Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-18 15:14:03    
Haiyang mkoani Shandong, China

cri

Baada ya kupita siku za joto, upepo mwanana wa majira ya mpukutiko unawafurahisha watu zaidi, katika majira hayo shughuli za kuwafuata wavuvi kwenda baharini kuvua samaki na kujionea maisha ya wavuvi zimekuwa shughuli za utalii zinazopendwa na watu wengi.

Kwenye ramani ya mkoa wa Shandong wa China, mji wa Haiyang uko karibu na miji maarufu mkoani humo Qingdao, Yantai na Weihai. Mji wa Haiyang chini ya utawala wa Mji wa Yantai, na Mji wa Yantai uko upande wake wa kaskazini, upande wake wa mashariki ni Mji wa Weihai, na upande wake wa magharibi ni Mji wa Qingdao, miji hiyo mitatu yote ni miji yenye vivutio vya utalii, kupanda gari kufunga safari kutoka Mji wa Haiyang kuelekea kwenye kila mmoja kati ya miji hiyo mitatu ya utalii kunahitaji zaidi ya saa moja tu. Ndiyo maana watalii wengi wanapenda kutembelea miji hiyo minne kwa wakati mmoja kwenye safari yao.

Lakini Mji wa Haiyang ulikuwa nyuma ya miji mitatu ya Qingdao, Yantai na Huihai, kwani pwani ya mji huo yenye ufukwe wa mita elfu 10 hivi inayowafanya wakazi wa huko waone majivuno zaidi ilijulikana nchini kuanzia katikati ya miaka ya 80 ya karne iliyopita; hata majumba madogo madogo yalijengwa moja baada ya lingine baada ya miaka ya 90. Ndiyo maana mandhari nzuri na hali ya utulivu ya Mji wa Haiyang huwafanya watalii wanaokwenda kuwa na mshangao na furaha.

Watalii wakifika huko wanaweza kulala nyumbani kwa wavuvi, kupanda mashua kwenda baharini kuvua samaki, baadaye kula chakula cha samaki wa aina mbalimbali, shughuli hizo za utalii wenye umaalum zimeanzishwa na serikali ya Haiyang kutokana na hali halisi ya sehemu hiyo, shughuli hizo zinapendwa sana na watalii wengi.

Wavuvi wanaoishi kandoni mwa bahari wamezoea kuona maji ya baharini yakipwa na kujaa, lakini watalii wanaotembelea sehemu ya pwani wanaweza kushangazwa na hali hiyo, hata wana hamu kubwa ya kuongea na wavuvi waliorudi punde kutoka baharini.

Samaki huyo anaitwaje?

Hawa ni samaki wa mullet

Samaki hao wadogo ni samaki gani?

Sisi wakazi wa hapa tunawaita Samaki wa Pomidou. n. croakers

Je samaki hao ni chakula kizuri?

Ndio.

Samaki wapi ni chakula kizuri zaidi?

Samaki aina ya weever.

Kwenye pwani mvuvi aitwaye Li Desheng aliyewaongoza watalii kwenda bahari kuvua samaki alikuwa amerudi punde, ambapo samaki hai kwenye kapu lake waliwavutia watalii waliotaka kuonja chakula cha samaki waliovuliwa muda mfupi uliopita. Samaki kadhaa walinunuliwa mara moja na watalii baada ya kugombea bei. Mvuvi huyo alisema wavu wake wa kuvulia samaki ulifungwa kwenye eneo la bahari lisilo la kina kirefu, asubuhi aliwaongoza watalii kupanda mashua kwenda kwenye eneo hilo kufungua wavu huo, aliona samaki aliowavua ni wengi na wa aina mbalimbali, baadhi yao ni wenye nyama nono, laini na ladha nzuri.

Kuwafuata wavuvi kupanda mashua kwenda baharini kwa pamoja ili kuvua samaki baharini, ama kukaa ndani ya mashua kuvua samaki, ili kujionea maajabu ya bahari na majivuno ya kuweza kuvua samaki baharini, ni shughuli zinazowavutia watalii wengi. Na shughuli nyingine ni kwenda pwani baada ya maji kutoweka, ili kuokota samaki wadogo au kamba wadogo pamoja na magamba ya samaki. Watalii wengi wanapenda kushiriki kwenye shughuli kama hizo, baada ya maji kutoweka, mawe yanaonekana kwenye pwani, watalii wanaanza shughuli zao za kuokotaokota samaki wadogo na vitu vya aina ya kombe.

Msichana Zhang Fan alitafutatafuta kwa makini ndani ya mwanya wa mawe, alimwambia mwandishi wetu wa habari akisema:

Nimechimba mchanga nimepata vitu mbalimbali vya aina ya kombe, ambavyo ni vitu vidogo vinavyopendeza, nafurahia shughuli hizo kwenye pwani ya bahari.

Msichana Zhang Fan pia alisema amevutiwa sana na shughuli za kuokota vitu au samaki na kamba wadogo kwenye pwani, akipekuapekua chini ya mawe anaweza kugundua magamba ya samaki ya aina mbalimbali, hata kaa, na anaweza kufurahi sana. Alisema:

Kwa kawaida wakati wa wikiendi mimi na marafiki zangu hufika pwani kuokotaokota vitu vidogovidogo vya aina ya kombe, ama kuangalia bahari, kusikiliza sauti ya mawimbi kwenye bahari, tunaona furaha na starehe kweli. Katika pwani za Mji wa Haiyang, mchanga ni laini sana, watu wengi wanapenda sehemu hiyo na kuja kujistarehesha.

Kama alivyosema msichana Zhang Fan, watalii wengi wanapenda kutembea peku kwenye pwani za Mji wa Haiyang, wanaona kuwa wakitembea huku wanaweza kuangalia mandhari nzuri ya baharini, na kujionea mawimbi yanavyopigapiga pwani.

Mtalii kutoka Anhui Bwana Wu Sheng alifika Haiyang mara ya kwanza lakini aliona amecheza vizuri sana. Alisema:

"Tulikuja Haiyang kutoka mkoa wa Anhui, tunaona sehemu hiyo ya pwani inatuvutia kweli, kwani mandhari ya sehemu hiyo ni nzuri sana, tena wakazi wa hapa ni wachangamfu".

Idhaa ya kiswahili 2006-09-18