemeana, hivyo mfumo wa ushirikiano wa pande mbalimbali uliothibitishwa na Umoja wa Mataifa ni msingi wa kuishi pamoja kwa amani kwa watu wote, pia ni mbinu zenye ufanisi zaidi za kuhakikisha usalama wa watu wote, kulinda haki za binadamu na utaratibu wa kisheria.

Pia alisema mapambano dhidi ya ugaidi duniani ni kazi kubwa yenye taabu duniani, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuchukua hatua za kukinga na kupambana na ugaidi.