Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-10-03 19:56:24    
Watu wapenda "wiki ya dhahabu"

cri

Mkurugenzi mtendaji wa ofisi inayoshughulikia mambo ya likizo ya serikali ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa idara ya utalii ya China Bw. Wang Zhifa, tarehe 28 mwezi Septemba alipohojiwa na mwandishi wa habari alisema, katika mazingira ya hivi sasa ambayo utaratibu wa mapumziko haujakamilika, utekelezaji wa utaratibu wa "wiki ya dhahabu" unahakikisha haki ya mapumziko ya wafanyakazi wa kawaida na kuungwa mkono na umma.

Ofisa huyu alisema uchunguzi uliofanywa na ofisi ya mambo ya likizo ya serikali kwa njia ya televisheni ya serikali kuu unaonesha kuwa, zaidi ya 50% ya watu waliohojiwa wanaona hatua zilizochukuliwa kuhusu "wiki ya dhahabu" zimeboreshwa, na zaidi ya 60% ya watu waliohojiwa wameweka mpango wa kufanya matembezi katika kipindi cha likizo ya siku ya taifa, hii inaonesha kuwa umma unahitaji "wiki ya dhahabu".

Bw. Wang Zhifa alisema mchango mkubwa iliotolewa na "wiki ya dhahabu" ni kuhimiza matumizi ya nchini na maendeleo ya uchumi. Utekelezaji wa utaratibu wa "wiki ya dhahabu" unashawishi watu kufanya matembezi katika sehemu nyingine na kuboresha maisha ya watu. Hivi sasa ingawa kuna mgongano kati ya huduma na mahitaji katika "wiki ya dhahabu", ambao umehimiza ubora wa shughuli za utalii za watu, lakini uchunguzi uliofanywa na idara ya utalii ya taifa unaonesha kuwa, watu wanahitaji kupata muda wa kufanya utalii kutokana na utaratibu wa "wiki ya dhahabu".

Bw. Wang amekadiria kuwa soko la utalii mwaka huu litakuwa na maendeleo tulivu, utalii wa mapumziko utakuwa kitu cha kwanza kinachochaguliwa na watu, na utalii wa sehemu ya vijiji na utalii wa utamaduni wa mijini umeanza kupendwa na watu wengi. Shughuli za "wiki ya dhahabu" zilianza mapema na zitachelewa kumalizika kutokana na kuwa siku ya taifa ni karibu sana na sikukuu ya jadi ya mwezi katika mwaka huu.

Alisema kwa ufupi matatizo yaliyoonekana katika "wiki ya dhahabu" ni mawili; la kwanza ni halaiki ya watu na msongamano wa magari, huduma za utalii zilishindwa kukidhi mahitaji ya watu hususan katika miji inayotembelewa na watu wengi na sehemu zenye mandhari nzuri. La pili ni kuwa matatizo yanayohatarisha usalama na huduma hafifu. Kwa mfano kulitokea ugomvi na ajali katika shughuli za utalii, pamoja na malalamiko kutoka kwa watalii.

Kuhusu matatizo hayo, "wiki ya dhahabu" ya tarehe 1 Oktoba mwaka huu ilisisitiza kazi 4: Ya kwanza ni kuboresha huduma ya mawasiliano ya habari kwa umma, na kupunguza mgongano kati ya huduma na mahitaji. Hususan kutoa makadirio kuhusu soko la utalii kabla ya kuwadia kwa "wiki ya dhahabu", kuongeza shughuli mpya za utalii na kutangaza habari hizo kwa watu wengi kwa njia za radio, televisheni, magazeti na Internet ili kufanya watu wengi wapate habari kuhusu soko la utalii na kuweza kufanya uchaguzi mwafaka.

Pili, kuimarisha usimamizi wa usalama na kuhakikisha usalama wa watalii, hususan kuzuia ajali za barabarani zisitokee katika shughuli za utalii.

Tatu, kuimarisha ushirikiano wa idara husika, na kuinua kiwango cha huduma ya serikali kwa umma. Baraza la uratibu wa utalii na mambo ya likizo ya kitaifa la ngazi ya wizara lina wanachama 18, kila mmoja anabeba jukumu lake maalumu na kupanga wafanyakazi maalumu kushika zamu kwa saa 24 ili kusikiliza malalamiko ya watalii, kushughulikia matukio ya dharura na kuhakikisha kuwa shughuli za "wiki ya dhahabu" zinaendeshwa kwa utaratibu mzuri.

Ya nne, ni kuinua ustaarabu wa utalii wa umma, kuanzisha hali ya kuhimizana kati ya huduma ya uaminifu na utalii wa ustaarabu pamoja na mazingira bora ya "wiki ya dhahabu".

Idhaa ya Kiswahili 2006-10-03