Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-26 10:39:30    
China yajenga mfumo wa upimaji kuhusu matetemeko ya ardhi kwenye bwawa la maji la Magenge Matatu

cri

Meneja mkuu wa kampuni ya uendelezaji wa mradi wa maji wa Magenge Matatu Bw. Li Yongan tarehe 21 mwezi huu alisema, takwimu za upimaji imethibitisha kuwa hivi sasa hali ya matetemeko ya ardhi yaliyotokea karibu na bwawa la maji la Magenge Matatu haikuzidi kiwango kilichosanifiwa, hata baada ya bwawa hilo kuwa na maji yenye kina cha mita 156, hali ya matetemeko ya ardhi pia itakuwa chini ya kiwango kilichosanifiwa.

Tarehe 20 mwezi huu bwawa la maji la Magenge Matatu liliingia kipindi cha kulimbikiza maji yenye kina cha mita 156, ili kusaidia ujenzi wa mradi wa maji wa Magenge Matatu, ambao ni wa kwanza kwa ukubwa duniani, serikali ya China ilijenga mfumo mkubwa wa kupima matetemeko ya ardhi kwenye sehemu ya bwawa ili kuhakikisha usalama wa bwawa hilo.

Mtafiti wa idara ya matetemeko ya ardhi ya mkoa wa Hubei, Bw. Gan Jiasi alisema kazi za upimaji kuhusu matetemeko ya ardhi yanayotokea kwenye sehemu ya bwawa la Magenge Mtatu ilianza mwaka 1959, na zilithibitishwa rasmi mwezi Julai mwaka 2001, hali hiyo ni nadra kuonekana katika historia ya ujenzi wa miradi ya uzalishaji umeme kwa nguvu za maji duniani. Rekodi za usimamizi katika miaka mingi iliyopita, zinaonesha kuwa matetemeko ya ardhi ya nyuzi 2 yaliyotokea kwenye sehemu ya bwawa la maji na pembezoni mwake yalikuwa machache sana, tena yalikuwa mbali na kingo za bwawa.

Baada ya ujenzi wa mradi wa maji wa Magenge Matatu kuzinduliwa rasmi mwaka 1994, kampuni ya Magenge Matatu iliiomba taasisi ya utafiti wa matetemeko ya ardhi ya idara ya matetemeko ya ardhi ya mkoa wa Hubei kuanzisha ujenzi wa mfumo wa upimaji wa matetemeko ya ardhi yanayosababishwa na bwawa la maji ya Magenge Matatu. Ili kusimamia na kutoa utabiri sahihi kuhusu matetemeko ya ardhi yanayosababishwa na bwawa baada ya kulimbikizwa maji mengi, mradi wa maji wa Magenge Matatu umejenga mfumo wa kisasa wa kutoa utabiri kuhusu matetemeko ya ardhi yanayosababishwa na bwawa la maji.

Mfumo wa upimaji kuhusu matetemeko ya ardhi ni pamoja na mfumo wa kupima matetemeko ya ardhi kutoka mbali kwa teknolojia ya kitarakimu, mfumo wa usimamizi kuhusu mabadiliko ya sehemu ya juu ya ardhi ya dunia, mfumo wa usimamizi wa hali ya maji yaliyoko chini ya ardhi na kituo cha takwimu ya mradi wa Magenge Matatu. Kati yake mfumo wa kupima matetemeko ya ardhi kutoka mbali kwa teknolojia ya kitarakimu una vituo 24 kuhusu upimaji wa matetemeko ya ardhi. Katika sehemu inayotiwa mkazo katika upimaji, matetemeko ya ardhi chini ya nyuzi 0.5 yanaweza kugunduliwa, na kuthibitishwa mahali halisi palipotokea tetemeko la ardhi.

Karibu na kingo za bwawa kuna visima 8, na kisima chenye kina kirefu zaidi kina urefu wa mita mia kadhaa ili kuona mabadiliko ya kina cha maji yaliyoko chini ya ardhi na mabadiliko ya kikemikali ya maji.

Mbali na mifumo 3 ya upimaji kuhusu matetemeko ya ardhi, mradi wa Magenge Matatu umeweka mpango wa upimaji wa matetemeko ya ardhi katika wakati wa dharura, pindi inapogundua tetemeko la ardhi kwenye sehemu ya bwawa, vitashirikishwa vituo vinne hadi vinane kwenye mfumo wa muda wa upimaji na kuongeza upimaji kuhusu matetemeko ya ardhi.

Wataalamu wanakadiria kuwa pamoja na kuongezeka kwa maji ya bwawa, matetemeko ya ardhi yataongezeka hatua kwa hatua, lakini matetemeko hayo ya ardhi hayo hayataleta uharibifu mkubwa. Aidha takwimu nyingi za upimaji kuhusu matetemeko ya ardhi, mabadiliko ya sehemu ya juu ya ardhi na upimaji katika visima, zinaonesha hivi sasa hakuna dalili za kutokea kwa matetemeko makubwa ya ardhi kiasi yanayoweza kuleta uharibifu mkubwa.

Idhaa ya kiswahili 2006-09-26