Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-19 15:44:41    
China siyo chanzo cha kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli duniani

cri

Bei ya mafuta ya petroli imepanda na kufikia kiasi cha dola 70 za kimarekani kwa pipa hivi sasa kutoka wastani wa dola za kimarekani 29 mnamo mwaka 2003. Baadhi ya watu walisema, ongezeko la mahitaji ya nishati nchini China ni chanzo cha kupanda kwa kiwango kikubwa kwa bei ya mafuta ghafi ya petroli.

Kwenye mkutano wa 7 wa baraza la kazi za viwanda vya mafuta ghafi ya petroli na gesi ya asili uliofanyika toka tarehe 10 hadi tarehe 12 mwezi Julai mjini Hangzhou, maofisa wa idara husika ya serikali na kampuni ya mafuta ghafi ya petroli ya China walisema, mafuta ghafi ya petroli yamekuwa moja ya bidhaa zinazotumika katika shughuli za kujipatia faida kubwa, China siyo chanzo cha kupanda kwa bei ya mafuta ghafi ya petroli duniani.

Ikiwa nchi ya pili inayotumia nishati kwa wingi duniani na nchi ya tatu inayoagiza mafuta ghafi kwa wingi duniani, uchumi wa China umeongezeka kwa kasi ya zaidi ya 10% kwa mwaka katika miaka 3 iliyopita, mahitaji ya nishati ya China bila shaka yanaongezeka kwa kiwango fulani, na China inahitaji kuagiza mafuta ghafi ya petroli kutoka nchi za nje, lakini mafuta ghafi ya petroli yanayoagizwa na China kutoka nchi za nje ni kiasi cha 6% tu cha soko la mafuta ghafi duniani, na ni kiasi kidogo sana ikilinganishwa na kiasi cha mafuta ghafi ya petroli yanayoagizwa na Marekani na Japan, hivyo athari ya mahitaji ya China kwa bei ya mafuta ya petroli duniani ni ndogo.

Naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa Bw. Zhang Guobao alithibitisha hoja hiyo kwa takwimu. Matumizi ya mafuta ghafi nchini China yalikuwa tani milioni 317 katika mwaka 2005, kiasi kilipungua kuliko mwaka uliotangulia. Kati yake mafuta ghafi yaliyoagizwa na China kutoka nchi za nje yalikuwa tani 136, kiasi hicho ni kupungua kidogo kuliko mwaka uliotangulia. Ikiwa China ni chanzo cha kupanda kwa bei ya petroli, basi kupungua kwa mafuta ghafi yaliyoagizwa na China kungefanya bei ya petroli duniani kushuka, lakini ukweli ni kuwa bei ya mafuta ya petroli duniani iliendelea kupanda.

Wastani wa rasilimali ya mafuta ya ghafi na gesi ya asili wa kila mchina ni kiasi cha 7% ya wastani wa kila mtu duniani, hivyo 40% ya mafuta ya ghafi yanayohitajiwa na China yanatakiwa kuagizwa kutoka nchi za nje, lakini China ni nchi inayotumia makaa ya mawe kwa wingi.

Takwimu za kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa zinaonesha kuwa, utoaji wa makaa ya mawe katika mwaka 2005 ulifikia tani bilioni 2.22 zikiwa ni 68.7% ya nishati inayotumika mara ya kwanza nchini China, wakati matumizi ya nishati ya mafuta ya petroli na gesi ya asili yalichukua 24% tu. Rasilimali ya makaa ya mawe inafanya China kuchukua nafasi ya pili kwa wingi wa uzalishaji wa rasilimali ya nishati, na kuchukua nafasi ya kwanza katika usafirishaji wa makaa ya mawe kwa nchi za nje. Sera za China kuhusu maendeleo ya nishati katika siku za baadaye zitaendelea kuwa ni "makaa ya mawe ni msingi, huku matumizi ya nishati za aina nyingi yakiendelezwa".

Bw. Zhang Guobao alisema ili kukabiliana na bei kubwa ya mafuta ghafi duniani, China inatumia vilivyo dhamana ya makaa ya mawe kwa mahitaji ya nishati nchini mwake, kuendeleza matumizi ya nishati mpya na nishati endelevu, kuvumbua nishati mbadala ya petroli, kuboresha muundo wa uzalishaji na matumizi ya nishati, kupunguza kiwango cha kutegemea mafuta ghafi yanayoagizwa kutoka nchi za nje.

Kuingia kwa wingi kwa fedha za biashara ya magendo kwenye soko la mafuta ghafi yatakayozalishwa kumekuwa chanzo muhimu cha kupanda kwa bei ya mafuta duniani. Mtaalamu husika alikadiria kuwa zaidi ya dola za kimarekani trilioni 1 za biashara ya magendo ya mafuta zimeingia kwenye biashara ya mafuta, hatua ambayo inafanya bei ya mafuta ya petroli duniani kuachana na kanuni za thamani.

Kupanda kwa mfululizo kwa bei ya mafuta ya petroli duniani kunakwamisha maendeleo ya uchumi wa dunia. Katika mkutano wa kongamano hilo, maofisa wa China wamesema China inapenda kuimarisha ushirikiano na Marekani na kutoa mchango kwa utulivu wa soko la mafuta duniani.

Idhaa ya kiswahili 2006-09-19