Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-13 20:38:44    
Mapishi ya mbavu za nguruwe na vitunguu saumu

cri

Mahitaji:

Mbavu za nguruwe gramu 1000, vipande vya vitunguu saumu, vitunguu maji na tangawizi, wanga wa pilipili manga, mvinyo wa kupikia, chumvi, sukari, kipande cha mkate, korosho, unga wa pilipili hoho, ufuta mweupe, M.S.G, maziwa ya unga

Njia:

1 tia vipande vya vitunguu saumu kwenye maji halafu vikaushe na uipashe moto, tia vipande vya vitunguu saumu kwenye sufuria vikaage mpaka viwe na rangi ya hudhurungi halafu vipakue, kanga vipande vya mkate na uvipakue na kukaanga korosho halafu uzisage. Tia ufuta mweupe kwenye sufuria korogakoroga upakue. Koroga vipande vya vitunguu saumu, vipande vya mkate, korosho, ufuta mweupe, sukari, chumvi,M.S.G, wanga wa pilipili hoho mpaka viwe unga.

2. koroga mbavu za nguruwe pamoja na vipande vya vitunguu maji, tangawizi, vitunguu saumu, unga wa pilipili manga mvinyo wa kupikia chumvi na maziwa ya unga. Baada ya masaa mabili tia mbavu kwenye maji moto ili kuondoa damu kwenye mbavu na zipakue.

3. washa moto tena tia mafuta mpaka yawe na joto la nyuzi ya 50 tia mbavu za nguruwe, zikaange mpaka ziwe na rangi ya hudhurungi kisha zipakue. Weka unga uliotengenezwa katika hatua ya kwanza, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.