Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-15 15:56:52    
China yazisaidia nchi za Afrika kwa dhati

cri

Mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 50 tangu China na nchi za Afrika zianzishe uhusiano wa kibalozi. Katika nusu ya karne iliyopita, misaada iliyotolewa na China kwa nchi za Afrika imetoa mchango mkubwa katika kuhimiza maendeleo ya uchumi, kuboresha maisha ya wananchi, na kuinua kiwango cha elimu, matibabu na afya kwa nchi za Afrika. Naibu mtafiti wa taasisi ya utafiti wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa kimataifa ya wizara ya biashara ya China Bwana Xu Qiang muda mchache uliopita aliandika makala iliyochapishwa kwenye gazeti la "Renminribao" akijumuisha mambo halisi na umaalum wa misaada iliyotolewa na China kwa nchi za Afrika.

Tangu China mpya iasisiwe imetoa misaada mingi isiyokuwa na masharti yoyote kwa nchi za Afrika, imetoa mchango mkubwa katika kuimarisha urafiki, undugu na ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika, na kusifiwa sana na serikali za nchi za Afrika na watu wake.

Bw. Xu Qiang alisema mwishoni mwa mwaka 1963 na mwanzoni mwa mwaka 1964, waziri mkuu wa zamani wa China Marehemu Zhou Enlai alipofanya ziara katika nchi kumi za Afrika, alitoa kanuni nane za China za kutoa misaada ya kiuchumi na kiteknolojia kwa nje akisisitiza kuwa, serikali ya China itaheshimu kwa makini mamlaka ya nchi zilizopewa msaada, misaada iliyotolewa na serikali ya China haitakuwa na masharti yoyote. Kanuni hizo hadi leo bado ni mwongozo wa kuelekeza China kutoa misaada kwa nchi za Afrika.

Katika miaka ya 50 hadi 60 ya karne iliyopita, njia muhimu zilizotumiwa na China katika kutoa misaada kwa nchi za Afrika ni pamoja na ujenzi wa miradi, utoaji vifaa na kuwatuma wataalamu wa aina mbalimbali kufanya kazi katika nchi za Afrika. Mwaka 1978 China ilianza kutekeleza sera ya kufanya mageuzi na kufungua mlango, wakati huo huo nchi za Afrika pia zilianza kufanya marekebisho ya miundo ya kiuchumi. Kutokana na mabadiliko halisi yaliyotokea China na katika nchi za Afrika, njia za China za kutoa misaada kwa nchi za Afrika pia zimebadilika na zimekuwa na ufanisi zaidi, kama vile kutoa mikopo bila ya riba, kutoa misaada ya kiteknolojia, kuanzisha viwanda moja kwa moja, kutuma wataalamu, kutuma nguvukazi, kutoa mafunzo kwa wataalamu wa aina mbalimbali kwa nchi za Afrika. Pande mbili za China na nchi za Afrika zinafuatilia zaidi ufanisi wa misaada inayotolewa, na umuhimu wake katika kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara, ili kukamilisha na kuimarisha malengo ya misaada na utaratibu wa utoaji dhamana. Kutenganisha hatua kwa hatua utoaji misaada na utekelezaji wa miradi yenyewe, makampuni yenye uwezo na sifa bora yamechaguliwa kufanya ujenzi wa miradi. Jambo lililotiliwa maanani zaidi ni kwamba, tokea miaka ya 90 ya karne 20, China inaweka mkazo kuzisaidia nchi za Afrika kwa njia ya kuzipatia maelekezo ya usimamizi wa teknolojia, kutoa mikopo nafuu, kuwekeza kituo cha kuhimiza uwekezaji na biashara, kupunguza au kufuta kabisa madeni iliyokuwa inazidai nchi maskini, na kuandaa mafunzo kwa maofisa wa Afrika wanaoshughulikia mambo ya uchumi na biashara.

Ikilinganishwa na misaada inayotolewa na nchi nyingine, misaada iliyotolewa na China kwa nchi za Afrika ina umaalum wa kutokuwa na masharti yoyote, na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi za Afrika. Baadhi ya nchi za magharibi zinatoa misaada kwa nchi za Afrika kwa ajili ya kuenzi msimamo wao wa kisiasa, hasa kujaribu kuelekeza mambo ya ndani na ya kidiplomasia ya nchi zilizopewa misaada. Zaidi ya hayo, tofauti na nchi za magharibi ya kutoa misaada kwa njia ya kifedha, sehemu kubwa ya misaada iliyotolewa na serikali ya China kwa nchi za Afrika ni misaada isiyo ya kifedha, hasa miradi iliyojengwa na vifaa halisi. Ukweli wa mambo umethibitisha kuwa, misaada inayotolewa na China kwa kuzipa nchi za Afrika miradi iliyokamilika, vifaa na kutoa mafunzo kwa mafundi au wataalamu inaweza kutosheleza zaidi mahitaji makubwa ya nchi zilizopewa misaada na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara wa pande mbili mbili. Tokea mwaka 2003, wakuu wa nchi nyingi za Afrika zikiwemo Madagascar, Eritrea na Rwanda waliwahi kusifu mara kwa mara misaada inayotolewa na China, na kutoa malalamiko kwa baadhi ya nchi za magharibi zinazohusisha misaada na masharti ya kisiasa.

Hivi sasa miradi mingi iliyojengwa kwa msaada wa China kama vile reli ya TAZARA na bandari ya urafiki ya Mauritius imekuwa vituo muhimu vya kiuchumi kwa nchi hizo. Misaada inayotolewa na serikali ya China kwa nchi za Afrika si kama tu imezidisha uhusiano wa pande mbili mbili wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za Afrika, bali pia imehimiza uaminifu wa kisiasa kati ya pande hizo mbili, kuhimiza China na nchi za Afrika kusawazisha msimamo wao wa kisiasa na shughuli za kidiplomasia. China iliushinda mara 11 muswada uliotolewa na nchi za magharibi dhidi ya China kwenye mkutano wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa ulikataa mara 13 ajenda ya Taiwan kujiunga tena katika Umoja wa Mataifa na kufanikiwa kupata haki ya kuandaa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 na maonesho ya duniani ya mwaka 2010, juhudi hizo zote zimepata uungaji mkono kutoka kwa nchi za Afrika.

Idhaa ya kiswahili 2006-09-15