Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-22 19:07:52    
Jumuiya ya kimataifa yatakiwa kuongeza ufanisi wa misaada yake Barani Afrika

cri

Mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa tarehe 21 huko Geneva ulitoa taarifa kuhusu maendeleo ya uchumi wa Bara la Afrika mwaka 2006, ikidhihirisha kuwa uchumi wa Bara la Afrika umeongezeka katika miaka mfululizo ya hivi karibuni. Ili kudumisha mwelekeo huo mzuri, jumuiya ya kimataifa inapoongeza msaada wake wa Bara la Afrika, inatakiwa kutilia maanani sifa ya msaada huo na kuongeza ufanisi wa msaada huo.

Taarifa hiyo ilisema tokea mwanzoni mwa karne hii, uchumi wa Bara la Afrika umeongezeka kwa haraka kwa miaka mfululizo, ambapo ongezeko kubwa la mahitaji kwenye masoko mapya ya China na India limeleta fursa mpya ya biashara na uwekezaji kwa Bara la Afrika. Baada ya kujumlisha uzoefu na mafunzo ya miaka mingi iliyopita, nchi nyingi zinafanya mageuzi ya uchumi, na jumuiya ya kimataifa imeahidi kuongeza msaada wa kiuchumi kwa Bara la Afrika na kusamehe madeni yao kwa kiasi kikubwa, ahadi hii pia imeleta matumaini mapya kwa maendeleo ya uchumi barani Afrika.

Lakini taarifa hiyo imedhihirisha kuwa, Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto kubwa sana. Katika mchakato wa kutimiza lengo la maendeleo ya milenia la Umoja wa Mataifa, Bara la Afrika limekuwa nyuma kuliko mabara mengine. Ili kukamilisha lengo hilo kwa wakati, nchi za Afrika zinapaswa kudumisha wastani wa ongezeko la uchumi kwa zaidi ya asilimia 8 katika miaka 10 ijayo, lakini shirika husika la Umoja wa Mataifa lilikadiria kuwa ongezeko la uchumi wa Bara la Afrika litakuwa asilimia 5.5 mwaka huu. Ingawa kupanda kwa bei za raslimali za nishati na madini kumeleta mapato makubwa kwa nchi kadhaa za Afrika, lakini mpaka sasa hali hii bado haijaonesha umuhimu mkubwa kwa kuhimiza nchi hizo kupunguza umaskini na kuondokana na umaskini, kupunguza pengo kati ya utajiri na umaskini na kuongeza nafasi za ajira.

Taarifa hiyo imeelezea zaidi namna jumuiya ya kimataifa inavyotoa misaada kwa Bara la Afrika. Taarifa hiyo inaona kuwa hivi sasa mfumo wa utaoji misaada wa kimataifa una mwelekeo wa kisiasa, gharama za makubaliano ni kubwa, unatilia maanani ufanisi wa muda mrefu tu, na unakosa uratibu na uwazi, ufanisi wa msaada hauwezi kukadiriwa, tena unatoa matakwa ya juu kupita kiasi kwa nchi zenye udhaifu zilizopewa misaada. Ili kupewa misaada, nchi zote zilizoomba misaada zililazimika kuchukua hatua sawasawa za marekebisho, pamoja na kutuliza bei, utandawazi wa uhuru wa kupita kiasi na utandawazi wa ubinafsishaji, hatimaye hatua hizo zilizifanya nchi nyingi zilizopewa misaada zikae hali ya kulazimishwa kuchukua tena hatua za kupunguza ongezeko la uchumi. Kwa upande mwingine nchi zilizotoa misaada hazikuweza kufanya majadiliano mazuri au uratibu na nchi zilizopewa misaada, hazikuzingatia hali halisi ya nchi zilizopewa misaada, bali zilifuata upendeleo wao kubuni malengo ya uchumi na kuchagua miradi iliyopewa kipaumbele badala ya nchi zilizopewa misaada. Tena nchi zilizopewa misaada ni nyingi, lakini mitizamo yao, maombi yao hata utaratibu wa uhasibu wa nchi mbalimbali ni tofauti, ndiyo maana hali ya vurugu ilionekana wazi katika mfumo wa utoaji wa misaada, hata wakati fulani nchi mbalimbali zilizotoa misaada zilifanya ushindani, zikazifanya serikali za nchi husika za Afrika zikae katika hali ya kuhangaika, na kuchoshwa na kukabiliana na kanuni na masharti mbalimbali ya kupewa misaada, hayo yote yalitumiwa kudhoofisha uwezo wa utawala wa nchi za Afrika.

Taarifa imependekeza kutunga mpango mpya wa utoaji wa misaada wa kimataifa, kupendekeza pande mbalimbali zishirikiane kutoa misaada, ambapo kuuachia mfuko mmoja wa fedha wa Umoja wa Mataifa usioathiriwa na shinikizo la kisiasa utoe misaada. Na mikopo inayotolewa na Benki ya dunia na Shirika la IMF pia inaweza kuukabidhi mfuko huo wa fedha wa Umoja wa Mataifa utoe misaada. Taarifa hiyo imesema jumuiya ya kimataifa inahitaji kuanzisha Baraza jipya ndani ya Umoja wa Mataifa ili pande zizonazopewa misaada ziweze kutoa maoni yao kuhusu masuala zinayofuatilia zaidi. Mpango huo mpya wa utoaji misaada utaweza kusaidia kupunguza ushindani kati ya pande zitoazo misaada, ili kupunguza gharama kubwa ya usimamizi wa utawala na kuzuia misaada ya kisiasa iliyoleta uharibifu mkubwa isitolewe tena.

Idhaa ya Kiswahili 2006-09-22