Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-25 19:24:47    
Uundaji wa serikali mpya ya Palestina utakabiliwa na changamoto nyingi

cri

Mwakilishi mkuu wa Palestina katika mazungumzo Bwana Saeb Erekat tarehe 24 alithibitisha kuwa, mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina ambaye pia ni kiongozi wa kundi la chama cha ukombozi wa Palestina Fatah atakwenda Gaza tarehe 25 au tarehe 26 kufanya majadiliano na waziri mkuu wa serikali ya utawala wa Palestina ambaye pia ni kiongozi wa chama cha upinzani cha kiislamu cha Hamas Bwana Ismail Haniyeh.

Makundi makubwa mawili ya Palestina Fatah na Hamas yalitangaza mwanzoni mwa mwezi huu kuwa, pande hizo mbili zitaunda serikali ya muungano badala ya serikali ya Hamas, ili kufanya juhudi za kuiwezesha jumuiya ya kimataifa irudishe misaada ya kiuchumi kwake, na kukomesha mgogoro wa kijamii na kifedha wa hivi sasa. Lakini nusu mwezi umepita, pande hizo mbili zimekuwa na migongano mingi katika mazungumzo ya kuunda baraza la mawaziri, na mpaka sasa hazijapata maendeleo yoyote.

Kwanza mgongano wa kimsingi kati ya Kundi la Hamas na Kundi la Fatah ni kuhusu kuitambua Israel au la, tarehe 11, baada ya makundi hayo mawili kukubali kuunda serikali ya muungano, Kundi la Hamas lilitoa maoni yake tofauti mara moja, lilisema halitaitambua Israel na wala kukubali makubaliano yaliyosainiwa kati ya Palestina na Israel katika siku zilizopita. Kutokana na mgongano huo, kabla ya kufunga safari ya kwenda New York kuhudhuria mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bwana Abbas alikuwa hana la kufanya ila tu kufunga mazungumzo kuhusu kuundwa kwa baraza la mawaziri. Na alipotoa hotuba kwenye mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bwana Abbas alisema, serikali mpya ya muungano itakidhi matakwa matatu ya jumuiya ya kimataifa yaani kuitambua Israel, kuacha nguvu za mabavu na kutambua mapatano yaliyosainiwa kati ya Palestina na Israel katika siku zilizopita. Kuhusu jambo hilo Kundi la Hamas lilisema, kama litatakiwa liitambue Israel, basi serikali mpya haitaweza kuundwa. Na waziri mkuu Haniyeh pia alisema hawezi kuiongoza serikali moja inayoitambua Israel. Wachambuzi wamedhihirisha kuwa Kundi la Hamas haliwezi kuitambua Israel mara moja, kwani kuitambua Israel kutakuwa na maana kuwa Kundi la Hamas limeacha kanuni yake, hii itadhuru hadhi yake miongoni mwa wananchi wa Palestina. Uchunguzi uliofanyika hivi karibuni umeonesha kuwa, nusu zaidi ya wapalestina hawataki kundi la Hamas liitambue Israel.

Aidha ni vigumu kwa Bwana Abbas kuunda serikali bila kujadiliana na Kundi la Hamas. Akiwa mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina, Bwana Abbas ana madaraka ya kuvunja serikali ya Hamas ya hivi sasa na kuteua serikali mpya. Lakini serikali mpya inapaswa kukubaliwa na Kamati ya utungaji wa sheria ya Palestina, wakati Kundi la Hamas limedhibiti theluthi mbili ya viti kwenye kamati hiyo, hivyo kweli ni vigumu kuundwa kwa serikali mpya. Na Bwana Abbas pia anaweza kutangaza kufanyika kwa uchaguzi mpya, lakini kufanya hivyo kunahitaji fedha nyingi, kufanya hivyo kutasababisha upinzani, kwani Palestina hivi sasa iko katika matatizo makubwa ya kifedha; na hata kama uchaguzi mpya utafanyika bado itakuwa ni nguvu kuhakikisha kuwa Kundi la Fatah linapata ushindi.

Zaidi ya hayo, serikali mpya ya muungano inapaswa kupata uungaji mkono wa makundi mengine. Mbali na makundi ya Hamas na Fatah, pia kuna makundi zaidi ya 10 ya kijeshi, kama makundi hayo yana malalamiko mengi juu ya serikali mpya, hali hiyo pia inaweza kusababisha mgogoro wa kimabavu ndani ya Palestina.

Na mwisho serikali mpya inapaswa kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa. Pande nne zinazohusiana na suala la mashariki ya kati zikiwemo Umoja wa Mataifa, Marekani, Russia na Umoja wa Ulaya zilitoa taarifa wiki iliyopita, ikiunga mkono Palestina kuunda serikali ya muungano na pia zimetangaza kurefusha muda wa kutekeleza utaratibu wa kuisaidia Palestina kwa miezi mitatu. Lakini msimano wa nchi za magharibi kuhusu suala la kuundwa kwa serikali mpya ya Palestina pia ni tofauti.

Wachambuzi wamedhihirisha kuwa jambo muhimu ni kwamba pande mbili za Palestina zitaweza kujadili na kupata mpango mmoja unaoweza kukidhi mahitaji ya jumuiya ya kimataifa pia kutokwenda kinyume na mwongozo wa kisiasa wa Palestina,.