Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-15 14:50:20    
Ni maafa au demokrasia? Wataalamu wa China wazungumzia suala la vita vya Iraq na Marekani kuondoa jeshi lake kutoka Iraq

cri
Ni maafa au demokrasia? Wataalamu wa China wazungumzia suala la vita vya Iraq na Marekani kuondoa jeshi lake kutoka Iraq

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan tarehe 13 alisema, hivi karibuni alitembelea nchi za Mashariki ya Kati na amefahamu kwamba viongozi wengi wa nchi hizo wanaona vita vilivyoanzishwa na Marekani dhidi ya Iraq vimeziletea maafa makubwa nchi za Mashariki ya Kati. Lakini Marekani inasema nchi nyingi ikiwemo Iraq zimekuwa zikijaribu au zimeanzisha mfumo wa kidemokrasia. Lakini je, vita dhidi ya Iraq vimeziletea nini hasa nchi za Mashariki ya Kati? Na je ni bora kwa jeshi la Marekani kuondoka au kubaki nchini Iraq? Kuhusu suala hilo mwandishi wetu wa habari alizungumza na mtaalamu Yin Gang wa masuala ya Mashariki ya Kati na mtaalamu Liu Weidong wa masuala ya Marekani.

Bw. Liu Weidong amesema mtazamo wa viongozi wa nchi za Mashariki ya Kati na wa Marekani kuhusu vita vilivyoanzishwa na Marekani dhidi ya Iraq ni tofauti kabisa kwa sababu ya misimamo tofauti. Marekani inaona kuwa vita hivyo imeleta mpasuko Mashariki ya Kati na imepenyeza demokrasia na kusukuma uenezi wa demokrasia kwa kuifanyia Iraq mageuzi, lakini watu wa Mashariki ya Kati hawaoni hivyo.

"Viongozi wa nchi za Mashariki ya Kati wameshuhudia vurugu zilioleta maafa makubwa kwa taifa na kwa maisha ya raia, na ugaidi ukishamiri itakuwa ni vigumu kuudhibiti. Kwa hiyo wanapolinganisha hali ya kabla na baada ya vita vya Iraq wanaona kwamba hali ya vurugu ya sasa ni hasara kuliko faida. Ingawa rais George Bush wa Marekani alisema, Palestina na Iraq zimeanza kufanya uchaguzi wa kidemokrasia, lakini kuwepo kwa mpango tu wa demokrasia hakumaanishi utekelezaji halisi wa demokrasia."

Bw. Yin Gang anaona kuwa chanzo muhimu cha vurugu nchini Iraq ni kushindikana kwa ukarabati wa Iraq baada ya vita, kwa mfano, mfumo wa uchaguzi ulioanzishwa umesababisha kuchomoza kwa vyama vingi na migogoro kati ya vyama hivyo na kati ya madhehebu ya dini.

Tarehe 13 Bw. Kofi Annan alisema inafaa Marekani iondoe jeshi lake kutoka Iraq katika wakati unaofaa, na baada ya kuondoa jeshi lake ni lazima ihakikishe utulivu wa nchi hiyo bila kutokea kwa migogoro ya kimabavu wala misukosuko. Bw. Yin Gang anaona kuwa majeshi yanayoongozwa na Marekani yanapaswa kuondoka kutoka Iraq.

"Ninaposema 'wakati unaofaa' nina maana ya kwamba nguvu za usalama za Iraq na nguvu za ulinzi wa taifa zinaweza kubeba majukumu ya kulinda usalama wa ndani na nje. Katika sehemu ya kusini ya Iraq madhehebu ya dini ni machache na mkoa mmoja umekwisha kabidhiwa jukumu la kulinda usalama, kutokana na uimarishaji wa nguvu za kulinda usalama wa ndani na nje, si Marekani tu bali nchi zote zenye majeshi ni lazima ziondoe majeshi yao kutoka Iraq."

Kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei tarehe 13 alipokutana na waziri mkuu wa Iraq aliyekuwa ziarani nchini Iran alisema ikiwa majeshi ya nchi za nje yataondoka kutoka Iraq, basi matatizo mengi yanayoikabili Iraq yanaweza kutatuliwa. Lakini Bw. Yin Gang anaona kwamba kama jeshi la Marekani likiondoka mara moja na kisingizio cha kufanya ugaidi hakitakuwepo, hatari nyingine zitaweza kutokea.

"Kama jeshi la Marekani likiondoka mara moja pengine makundi yanayopinga mfumo wa sasa wa Iraq kama ya Sunni na wafuasi wa Al Zaqawi pengine watapenyeza pengo hilo na kuleta mabadiliko mapya ya hatari."

Bw. Kofi Annan alisema alipozuru Iran aliambiwa kwamba Iran inapenda kusaidia Marekani kuondoa jeshi lake kutoka Iraq. Wataalamu hao wawili wanaona hii ni nia ya Iran kutaka kuifanya Marekani igeuze macho kutoka suala la nyuklia la Iran. Alisema,

"Sababu ya Iran kufanya hivyo ni kutaka kutumia athari yake kwa madhehebu ya Shiya na kuiambia Marekani kwamba kama ikiondoa jeshi lake, Iran inaweza kuituliza Iraq kwa athari yake kwa madhehebu ya Shiya."

Hivi sasa hali ya Iraq ni mbaya sana, mashambulizi ya mauaji yanatokea mara kwa mara, kazi ya ukarababi inasota sana. Bw. Liu Weidong alisema,

"Kwanza utulivu ni wa lazima, lakini utulivu huo unapatikana kwa kupambana na watu wenye silaha. Pili, mazingira ya kuishi lazima yaboreshwe kwa juhudi kubwa na kukwepa migogoro kati ya madhehebu na makundi mbalimbali."

Idhaa ya kiswahili 2006-09-15