Mwakilishi mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya kidiplomasia na sera za usalama Bw. Javier Solana na mwakilishi mkuu wa mazungumzo ya nyuklia wa Iran Bw. Ali Larijani tarehe 27 huko Berlin walifanya duru jipya la mazungumzo kuhusu suala la nyuklia la Iran, ambapo walijadili njia mpya yenye ufanisi ya utatuzi wa suala hilo. Mazungumzo hayo yalisimamishwa kwa muda baada ya kufanyika kwa saa tano, na pande hizo mbili ziliamua kuendelea na mchakato wa mazungumzo hayo tarehe 28. Wachambuzi walisema, kwa kuwa Bw. Solana ataamua kama ataendelea na mazungumzo na Iran au atalikabidhi suala hilo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na mazungumzo hayo, hivyo duru hilo la mazungumzo huenda ni duru la mazungmzo lenye "umuhimu mkubwa", ambalo litahusiana na mwelekeo wa suala la nyuklia la Iran.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika hoteli ya wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani iliyoko kwenye kitongoji cha Berlin. Baada ya mazungumzo semaji wa Bw. Solana alidokeza kuwa, mazungumzo hayo yalifanywa katika hali ya uangalifu. Wachambuzi waliona kuwa, kwa kuwa misimamo ya Iran na Marekani imekuwa na mabadiliko madogo hivi karibuni, hivyo bado kuna uwezekano wa kupata maendeleo, lakini sababu nyingi zisizo za uhakika zikiwemo misimamo ya pande hizo mbili isiyo ya uhakika kabla ya mazungumzo hayo zitayafanya mazungumzo hayo yawe na mabadiliko mengi.
Kwanza, msimamo wa Iran katika suala la kusimamisha shughuli za uranium nzito haueleweki. Kabla ya mazungumzo hayo, habari zilisema Bw. Larijani na Bw. Solana watazungumzia suala la kusimamisha shughuli za uranium nzito kwenye mazungumzo hayo. Gazeti la Washington Times la Marekani tarehe 26 lilisema, Iran karibu imekubali kusimamisha shughuli hizo kwa siku 90, ili kuweka mazingira kwa mazungumzo kati yake na nchi za Ulaya. Lakini serikali ya Iran ilikanusha kauli hiyo na kusema, kwenye mazungumzo hayo Bw. Larijani na Bw. Solana "hawatajadili mambo yanayohusiana na kusimamisha shughuli za uranium nzito". Ilisema "habari hizo hazina msingi hata kidogo, na wala haziwezi kusaidia utatuzi wa suala hilo." Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran tarehe 27 alitoa hotuba akisema, msimamo wa Iran kutumia kiamani nishati ya nyuklia haubadiliki. Lakini msemaji wa bunge la Iran Bw. Gholam Ali Hadad-Adel siku hiyo alipohojiwa na vyombo vya habari vya Iran alisema, "kama mazungumzo yataanzishwa tena, mada ya kusimamisha shughuli za uranium nzito unaweza kujadiliwa." Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Manochener Motaki kabla ya mazungumzo pia alitoa maelezo akisema, kuna mazingira ya maelewano kati ya Iran na Umoja wa Ulaya, hivyo kunaweza kuwa na matumaini kuhusu mazungumzo ya Berlin. Wachambuzi walieleza kuwa, katika hali ambayo shinikizo la kimataifa linaongezeka, uwezekano wa Iran kurudi nyuma.
Pili, msimamo wa Marekani ambayo ni muhimu katika suala la nyuklia la Iran unabadilika kidogo hivi karibuni. Kabla ya hapo Marekani ilisema, kama baraza la usalama halitafikia maoni ya pamoja kuhusu kuiwekea Iran vikwazo, Marekani itashirikiana na nchi muungano wake na kuunda "muungano wa kuweka vikwazo" ili kuiwekea Iran vikwazo bila idhini ya Umoja wa Mataifa. Lakini msimamo huo umebadilika. Rais George Bush wa Marekani na rais Jacques Chirac wa Ufaransa tarehe 20 walifanya mazungumzo. Baada ya mazungumzo walisema, walipata msimamo wa pamoja kuhusu suala la nyuklia la Iran, yaani Ufaransa na Marekani zinaitaka Iran isimamishe shughuli za uranium nzito, pia ziliamua kutoweka vikwazo kwa Iran kwa muda. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bibi Condoleezza Rice tarehe 27 aliongea kwa simu na Bw. Solana, akiunga mkono mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Iran. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Bw. Sean McCormack siku hiyo alisema, baada ya maduru kadhaa ya mazungumzo, pande mbalimbali zi\naweza kupata maendeleo katika suala hilo. Wachambuzi wanasema, Marekani inapenda kuzipa nchi za Ulaya muda ili kuishawishi Iran isimamishe shughuli za uranium nzito, na kuanzisha tena mazungumzo ya mpango wa nyuklia wa Iran. Mabadiliko hayo ya msimamo wa Marekani yanatoa watu matumaini fulani.
Wachambuzi wanasema, katika juhudi za jumuiya ya kimataifa, mchakato wa kutatua suala la nyuklia la Iran kwa njia ya mazungumzo haukatishwi siku zote. Watu wanatumai kuwa baada ya mazungumzo ya siku 2, Bw. Solana na Bw. Larijani watapata maendeleo fulani ili kutafuta njia mpya ya kutatua suala hilo.
Idhaa ya Kiswahili 2006-09-28
|