Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-20 16:16:45    
Mapishi ya slesi ya aina tatu

cri

Mahitaji

Viazi mviringo vitatu, pilipili mboga mbili, vipande vine vya uyoga, kiasi kidogo cha tangawizi, mvinyo wa kupikia, siki, M.S.G na Chumvi.

Njia

1. Menya viazi mviringo, halafu vikate viwe slesi. Ondoa vitu vilivyo ndani ya pilipili mboga, na uikate iwe selsi. Kata uyoga na tangawizi ziwe slesi.

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi 50, tia slesi ya viazi mviringo na tangawizi, korogakoroga kwa dakika 3, mimina siki ili kulainisha slesi ya viazi mviringo, korogakoroga, tia vipande vya pilipili mboga na uyoga, korogakoroga kwa dakika 5, tia chumvi na M.S.G korogakoroga. Ipakue, mpaka hapo kitoweo hicho kiko tayari kuliwa.