Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-27 19:19:09    
Mapishi ya kuku vitunguu maji na mafuta

cri

Mahitaji:

Kuku mmoja, vipande vya vitunguu maji, tangawizi, unga wa pilipili manga,chumvi, mvinyo wa kupikia, maji ya wanga

Njia:

1. osha kuku halafu mkaushe, paka chumvi, na mvinyo wa kupikia kwenye kuku na weka vipande vya vitunguu maji na tangawizi pamoja na kuku kwenye bakuli kubwa. Baada ya saa mbili weka kuku kwenye sufuria yenye maji, washa moto chemsha kwa mvuke kwa dakika 20.

2. kata kuku awe vipande, weka vipande vya vitunguu maji na tangawizi kwenye kuku na tia unga wa pilipili manga.

3. tia mafuta kwenye sufuria washa moto mpaka yawe na joto la nyuzi 80, mimina mafuta kwenye kuku, pasha moto tena na tia maji ya kuchemsha kuku mpaka ichemke, mimina maji ya wanga korogakoroga halafu mimina kwenye kuku. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-09-27