Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-20 13:47:37    
Vyuo vikuu vya Beijing vyachukua hatua za kuwahudumia vizuri wanafunzi wapya na wazazi wao

cri
Katika siku za karibuni wanafunzi wapya waliandikisha katika vyuo vikuu hapa Beijing, na vyuo vikuu mbalimbali vimechukua hatua kadha wa kadha za kuwahudumia vizuri zaidi wanafunzi na wazazi wao.

Tarehe 9 Septemba ilikuwa siku ya kujiandikisha kwa wanafunzi wapya wa Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing. Siku hiyo katika vituo vya uandikishaji vya idara mbalimbali vya chuo hicho, kila mwanafunzi mpya alipewa faili moja iliyowekwa dira ya wanafunzi wapya kwenye chuo kikuu, na mwaka huu kila mwanafunzi mpya pia a;opewa kitabu cha mwongozo kuhusu "Wazazi kukua pamoja na watoto---ujuzi wa lazima kwa wazazi", ambapo kinaeleza hali halisi ya wanafunzi katika chuo hicho na vyuo vingine vya nchini na nchi za nje, kuwaelezea wazazi maisha ya wanafunzi katika vyuo vikuu katika nyanja mbalimbali zikiwemo maadili, usalama, maisha, masomo, saikolojia, mapenzi, uwezo na matumizi ya mtandao wa Internet, pia kinaeleza matatizo yatakayowakabili wanafunzi katika vyuo vikuu, na kutoa maoni na mapendekezo kwa wazazi wa wanafunzi.

Ofisa wa idara inayoshughulikia mambo ya wanafunzi kwenye Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing Bw. Qi Jiayong alisema chuo hicho kitatuma kitabu hicho kwa wanafunzi kwa njia ya posta pamoja na uarifu wa kukubaliwa kusoma katika Chuo Kikuu hicho, ili kuwasaidia wazazi wapate ufahamu kuhusu chuo kikuu kabla ya wanafunzi kuanza masomo.

Aidha Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing kiliandaa mafunzo ya saikolojia yaitwayo "Tunakua pamoja na watoto wetu" kwa wazazi tarehe 9 mwezi Septemba, ambapo naibu mkurugenzi wa kituo cha ushauri wa saikolojia cha chuo hicho Bw. Nie Zhenwei alieleza matatizo ya kawaida ya saikolojia yanayowakumba wanafunzi wa chuo kikuu, na kujadiliana na wazazi wa wanafunzi kuhusu namna ya kuwasiliana na watoto, na kupunguza shinikizo la saikolojia kwa watoto wao.

Katika Chuo kikuu cha Beijing, wanafunzi watatu wapya na wazazi wa wanafunzi watano waliotoka mbali walikaribishwa kwa vyakula vitamu alfajiri ya siku ya kwanza ya uandikishaji. Aidha wazazi wa wanafunzi kumi kadhaa ambao hawakupata sehemu ya kulala karibu na chuo kikuu walipangiwa kulala kwenye bweni la chuo kikuu lililoandaliwa mapema. Usiku huo wazazi hao waliandaliwa vinywaji, matunda na keki kwa saa 24 bila ya kulipa kwenye Bwalo la Chuo.

Aidha katika siku ya uandikishaji, Idara ya utoaji huduma ya ajira ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Beijing iliweka kituo cha ushauri wa ajira kwa wanafunzi wapya, ili kutoa mwongozo wa ajira kwao, na hii ilikuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Chuo kikuu cha Beijing kuwapokea wanafunzi wapya. Walimu wa idara hiyo walijibu maswali ya wanafunzi wapya kuhusu ajira katika siku za mbele, kufanya tathmini na kutoa mwongozo kwa wanafunzi wenye mahitaji.

Katika Chuo kikuu cha mawasiliano cha Beijing, ili kuwakaribisha wanafunzi wapya waliofika chuoni, chuo hicho kilikuwa kimeunda vikundi 11 vyenye watu 2000 vya kuwahudumia. Aidha chuo hicho kiliweka posho ya kujikimu maisha ya mwezi wa kwanza kwenye kadi ya wanafunzi wapya, ili kuwawezesha kula na kuogelea kwa kutumia kadi hiyo kwa urahisi. Aidha chuo hicho kilifungua mabwalo mawili na kuandaa vitanda 500 hadi 600 kwa ajili ya mapumziko ya wazazi wa wanafunzi wapya.

Idhaa ya Kiswahili 2006-09-20