Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-26 10:35:34    
Maonesho ya bidhaa za elektroniki yavutia watu wengi

cri

Maonesho ya bidhaa za elektroniki ya kimataifa ya mwaka 2006 yalifanyika katika mji wa Qingdao iliyoko sehemu ya pwani ya mashariki nchini China. Kampuni za elektroniki zaidi ya 400 za duniani zimefika huko kuonesha bidhaa mpya na teknolojia yao ya kisasa zikitaka kupata ushirikiano mpya.

Watu wanaweza kudhibiti vyombo vya kuchemsha maji, viyoyozi na mashine za kufulia nguo kutoka mbali kwa kutumia simu ya mkononi na kompyuta, vyombo vya umeme vya nyumbani pindi vinapotokewa matatizo vinaweza kuthibitisha chanzo chake na watu wanaweza kuangalia michezo ya televisheni kwenye tovuti. Hizi ni bidhaa mpya za seti ya vyombo vya umeme vya Internet vya nyumbani zinazojulikana kwa U-HOME zinazotolewa na kampuni ya Haier, ambayo inachukua nafasi ya kwanza katika uzalishaji wa vyombo vya umeme vya nyumbani nchini China. Naibu mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Haier Bw. Zhou Yunjie alisema, bidhaa hizo za U-HOME zinaleta mawasiliano mepesi kati ya watu na vyombo vya umeme vya nyumbani, na kati ya vyombo vya umeme vya nyumbani na Internet. Alipoeleza wazo kuhusu bidhaa za U-HOME, alisema,

"Watu wamekuwa na wazo la kuwa na seti ya vyombo vya umeme vinavyoleta raha na mawasiliano na dunia nyumbani kwao, kwa ufupi wazo letu kuhusu U-HOME ni kuwa hata ukiwa sehemu ya nje, lakini unasikia kama nyumba yako iko karibu, na baada ya kurejea nyumbani unajihisi unaungana na dunia kwa vyombo vya umeme vya nyumbani."

Kampuni ya Legend ikiwa kampuni inayoongoza sekta ya teknolojia ya mawasiliano, safari hiyo ilionesha bidhaa za kisasa zinazoendana na enzi ya sasa ya mawasiliano. Naibu mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Legend Bw. Du Jianhua alimwambia mwandishi wetu wa habari kwenye maonesho hayo, bidhaa mpya za kampuni ya Legend zinaweza kuonesha picha na rekodi ya video zilizohifadhiwa katika kompyuta katika televisheni, hatua hiyo inaongeza matumizi ya kompyuta na televisheni. Mtu akiwa sehemu ya nje anaweza kupata habari kutoka kwenye server ya kompyuta ya nyumbani. Uwezo wa bidhaa hizo unaweza kupanua eneo la maisha watu bila kikomo.

2Kampuni nyingi zilizoshiriki kwenye maonesho hayo zilileta bidhaa na teknolojia ya kisasa zikiwa ni pamoja na teknolojia ya kutoa kwa haraka picha zilizopigwa na simu za mkononi, walkman nyepesi yenye uzito wa gramu 50, kalamu ya scan ya kusomea. Kampuni ya kazi za viwanda ya Florida ya Marekani ilionesha aina mpya ya LED zinazotumika katika display. Naibu meneja mkuu wa kituo cha utafiti cha kampuni hiyo kilichoko nchini China Bw. Li Mengxian alisema,

"LED za display na mashine ndogo ya kutengeneza barafu ni bidhaa zetu mpya, kampuni yetu ni ya kwanza kutengeneza mashine hiyo ya kutengeneza barafu nchini mwetu, hususan bidhaa za display za LED ambazo tulizizalisha mwaka huu, bidhaa zote zinazooneshwa hapa ni bidhaa zetu mpya kabisa."

Maonesho ya bidhaa za elektroniki ya kimataifa nchini China ni maonesho ya kazi maalumu za elektroniki, ambayo yaliandaliwa na wizara za biashara, uzalishaji mali wa teknolojia ya mawasiliano na teknolojia ya kisayansi za China. Sifa za maonesho hayo ambayo yalianzishwa mwaka 2001, zinaongezeka mwaka hadi mwaka, hususan yameimarisha hadhi yake katika sekta za uzalishaji bidhaa za elektroniki za China na Asia nzima baada ya kuwa na ushirikiano na maonesho ya bidhaa za elektroniki ya Marekani, ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa duniani, na yanahimiza maendeleo ya sekta ya uzalishaji bidhaa za elektroniki duniani.

Maonesho ya bidhaa za elektroniki ya mwaka huu si kama tu yalivutia watazamaji wengi, tena ununuzi bidhaa wa wafanyabiashara wakubwa duniani kwenye maonesho hayo umevutia sana kampuni za uzalishaji bidhaa za elektroniki. Bw. Zhang Cida kutoka kampuni ya BENQ mwaka huu ni mara yake ya pili kuongoza kundi la watu la kampuni yao kushiriki kwenye maonesho hayo. Anaona ununuzi wa wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali duniani unamaanisha nafasi nyingi za ushirikiano na biashara kwa kampuni zinazoshiriki kwenye maonesho, kwa upande mwingine kushiriki kwenye maonesho kwa kampuni kunaweza kuongeza sifa za kampuni.

"Watu walioshiriki kwenye maonesho ya mwaka huu ni wengi kuliko maonesho yaliyopita, tena maonesho ya mwaka huu ni makubwa zaidi. Hali halisi ni kuwa bidhaa zilizooneshwa zilikuwa baadhi ya bidhaa zetu, lengo letu ni kuonesha uzuri wa bidhaa zetu. Kwa sisi wafanyabiashara, maonesho ni nafasi ya kuonesha bidhaa zetu bora."

Maonesho ya mwaka huu ni makubwa kuliko ya mwaka jana, licha ya hayo kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu imebadilika, waandaaji wa maonesho waliamua kufanya maonesho ya bidhaa za elektroniki ya mwaka huu kuwa "dunia inabadilika kufuatana na U", herufi ya "U" ina maana ya kuungana, kuenea na wa kipekee, inaeleza maendeleo ya teknolojia ya kisayansi na kuenea kwa mtandao kutafanya mawasiliano ya habari yawe katika kila sehemu na kila mahali. Naibu waziri wa uzalishaji mali wa teknolojia ya mawasiliano ya habari Bw. Lou Qinjian alisema, kauli mbiu hiyo inaonesha mkondo wa maendeleo ya vyombo vya umeme vya nyumbani. Alifafanua suala hilo kwa kutoa mfano wa simu za mkononi. Alisema, "Kwa mfano, hapo awali simu za mkononi zilichukuliwa kuwa ni bidhaa za mawasiliano ya habari, lakini hivi sasa tukisema bidhaa hizo ni za kompyuta, lakini zina uwezo wa kuongea na watu, tukisema hizo ni televisheni, lakini licha ya kuweza kutumika kuongea na watu, zinaweza kutumika kuungana na Internet. Kuunganisha bidhaa za elektroniki zitumiwazo kwa mawasiliano ya aina mbalimbali kumekuwa mkondo wa maendeleo ya vyombo vya umeme vya nyumbani vya teknolojia ya mawasiliano."

Ni kweli kwamba wakati teknolojia hizo mpya zinapoingia katika maisha yetu, kama vile televisheni za nyumbani zinazoweza kuungana na Internet na majokofu zinaweza kutumika kupeleka ujumbe, ndiyo kuwadia kwa enzi tunayotarajia ya ushirikiano mkubwa wa bidhaa za elektroniki, mawasiliano ya habari na vyombo vya umeme vya nyumbani. Wawe wafanyabiashara wa uzalishaji bidhaa au wateja, mahitaji ya uwezo mkubwa wa vyombo vya umeme yamekuwa ni matarajio ya pamoja. Maonesho ya bidhaa za elektroniki ya kimataifa yanayofanyika nchini China kila mwaka yanaweza kuunganisha pamoja kampuni za uzalishaji bidhaa na wateja na kuhimiza maendeleo ya sekta ya uzalishaji bidhaa za elektroniki. Hivyo kuandaa maonesho yenye umaalumu na ya kiwango cha juu, kumekuwa changamoto kubwa kwa waandaaji wa maonesho. Naibu meya wa mji wa Qingdao ambao ni mji ulioandaa maonesho hayo Bw. Yu Chong alisema, kwenye maonesho ya mwaka kesho wataalikwa wafanyabiashara wengi zaidi wa ununuzi, na kuongeza bidhaa bora za aina nyingi. Alisema serikali ya mji wa Qingdao imeamua kuwa itafanya maonesho makubwa na mazuri zaidi kila baada ya mwaka.

Idhaa ya kiswahili 2006-09-26