Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-09-27 19:22:06    
Baraza la uchumi duniani latoa taarifa kuhusu nguvu ya ushindani duniani

cri

Baraza la uchumi duniani, ambalo makao makuu yake makuu yako mjini Geneva, Uswisi, tarehe 26 mwezi huu lilitoa "taarifa kuhusu nguvu ya ushindani duniani katika kipindi cha mwaka 2006-2007", Uswisi kwa mara ya kwanza ilithibitishwa kuchukua nafasi ya kwanza kwa nguvu za ushindani duniani ikifuatiwa na Finland na Sweden.

Taarifa kuhusu nguvu ya ushindani duniani ya mwaka huu inahusisha nchi na 125, na ni mara ya kwanza kuhusisha nchi nyingi namna hii. Baraza la uchumi duniani lilipanga orodha hiyo kuhusu nguvu za ushindani duniani kutokana na takwimu zilizotolewa na nchi mbalimbali na mashirika ya kimataifa, pamoja na kufanya uchunguzi na kusikiliza maoni ya wasimamizi waandamizi wa kampuni. Orodha ya nguvu za ushindani iliyotolewa katika taarifa yake ya mwaka huu kutoka nafasi ya 4 hadi 12 ni Denmark, Singapore, Marekani, Japan, Ujerumani, Uholanzi, Uingereza, Hong Kong ya China na Norway. China iliwekwa katika nafasi ya 54, wakati India inachukua nafasi ya 43, Russia ya nafasi ya 62 na Brazil ambayo inachukua nafasi ya 66.

Mkurugenzi wa "mradi wa nguvu ya ushindani duniani" wa baraza la uchumi duniani Bw. Augusto Lopez-Claros alisema, kuchukua nafasi ya kwanza kwa Uswisi katika orodha ya nguvu ya ushindani duniani mwaka huu ni kutokana na kuwa nchi hiyo ilipata maendeleo makubwa katika kuinua ubora wa asasi za umma, idara za serikali ya Uswisi zina uwazi na ufanisi mkubwa katika uendeshaji kazi; licha ya hayo nchi hiyo imejenga msingi madhubuti katika utafiti wa kisayansi, viwanda na kampuni zilitoa misaada mingi ya fedha, tena zina ushirikiano mkubwa na vyuo vikuu na taasisi za utafiti wa kisayansi, hali ambayo inahimiza kwa nguvu maendeleo ya uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia.

Taarifa inasema ikilinganishwa na miaka kadhaa iliyopita, nafasi ya Marekani imerudi nyuma. Hali ya jumla ya kiwango cha teknolojia Marekani ni ya juu kabisa duniani, lakini hali yake katika maeneo mengine, hususan mazingira ya uchumi wa taifa siyo mazuri kabisa, ambayo yalipunguza sifa za teknolojia yake. Kutokana na taarifa hiyo, mazingira ya uchumi wa taifa ya Marekani yanachukua nafasi ya 69. Mapengo makubwa yaliyotokea katika biashara na mambo ya fedha ya nchi hiyo yamezorotesha uchumi wa taifa. Sekta ya kampuni ya kimataifa ilipohojiwa ilionesha wasiwasi kuhusu uchumi wa Marekani hususan hali ya kukosa uwiano katika mambo ya fedha ya umma. Aidha uendeshaji kazi wa idara za serikali za Marekani kuhusu maafa ya kimbunga cha Katrina kilichoikumba Marekani mwaka jana siyo ya kuridhisha.

Taarifa hiyo inasema kuna tofauti kubwa kati ya nchi za Ulaya, nchi za Ulaya ya kaskazini zinachukua nafasi za mbele kwa nguvu za ushindani duniani, taarifa inaona kuwa nchi hizo ni hodari katika usimamizi wa uchumi wa taifa, tena ubora wa asasi za umma za nchi hizo ni wa kiwango cha juu; mbali na hayo sekta ya kampuni na viwanda za binafsi pia inaonesha uhamasa mkubwa katika kutumia teknolojia ya kisasa na kuendeleza utamaduni mpya. Kwa kawaida, kutoza kodi kubwa kutaathiri nguvu za ushindani wa nchi, lakini uzoefu wa nchi za Ulaya ya kaskazini umetoa changamoto kwa maoni hayo ya jadi. Taarifa inaona jambo lililo muhimu siyo kuangalia kiwango cha kodi zinazokusanywa, bali ni matumizi ya fedha za kodi zilizokusanywa.

Nafasi za nchi kubwa za Ulaya zikiwemo Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Italia, zimerudi nyuma mwaka huu. Tunachukua mfano wa nchi ya Ufaransa, imerudi kwa nafasi 6 ikilinganishwa na ile ya mwaka jana. Chanzo chake licha ya kuwa nchi hiyo imekuwa na pengo kubwa zaidi katika mambo ya fedha, chanzo kingine muhimu ni kukosa unyumbufu katika soko la nguvukazi.

Taarifa inasema matatizo ya asasi za umma yanaendelea kukwamisha uchumi wa China; Licha ya hayo China inatakiwa kufanya haraka kuongeza ufanisi wa kazi za benki. Endapo matatizo hayo hatatatuliwa haraka, yataathiri ongezeko la nguvu za ushindani za China katika siku za baadaye. Katika miaka 27 iliyopita, taarifa iliyotolewa kila mwaka na baraza hilo kuhusu nguvu ya ushindani duniani iliwasaidia watunga sera na viongozi wa sekta za biashara za nchi mbalimbali katika ubunifu wa sera.

Idhaa ya Kiswahili 2006-09-27