Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-02 19:17:03    
Matembezi kwenye sehemu ya vijiji na mapumziko kwa shughuli za kiutamaduni yapendwa zaidi na watalii wakati wa sikukuu

cri

Tarehe 1 mwezi Oktoba mwaka huu ni siku ya kutimia miaka 57 tangu Jamhuri ya watu wa China iasisiwe, ambapo watu wa China wanapata likizo ya wiki moja, hivyo sehemu mbalimbali zimeanzisha shughuli mbalimbali za utalii zikiwemo za masafa ya wastani na mafupi, kutalii kwa kuendesha gari mwenyewe, matembezi kwenye sehemu ya vijiji na mapumziko kwa shughuli za kiutamaduni. Wilaya zote za mji wa Tianjin zilianzisha shughuli za kutembelea sehemu ya vijiji kwa kuunganisha na kuboresha rasilimali za utalii kwenye sehemu ya vijiji pamoja na miradi iliyoanzishwa hivi karibuni ya kutembelea sehemu ya vijiji zikiwemo Shamba la Longshun, Furaha ya wakulima, Ukoo wa wakulima hukoe Daliutan, shamba la majaribio la kilimo ya teknolojia ya kisasa na shamba la Xinsan.

Mji wa Shanghai umeandaa maandamano ya magari yaliyopambwa kwa maua barabarani, siku ya China ya Yuyuan, tamasha ya kimataifa ya muziki na urushaji fashifashi, sherehe ya harusi ya waridi matuta ya maua kwenye bustani ya Shiji na wiki ya utamaduni ya ngoma ya mashariki, shughuli hizo na mahali hapo pamekuwa panapendwa na wakazi wa Shanghai katika likizo ya siku ya taifa.

Mji wa Wuxi umeanzisha shughuli za utalii za mapumziko kwenye nyumba za wakulima, matembezi ya kupumzika ya likizo pamoja na shughuli za kiutamaduni za kufurahia majira ya mpukutiko, ambazo zinapendwa zaidi na wakazi wa mji wa Wuxi.

Mkoa wa Fujian ulioko kusini mashariki mwa China pia umejiandaa kwa mambo yake maalumu ya kuwafurahisha wageni waliotoka sehemu mbalimbali. Kwa kuwa huko ni karibu sana na Taiwan, mkoa huo ulijenga nyumba ya maonesho ya vipepeo la Taiwan kwenye uwanja wa jumba la kijiolojia la ziwa na Dajin, ambapo vinaoneshwa vielelezo vya aina zaidi ya 1,000 vya vipepeo. Kiongozi wa jumba la maonesho ya vipepeo Bibi Wu Juxiang alisema, kwa kuwa ziwa na Dajin liko karibu na ziwa la Riyue la Taiwan, na maji yake na milima iliyoko kule ni mizuri sana, kwa hiyo watu wengi wanakwenda kuangalia vipepeo katika siku za mapumziko.

Wakazi wa mtaa wa Hongqi wa mji wa Ganzhou, mkoani Jiangxi, walifanya maonesho ya mavazi. Wachezaji waliofanya maonesho kwenye jukwaa, waliovaa mavazi yenye umaalumu wa kikabila waliwavutia wakazi wa huko mia kadhaa. Kiongozi wa kikundi cha sanaa cha mtaa huo bibi Wang alisema, watu wanapenda kufanya shughuli wanazopenda katika likizo la siku ya taifa na kuonesha maisha yao mazuri.

Idhaa ya Kiswahili 2006-10-02